Wakili Jebra Kambole: Mtu Mzalendo ni yule anayependa Nchi yake na siyo Serikali yake


Wakili Jebra

Nakubaliana nawe katika hayo maelezo yako. Ni kweli kuwa, hakuna mtu muungwana ambaye anaweza kusimama hadharani na kusema wazi kuwa anakubaliana na uongozi wa udhalimu kwa watu wake. Vivyo hivyo kwa taifa pia. Ikumbukwe hata Jamhuri ya Tanzania miaka ya 1970 ili laani vikali utawala wa kimabavu/kidhalimu wa Iddi Amin nchini Uganda n.k ili kutekeleza kwa vitendo na kuwaambia dunia wazi wazi kuwa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi na watanzania wote, hata siku moja haikubaliani na matendo ya kidhalimu, unyonyaji na uonevu dhidi ya binadamu. Na hivyo ndivyo ilivyo hata sasa katika Tanzania ya zama hizi.

Narudia kwa kusisitiza kwamba, si Tanzania, wala CCM ya sasa, au watanzania hawa ambao wanaweza kukubaliana na vitendo vya utawala wa kidhalimu kwa wananchi: Ama nje ya nchi au ndani ya nchi.
 
Hapo unaona upinzani kwenye hoja? Kweli tuna Muroto wengi nchi hii..ukiweka kofia kichwani, kofia ndio yenye akili kuliko wewe...bogus
Ndugu mleta mada Tafadhali badilisha jina unalotumia. Uhilitendei haki hilo jina, habari zako zinapendelea upande mmoja.
Afadhali Ungejiita MWANAHABARI MPINZANI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja ya kambole dhaifu mno Ana upeo mdogo serikali kuipenda hata ya ya Idd Amin au ya makaburu mtu aweza ipenda kutegemea mahusiano aliyonayo na faida anayopata kwenye hiyo serikali. kwa mfano mfanyabiashara umepewa tenda ya ku supply mafuta kwa magari yote ya serikali huwezi acha kuipenda.Nadhani angesema baadhi.Sisi tulipovunja uhusiano na makaburu waarabu walikuwa na uhusiano nao na kuwauzia mafuta Kama kawaida.Mtu kupenda serikali hutegemea maslahi anayopata iwe ya kidemokrasia au la.
 
Huwezi kulipenda Taifa lako bila kuipenda serikali yako,sababu Taifa ndio linakuwa limeichagua serikali iliyoko madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuipenda nchi yako hakuna MJADALA.... By the way, tuna wimbo unaoimbwa,... TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE...

Kuichagua serikali si lazima uipende... Kuipenda kunatokana na matendo ya serikali kwa wananchi wake baada ya kuichagua... Udikteta etc
 
Back
Top Bottom