Wakili: DOWANS itadhoofisha nchi

Huyu jamaa amesoma hiyo hukumu mara saba kwa sababu ana instructions za kumuwakilisha boss wake RA na hata sasa hivi ana kesi ya Dowans iliyo mahakama ya biashara na ambayo aniendesha yeye kwa niaba ya Dowans. maoni yake hayawezi kuchukuliwa kwamba ni ya mtu independent na asiye na interest. Yeye anatishia ili apate fee note yake.

Halafu hii tabia ya kumuita wakili kuwa ni MAARUFU sijui ni kwa kutumia vigezo gani. Kuna kesi gani yenye public interest amewahi kuiendesha akaishinda? Mimi najua umaarufu wa huyu jamaa na forgery na kuhonga honga. Hata wakati mmoja aliwahi kushtakiwa mahakama ya kisutu kwa kughushi hukumu ili ionekane ilitolewa na mahakama kumbe aliitayarisha yeye na kumpelekea mteja aliyeko Marekani.
 
RA anapiga kross na kufunga mwenyewe.Anatumia watu wenye njaa kuhalalisha uporaji wa mali ya wanyonge.Jamani ni wakati wa kuundwa kwa tume huru kuchunguza suala lote la hii kesi.
Kwanza inaelekea hata mashahidi wetu walikuwa kitu kimoja na Dowan kwani RA amekuwa akijificha nyuma ya pazia na kuendesha upande wa serikali na huo wa Dowan.Siamini kama alishindwa kuwa-influence in his favaour.
Pili ni Rex Attorney ya Balozi wa Tanzania USA Mwanaidi Maajar,rafiki wa JK tokea wakiwa UDSM kwenye uongozi wa MUWATA.Ukaribu wake na dola ambayo nayo ilikuwa si safi kwenye deal yote hii unatia mashaka kwani mteja wake alikuwa akipendelea ashindwe badala ya kushinda.
Fungamtama amekiuka maadilio ya uwakili kuwa mpiga debe kwenye kesi ambayo mhusika ana mahusiano naye.
TLS bila shaka mtachukua hatua kuokoa taaluma tukufu.
 
1. Hizi hoja za huyu wakili mbona zinaonekana nipersonal attack kwa Sitta zaidi ya kujenga hoja kwa nini Dowans ilipwe. Kwa utaratiobu uliopo Tanzania miaka hii huyu jamaa ana interest gani hapa?
Mimi naamini kabisa kwamba tumekaribia kuwalipua akina Rostam na wenzie, na tutakapofanikiwa, nchi hii italipwa fidia. Kutozwa fidia ndicho hawa mafisadi wanachoogopa. Mbinu wanayotumia sasa ni kuutisha umma.

Hebu tizama intro ya ICC:
What is ICC?
"Setting rules and standards
Arbitration under the rules of the ICC International Court of Arbitration is on the increase. Since 1999, the Court has received new cases at a rate of more than 500 a year."
Swali kwa fisadi Bw. Kennedy Fungamtama - Je, kwa idadi hiyo hapo juu ya kesi 500 kwa mwaka huko ICC, ni taifa gani mpaka sasa limedhoofishwa na kujikuta kwenye matatizo makubwa?
 
Kwa maneno mengine, Tanzania inatakiwa ipeleke kesi nyingine zisizopungua 6 huko ICC kabla ya mwaka kuisha. Huu mbona ni mwanzo tu Bw. Fungamitama?!
 
Fungamtame amesoma hukumu kwa kutafuta vipengele vya kuibeba DOWANS kwanini asituonyeshe vipengele vya kuishinda DOWANS. Naamini mawakili ni wazuri wa kutafuta weakness and wanaweza leta ushindi katika hali ngumu pasipo tarajiwa na watu kwanini hawakuwa motivated hivi?

Kama tutawalipa DOWANS before kuwalipa wote waliosababisha hasara wafukuzwe kwenye ofisi za umma, wasipewe pension na malipo yao stahiki ( Wastaafishwe kwa maslahi ya Umma) na mawakili wote wlioisimamia serikali wasipewe kazi popote Tanzania
 
Hao ndo wasomi wetu.Kama kuwa na wasomi wengi katika serikali ndo kuleta maendeleo basi tungekuwa mbele kiuchumu. Nchi yetu imejaa PHDs and Maprofesa lakini hakuna wanachokifanya. Labda sababu walisoma kwa shida ndoo wanalipiza kisasi! Aaaaaah! Inaudhi sana.
 
wakili: Dowans itadhohofisha nchi

• ataja mashahidi walioiponza tanesco icc

na happiness katabazi



mmoja wa mawakili mahiri wa kujitegemea nchini, kennedy fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa spika wa bunge, samuel sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 kampuni ya kuzalisha umeme ya dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.

fungamtama aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na tanzania daima yaliyofanyika ofisini kwake jijini dar es salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti hili kupata taarifa kuwa wakili huyo ni miongoni mwa wanasheria walioisoma hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya uwekezaji (icc).

mwanasheria huyo ambaye alimuelezea sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya icc, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili.

alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.

wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si waziri sitta binafsi.

fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma na kujiridhisha kwamba hukumu hiyo yenye kurasa 150 ya kesi namba 15947/vro kati ya kampuni ya dowans na tanesco ilipokewa na icc novemba 20, mwaka 2008 na ikatolewa hukumu novemba 15 mwaka jana.

alisema mkataba kati ya tanesco na dowans ulisainiwa juni 23, mwaka 2006 na mkataba huo unajulikana kama ‘power off - take aggreement (poa)” chini ya kifungu cha 14 (e) cha poa, na kufafanua kwamba pande zote mbili katika mkataba huo zilikubaliana kwamba uamuzi wa mahakama ya icc ndio utakuwa wa mwisho na utazibana pande zote mbili na hautaweza kukatiwa rufaa.

fungamtama alisema kifungu cha 14 (f) cha poa, kinasomeka: “the parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability of this arbitration agreement or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this section.”

kwa tafsiri nyepesi, fungamtama alisema kifungu hicho kinasema, tanesco na dowans katika mkataba wao walikubaliana kwa maandishi kuweka kando haki za kupinga au kuhoji mwenendo na tuzo zitakazotolewa na baraza la usuluhishi.

alisema waziri sitta amenukuliwa na vyombo vya habari akitaka serikali itumie kifungu cha 16 cha sheria ya tanzania ya usuluhishi sura ya 15 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwamba serikali inaweza kutumia kifungu hicho kutengua hukumu ya mahakama ile ya kimataifa.
“ni kweli mahakama kuu ya tanzania imepewa mamlaka ya kutengua maamuzi yanayotolewa na mahakama za kimataifa endapo tu itadhihirika kuwapo kwa mambo mawili yafuatayo:
Moja; msuluhishi wakati akiendesha kesi alikuwa akiegemea na kupendelea upande mmoja (arbitrator has miss - conducted himself. pili: mazingira ya kufikia uamuzi ule yalitawaliwa na rushwa au shauri lilifikishwa mahakamani bila kufuata taratibu za kisheria (an arbitration or award has been improperly procured).



“hayo ndiyo mambo mawili peke yake yanayoweza kusababisha mahakama kuu ya hapa nchini kutengua hukumu zilizokwisha kutolewa na mahakama za kimataifa za usuluhishi na si kwa jambo jingine lolote.

“sasa kama sitta ana ushahidi, vigezo hivyo viwili vya kisheria katika lililokuwa shauri baina ya dowans na tanesco kwamba wasuluhishi wale ambao ni majaji waliipendelea dawans, au walikura rushwa, ingekuwa ni vyema haraka apeleke ushahidi huo kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili aweze kuwatuma wanasheria wake wakafungue kesi mahakama kuu ili iweze kutengua hukumu hiyo kupitia huo ushahidi wake kama anao na si kama anavyofanya hivi sasa kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari,” alisema wakili huyo.
aidha, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha jedwali la 3 katika sheria ya usuluhishi ya tanzania, sura ya 15 ya mwaka 2002 kinasomeka hivi:

“each contract state undertakes to ensure the execution by its authorities and in accordance with the provisions of its national laws of arbitrarily awards made in its own territory under the preceding articles”.


“kwa tafsiri rahisi, kifungu hicho utaona tayari nchi imejifunga mikono na utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama za kimataifa kwa sababu ni nchi yetu yenyewe imeridhia sheria na mikataba ya kimataifa.”

alisema kwa hiyo maelezo ya waziri sitta ya kutaka dowans isilipwe, ni kutaka kuishawishi serikali na umma kukaidi kutekeleza maamuzi halali chini ya sheria na mikataba ambayo serikali iliiridhia kuitii na kuitekeleza.

aidha, alisema jambo jingine lililojitokeza wakati kesi hiyo ikiendelea baina ya dowans na tanesco ni tanesco walitaka kujua wamiliki wa dowans ni kina nani na mahakama ya icc iliona hoja hiyo ya tanesco ya kutaka kumjua mmiliki haina umuhimu wowote katika mgogoro uliokuwa mbele yao na ikatupilia mbali, kwa sababu iliona hoja hiyo haina maana yoyote mbele yao.

“kwa hiyo kwa kitendo cha waziri sitta kulianzisha suala hilo la kutaka kujua wamiliki wa dowans wakati hoja hiyo tayari ilikwishatolewa uamuzi na icc, kisheria hawezi kulianzisha tena jambo hilo la kutaka kujua wamiliki kwa njia anayoitumia ya vyombo vya habari.

“kwa hiyo maelezo yote yanayoendelea kutolewa kuhusu hukumu hiyo ni kutaka kujinasua katika lawama wakati yeye na baadhi ya maswahiba zake enzi zile akiwa spika wa bunge ndio waliokuwa chanzo cha tanesco kuvunja mkataba na dowans, hivyo mwisho wa siku shirika hilo la umeme kujikuta likiburuzwa katika korti ya icc.

“na ifike mahala wananchi na vyombo vya habari na serikali itoke usingizini na ijiulize maswali yafuatayo kwamba sitta hakuwepo kwenye usikilizwaji wa shauri hilo? Sitta hakuwa akijua kwamba tanesco imefunguliwa kesi na dowans katika mahakama ya icc?

“kwa kuwa sitta alikuwa mstari wa mbele kuzipiga vita dowans na richmond, ni wazi alikuwa akifahamu kwamba tanesco imeburuzwa mahakamani na kama kweli sitta ni mzalendo wa kweli na hana chuki binafsi katika hili ni kwanini hayo madai anayoyasema asingeiomba serikali imuweke kama shahidi wa upande wa tanesco ili akatoe ushahidi anaousema kila kukicha kwenye vyombo vya habari?

“amesubiri tayari shirika letu la umeme ambalo ndilo lilikuwa mdaiwa katika shauri hili limeshindwa kufurukuta kwenye kesi hiyo na tumetakiwa tulipe kiasi hicho kikubwa cha fidia ndiyo kila kukicha anazungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo,

tena ukitazama maoni anayoyatoa utafikiri si mtu aliyesomea sheria kabisa….naomba sana hasa serikali ipuuze ushauri wa sitta kwani ni wazi kabisa anataka kuliingiza taifa kwenye matatizo mengine makubwa.

“watanzania na huyo waziri sitta ambao hawajaisoma hukumu ile naomba niwaeleze wazi mimi nimeisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba, kama taifa kupitia hukumu hiyo tumeshikwa pabaya, hivyo hatuwezi kukata rufaa, isipokuwa tu kama tutathibitisha sababu zile mbili nilizozitaja,” alisema wakili fungamtama.

aidha, fungamtama aliviasa baadhi ya vikundi mbalimbali vya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuzungumzia hukumu hiyo ambayo hata wengine hawajawahi kuisoma wala kuiona, kwani tayari kuna baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika makala kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa tanesco haijawahi kuleta shahidi hata mmoja kutoa ushahidi.

jambo ambalo fungamtama alisema si kweli na linalenga kuhadaa umma, kwani majibu na nakala ya hukumu hiyo ambayo anayo inaonyesha tanesco ilipeleka mashahidi watano na walitoa ushahidi wao. wakili huyo aliwataja mashahidi hao kuwa ni subira wandiba, ambaye ni mwanasheria wa tanesco, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya zabuni iliyotoa tenda kwa dowans, balozi fulgence kazaura, ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa tanesco, dk. Idrisa rashid, mhasibu mkuu wa shirika hilo, jamhuri ngeline na boniface njombe.

my take:


1. Hizi hoja za huyu wakili mbona zinaonekana nipersonal attack kwa sitta zaidi ya kujenga hoja kwa nini dowans ilipwe. Kwa utaratiobu uliopo tanzania miaka hii huyu jamaa ana interest gani hapa?

2.
mbona tanzania imeridhia kufuata haki za binadamu katika medani hiyo hiyo ya kimataifa na haifuati kama tulivyoona wiki iliyopita arusha, je tumenyyimwa misaada? N hii concept ya misaada misaada mbona tumegota hapa tutatoka linni? Na ni wafadhili gani wanafurahia kuona hela za walipa kodi wao wanalipwa matapeli?


ndugu yangu mbona inaonekana kama umetumwa, nafikiri sitta yuko sahihi katika kifungu alichotaka tanzania ikitumie kukwepa kulipa fedha hizo kwa kuwa iliwezekana vili kesi ifantike pasipo anayedai kuwa nafahamika hivyo ni wazi kuwa ulikuwepo upendeleo.

Nataka pia wakili huyu akumbuke kuwa fisadi karamagi ndiye aliyeishinika tanesco kuhuisha mkataba wa kampuni feki ya richmond kwa dowans tena wakati makali ya upungufu wa umeme yakiwa yameisha
.
 
Kataeni kuwalipa muone yatayojiri. Mlishinikiza kuvunja mkataba sasa matokeo mnayaona.

Nyerere alijidai kuwataifisha LONRHO, ingawa taifisha yake ya Ma Benki na Mashamba Na Viwanda vya wazungu ilikuwa ya geresha kwani wote alikuwa akiwalipa, wote walilipwa, wasiolipwa ni waIslam tu waliokuwa na mali zao. Akajidai kuwalipa LONRHO anavyotaka yeye, mbona ilimtokea puani! Jee hamkumbuki? Kama wengi wenu hamkuwepo wakati huo, m-google mtazipata data.

Sasa haya ya Dowans tunapiga kelele na madudu tumefanya wenyewe, huwezi kuvunja mkataba na mtu aliyekwisha kuingia hasara ya kukuletea mlivyo ahidiana, labda viwe chini ya kiwango mlichokubaliana au viwe vibovu au awe hajavileta kabisa. Lakini hakuna sababu nyengine yoyote utayoitowa ukashinda, mahakama yoyote duniani labda iwe haifati haki.

Hili La Dowans, tutapiga kelele weee, at the end lazima lilipwe.



Acha uwongo.
AFRICA: Bye-Bye for Tiny Rowland

Monday, Jun. 19, 1978






An industrialist gets burned at Rhodesian liberation politics
He has been described as a modern-day Cecil Rhodes. If anything, comparison with the great 19th century imperialist understates the restless, driving ambition and material success of Roland ("Tiny") Rowland, 60, chief executive of the London-based conglomerate Lonrho, Ltd. Rowland has transformed a small initial stake in Africa into one of the continent's biggest commercial empires. Among his friends are Presidents Kenneth Kaunda of Zambia, Mobutu Sese Seko of Zaïre, Hastings Kamuzu Banda of Malawi and Jomo Kenyatta of Kenya -not to mention Prime Minister Ian Smith of Rhodesia.
Last week Tiny Rowland came a cropper at one of his favorite vocations:meddling in the politics of black majority rule in Rhodesia. Not only does Lonrho have vast investments in the breakaway British colony but Rowland has friends-favored ones-both among the leaders involved in Smith's "internal settlement" and among the Patriotic Front leaders who are fighting them. The industrialist's immediate problem, however, lay in nearby Tanzania, where the socialist government of President Julius Nyerere announced plans to nationalize Lonrho's 18 local affiliates.
Ostensibly, the reason for the takeover was that Lonrho had been evading the United Nations' economic sanctions against Rhodesia (which black African leaders refer to as Zimbabwe). In fact, the move was an irritated response by Nyerere, a prominent backer of the Patriotic Front, to Rowland's ambiguous dealings with both sides in the delicate Rhodesian situation.
Rhodesia has a special meaning for Rowland: it is where the India-born entrepreneur got his start. Emigrating from London to Salisbury in 1948, Rowland used a small fortune acquired from a local Mercedes-Benz dealership to buy up 30% of Lonrho in 1961; at that time it was a sleepy ranching and mining company known as London and Rhodesian Mining and Land Co. Ltd. He then embarked on a strategy of befriending black nationalist leaders on the way to furthering his business interests. It paid off: Lonrho's holdings now include an estimated 1 million acres of Rhodesian land and substantial concessions, sugar and tea plantations in Malawi, textile mills in the Ivory Coast, newspapers, copper mines and breweries in Zambia, coal, platinum and copper mines in South Africa, and the continent's largest auto dealership (selling, in addition to Mercedes, Ford and Toyota cars). The company has diversified far beyond Africa, employing 100,000 people in 600 subsidiaries in 43 countries.
Ever since U.N. sanctions were imposed on Rhodesia in 1965, Lonrho's Rhodesian subsidiaries have operated -theoretically, at least-at arm's length from the parent firm. Rowland, who for years has known virtually all of the country's political leaders, black and white, seems to be obsessed with finding a workable solution to the political dilemma. Says one of his London business colleagues: "There is a messianic streak in Tiny's makeup that he, and he alone, can solve the Rhodesian problem."







Read more: AFRICA: Bye-Bye for Tiny Rowland - TIME
 
Jitu zima linahofia misaada utadhani hiyo inayoitwa misaada inatusaidia chochote. Kwa taarifa yake wakoloni wataendelea kutoa hiyo anayoamini kuwa ni misaada hata ikiwaje kwa vile kwao haimaanishi misaada zaidi ya utapeli tu
 
Ostensibly, the reason for the takeover was that Lonrho had been evading the United Nations' economic sanctions against Rhodesia


And of course this was the matter, na JKN kama mwanamapinduzi katika kulikomboa bara la Afrika kutoka kwa wakoloni by then he had to do something on this! Inashangaza kuona huyu ndugu yetu Zoba yuko bize kufananisha Lonrho na Dowans wakati situations, times, na hata interested parties ni completely different.
 
Watu kama Fungamata ndio wale ambao wapo tayari wam'sacrifice mke wake wa ndoa kwa kibosile ili apate msaada wa kifedha.
 
Hapa kuna mambo mawili ya wazi:

1. Wakili huyu ni dhahiri kapewa pesa na Rostam atetee uamuzi wa serikali kuilipa Dowans na kumshutumu Sitta

2. Gazeti la Tanzania Daima linaendelea kutumiwa na Rostam Aziz/Edward Lowassa kueneza propaganda kutokana na mhariri wake kuwa kwenye payroll ya mafisadi hawa.
 
HATA KAMA SINA UTAALAMU WA SHERIA LAKINI WANASHERIA WATANZANIA WENYE UCHU WA NCHI YAO WANASEMA KUWA HAKUNA HAJA YA KULIPA KAMPUNI AMBAYO YAINA WAMILIKI.. SASA NINI HUYU JAMAA ANASEMA???

SITTA NI MWANASHERIA, MWAKYEMBE NI DAKTARI WA SHERIA HAWA WOTE WANASEMA SIYO SAHIHI IWEJE HUYU Kennedy Fungamtama, Aseme tulipe??

Tutasimama na wananchi wenye mapenzi mema na wacha tusilipe halafu tuone hiyo misaada tutakayokosa kutoka kwa wafadhili..
 
Jamani mi niko ignorant kidogo na maswala ya TIC na BRELA kwa ujumla kuhusu usajili wa kampuni za nje Tanzania.

Kutokana na list iliyotajwa ya wamiliki wa Dowans kutoka BRELA, kama sijakosea, wote ni watu kutoka nje ya Tanzania.

Hivi inawezekana kweli kampuni ikasajiliwa BRELA ikiwa na wamiliki wote sio watanzania??? au inatakiwa atleast kuwepo na share holder mmoja ambaye ni Mtanzania????

Jamani naomba mnisaidie kwenye hili...

Sheria ya Makampuni ya mwaka 2002 kama ilivyokuwa ya zamani haiweki masharti ya wanahisa wa kampuni kuwa raia au residents wa Tanzania wala kwa kampuni yenye hisa katika kampuni hiyo kuwa domiciled Tanzania. Hata wakurugenzi wanaweza wote kutoka nje ili mradi awepo ofisa mmoja mkazi wa Tanzania. Hilo kwa maoni yangu ni moja kati ya mapungufu katika sheria zetu za makampuni na uwekezaji ambayo yanahitaji kuondolewa.

Kwa kuliona hili Sheria ya Adhi inayatoa makampuni ambayo wanahisa wake wengi ni wageni kuwa kampuni ya kitanzania kwa lengo la umilikaji wa Ardhi. Ningeshauri Sheria ya Makampuni irekebishwe kwa kuweka masharti ya kuwepo japokuwa mkurugenzi mmoja katika kila kampuni ambaye ni raia wa Tanzania
 
Hapa kuna mambo mawili ya wazi:

1. Wakili huyu ni dhahiri kapewa pesa na Rostam atetee uamuzi wa serikali kuilipa Dowans na kumshutumu Sitta

2. Gazeti la Tanzania Daima linaendelea kutumiwa na Rostam Aziz/Edward Lowassa kueneza propaganda kutokana na mhariri wake kuwa kwenye payroll ya mafisadi hawa.

That is strange.Lakini hii imemu-expose huyo Fungamtama and the one who is behind him.
 
Mimi sijabahatika kupata nakala ya uamuzi huo. Nimesikiliza hoja za Mh. Ngeleja, Sita na DR Mwakyembe kuhusiana na suala hili na pia nimewasikiliza wataalamu mbalimbali wa sheria kama akina Nshalla, Jaji Bomani na sasa Fungamtama. Wote kwa pamoja ukisikiliza hoja zao wanakubali kwamba kwa mujibu wa mkataba pande zote mbili walikubaliana kufungwa na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhisi na kwamba maamuzi yao yatakuwa ya mwisho. Tofauti inayojitokeza kati ya kundi la Mh. Ngeleja na Mh. Sita ni juu ya uamuzi wa kulipa bila kujaribu kutumia njia nyingine kupinga uamuzi huu. Ni dhahiri kwa mujibu wa pande zote mbili kwamba hiyo njia nyingine haiwezi kuwa Rufaa kwakuwa kwa mujibu wa mkataba haki ya Rufaa haipo. Kuna mianya mitatu tu ya kuweza kupinga uamuzi huo. Ya kwanza ni kama uamuzi ulipatikana kwa rushwa, pili kama waamuzi hawakuwa huru katika uamuzi wao na tatu kama hiyo tuzo ilipatikana kinyume cha taratibu (improperly procured). Kwa mujibu wa Nshalla na Mh Sita na DR Mwakyembe bado kuna uwezekano wa kuipinga tuzo kwa kutoa hoja kwamba tuzo ilipatikana kwa udanganyifu kwa kuwa mkataba uliyotokana na kampuni hewa hauwezi kuwa umepatikana kwa njia isiyo ya udanganyifu (SITA na MWAKYEMBE). Kwamba tuzo haikupatikana katika utaratibu sahihi maana Mahakama ilipogundua kwamba Mkataba ulikiuka Sheria ya Ugavi ilipaswa kutamka kwamba mkataba huo ulikuwa batiri toka katika mizizi yake. Mengi yanaweza kusema katika hili. Sijasoma Tuzo kujua kama hoja hizi zilijitokeza na kutolewa maamuzi au la.

Lakin kwa hali ya kawaida suala la Tuzo kupatikana kwa udanganyifu ni suala la kimantiki na ukweli wa mambo. Haliwezi kuthibitika kwa assumption tu bila kuwepo ushahidi uliyodhahiri. Suala la Tuzo kuwa improperly procured ni suala la mchanganyiko wa sheria na mantiki. Sijaisoma Tuzo kuona namna Mahakama ilivyoadress suala la Mkataba kupatikana kwa kukiuka Sheria ya Ugavi. Kama Mahakama iliona kwamba Sheria imekiukwa ilipaswa kulitolea maamuzi suala la uhalali wa Mkataba uliokiuka sheria. Kama haikufanya hivyo, mtu anaweza kusema kwamba Mahakama ilishindwa kutumia mamlaka yake vizuri kwa kufanya uchunguzi wa kimahakama (Improper exrcise of jurisdiction). Hilo linaweza kuangukia katika mwanya wa tatu.

Nadhani kutokana na vilio vingi vya wananchi kutokana na hili bila kujali mantiki ya hoja zao ingekuwa bora kama Serikali ikalitizama upya suala hilo kwa kuitisha kikao cha dhalura cha Baraza la Mawaziri kulitafakari upya suala hili kwa kushirikiana na ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, mawakili walioitetea serikali katika suala hili na wataalamu wengine. Na hili lifanyike haraka ili kuzuia uwezekano wa malimbikizo ya riba zaidi. Kama ikionekana kuna mwanya wowote wenye uwezekano wa busara kuweza kupeleka maombi mahakama kuu ya kuhoji uhalali wa Tuzo wafanye hivyo chini ya Certificate of Urgency.
 
Mimi nasisitiza ubaya wa majina yetu...yanatuathiri akili zetu....mara NUNDU sasa huyu FUNGAMTAMA...SIJUI MTAMA UMEKOSA NINI HATA UFUNGIWE

Fungamtama ni wakili wa Rostam na siajabu hata hiyo kwenye kesi hiyo alihusika, hivyo anapasenti yake.

Alishawahi kumuwakilisha RA kwenye kesi ambayo RA alikuwa analalamikia magazeti fulani alipwe fidia.
 
*Afichua mashahidi walioitetea Tanesco Tanesco ICC
*Atoa tahadhari kuhusu msimamo wa Sitta

Na Happiness Katabazi

MMOJA wa mawakili mahiri wa kujitegemea nchini, Kennedy Fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.



Fungamtama aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti hili kupata taarifa kuwa wakili huyo ni miongoni mwa wanasheria walioisoma hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICC).


Mwanasheria huyo ambaye alimuelezea Sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za Watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya ICC, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili.
Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.


Wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si Waziri Sitta binafsi.


Fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma na kujiridhisha kwamba hukumu hiyo yenye kurasa 150 ya kesi namba 15947/VRO kati ya Kampuni ya Dowans na Tanesco ilipokewa na ICC Novemba 20, mwaka 2008 na ikatolewa hukumu Novemba 15 mwaka jana.


Alisema mkataba kati ya Tanesco na Dowans ulisainiwa Juni 23, mwaka 2006 na mkataba huo unajulikana kama ‘Power Off - Take Aggreement (POA)” chini ya kifungu cha 14 (e) cha POA, na kufafanua kwamba pande zote mbili katika mkataba huo zilikubaliana kwamba uamuzi wa Mahakama ya ICC ndio utakuwa wa mwisho na utazibana pande zote mbili na hautaweza kukatiwa rufaa.


Fungamtama alisema kifungu cha 14 (f) cha POA, kinasomeka: “The parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability of this arbitration agreement or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this section.”


Kwa tafsiri nyepesi, Fungamtama alisema kifungu hicho kinasema, Tanesco na Dowans katika mkataba wao walikubaliana kwa maandishi kuweka kando haki za kupinga au kuhoji mwenendo na tuzo zitakazotolewa na baraza la usuluhishi.


Alisema Waziri Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari akitaka serikali itumie kifungu cha 16 cha Sheria ya Tanzania ya Usuluhishi Sura ya 15 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwamba serikali inaweza kutumia kifungu hicho kutengua hukumu ya mahakama ile ya kimataifa.


“Ni kweli Mahakama Kuu ya Tanzania imepewa mamlaka ya kutengua maamuzi yanayotolewa na mahakama za kimataifa endapo tu itadhihirika kuwapo kwa mambo mawili yafuatayo:


Moja; msuluhishi wakati akiendesha kesi alikuwa akiegemea na kupendelea upande mmoja (arbitrator has miss - conducted himself. Pili: Mazingira ya kufikia uamuzi ule yalitawaliwa na rushwa au shauri lilifikishwa mahakamani bila kufuata taratibu za kisheria (an arbitration or award has been improperly procured).


“Hayo ndiyo mambo mawili peke yake yanayoweza kusababisha Mahakama Kuu ya hapa nchini kutengua hukumu zilizokwisha kutolewa na mahakama za kimataifa za usuluhishi na si kwa jambo jingine lolote.


“Sasa kama Sitta ana ushahidi, vigezo hivyo viwili vya kisheria katika lililokuwa shauri baina ya Dowans na Tanesco kwamba wasuluhishi wale ambao ni majaji waliipendelea Dawans, au walikura rushwa, ingekuwa ni vyema haraka apeleke ushahidi huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuwatuma wanasheria wake wakafungue kesi Mahakama Kuu ili iweze kutengua hukumu hiyo kupitia huo ushahidi wake kama anao na si kama anavyofanya hivi sasa kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari,” alisema wakili huyo.


Aidha, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha jedwali la 3 katika Sheria ya Usuluhishi ya Tanzania, Sura ya 15 ya mwaka 2002 kinasomeka hivi:


“Each contract state undertakes to ensure the execution by its authorities and in accordance with the provisions of its national laws of arbitrarily awards made in its own territory under the preceding articles”.


“Kwa tafsiri rahisi, kifungu hicho utaona tayari nchi imejifunga mikono na utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama za kimataifa kwa sababu ni nchi yetu yenyewe imeridhia sheria na mikataba ya kimataifa.”


Alisema kwa hiyo maelezo ya Waziri Sitta ya kutaka Dowans isilipwe, ni kutaka kuishawishi serikali na umma kukaidi kutekeleza maamuzi halali chini ya sheria na mikataba ambayo serikali iliiridhia kuitii na kuitekeleza.


Aidha, alisema jambo jingine lililojitokeza wakati kesi hiyo ikiendelea baina ya Dowans na Tanesco ni Tanesco walitaka kujua wamiliki wa Dowans ni kina nani na Mahakama ya ICC iliona hoja hiyo ya Tanesco ya kutaka kumjua mmiliki haina umuhimu wowote katika mgogoro uliokuwa mbele yao na ikatupilia mbali, kwa sababu iliona hoja hiyo haina maana yoyote mbele yao.


“Kwa hiyo kwa kitendo cha Waziri Sitta kulianzisha suala hilo la kutaka kujua wamiliki wa Dowans wakati hoja hiyo tayari ilikwishatolewa uamuzi na ICC, kisheria hawezi kulianzisha tena jambo hilo la kutaka kujua wamiliki kwa njia anayoitumia ya vyombo vya habari.


“Kwa hiyo maelezo yote yanayoendelea kutolewa kuhusu hukumu hiyo ni kutaka kujinasua katika lawama wakati yeye na baadhi ya maswahiba zake enzi zile akiwa Spika wa Bunge ndio waliokuwa chanzo cha Tanesco kuvunja mkataba na Dowans, hivyo mwisho wa siku shirika hilo la umeme kujikuta likiburuzwa katika korti ya ICC.


“Na ifike mahala wananchi na vyombo vya habari na serikali itoke usingizini na ijiulize maswali yafuatayo kwamba Sitta hakuwepo kwenye usikilizwaji wa shauri hilo? Sitta hakuwa akijua kwamba Tanesco imefunguliwa kesi na Dowans katika Mahakama ya ICC?


“Kwa kuwa Sitta alikuwa mstari wa mbele kuzipiga vita Dowans na Richmond, ni wazi alikuwa akifahamu kwamba Tanesco imeburuzwa mahakamani na kama kweli Sitta ni mzalendo wa kweli na hana chuki binafsi katika hili ni kwanini hayo madai anayoyasema asingeiomba serikali imuweke kama shahidi wa upande wa Tanesco ili akatoe ushahidi anaousema kila kukicha kwenye vyombo vya habari?


“Amesubiri tayari shirika letu la umeme ambalo ndilo lilikuwa mdaiwa katika shauri hili limeshindwa kufurukuta kwenye kesi hiyo na tumetakiwa tulipe kiasi hicho kikubwa cha fidia ndiyo kila kukicha anazungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo, tena ukitazama maoni anayoyatoa utafikiri si mtu aliyesomea sheria kabisa….naomba sana hasa serikali ipuuze ushauri wa Sitta kwani ni wazi kabisa anataka kuliingiza taifa kwenye matatizo mengine makubwa.


“Watanzania na huyo Waziri Sitta ambao hawajaisoma hukumu ile naomba niwaeleze wazi mimi nimeisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba, kama taifa kupitia hukumu hiyo tumeshikwa pabaya, hivyo hatuwezi kukata rufaa, isipokuwa tu kama tutathibitisha sababu zile mbili nilizozitaja,” alisema wakili Fungamtama.


Aidha, Fungamtama aliviasa baadhi ya vikundi mbalimbali vya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuzungumzia hukumu hiyo ambayo hata wengine hawajawahi kuisoma wala kuiona, kwani tayari kuna baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika makala kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa Tanesco haijawahi kuleta shahidi hata mmoja kutoa ushahidi.


Jambo ambalo Fungamtama alisema si kweli na linalenga kuhadaa umma, kwani majibu na nakala ya hukumu hiyo ambayo anayo inaonyesha Tanesco ilipeleka mashahidi watano na walitoa ushahidi wao.


Wakili huyo aliwataja mashahidi hao kuwa ni Subira Wandiba, ambaye ni Mwanasheria wa Tanesco, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Zabuni iliyotoa tenda kwa Dowans, Balozi Fulgence Kazaura, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk. Idrisa Rashid, Mhasibu Mkuu wa shirika hilo, Jamhuri Ngeline na Boniface Njombe.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Januari 13 mwaka 2011
 
Wakati sisi laymen tunajadili ishu kama za ufisadi wa Dowans lazima pia tusome maoni ya kitaalamu kama hayo hapo juu badala ya kupandisha jazba tu.
 
Mimi kama Mtanzania niko tayari kwa adhabu nyingine toka ICC ya kunyimwa misaada toka nje kuliko kuilipa dowans
 
Back
Top Bottom