TEACHER FRANK MSIGWA
JF-Expert Member
- Oct 19, 2016
- 537
- 443
Kesi ya kutoa lugha za matusi haina dhamana???Tafsiri ya ukamanda inapotoshwa na Chadema, ukamanda sio kuvunja sheria na kutoa lugha za matusi.
Kesi ya kutoa lugha za matusi haina dhamana???Tafsiri ya ukamanda inapotoshwa na Chadema, ukamanda sio kuvunja sheria na kutoa lugha za matusi.
Nani kasema LEMA hana kesi ya kujibu?ifike mahari tuitii mamlaka na sio kuibeza, Lema anakesi ya kujibu, tatizo ni ujuaji wa mawakili wake
Vipi kula rambirambi nako hakuleti umaarufu??Ndio maana nasema Lema this time akitoka atakuwa amenyoooka vizuri.Asifikiri kuvunja sheria ndio kutamletea umaarufu.Serikali hii haijaribiwi kabisaa
Sidhani mkuuVipi kula rambirambi nako hakuleti umaarufu??
Kunaleta umaarufu sana tu.....hujaona trump wa bongo baada ya kula rambirambi kawa maarufu though dhambi ya kula rambirambi ishaanza mtafunaSidhani mkuu
Nimemwelewa sana Msando, umeongea ukweli kuwa kwenye sheria hakuna ushabiki kama wa Yanga Na simba.
Na Lema aangalie aina ya siasa zake, kwa nini yeye tu akae ndani Na sio wenzie.!
AA wapi nyie juzi mliimba Musoma na kuisifu mahakama,Nikawaambia mtakuja kulia humu,yametimia,Tatizo lenu kila kitu mnataka kushinda,kubalini na kushindwa,kesi ngapi Muheshimiwa Mbunge mwanasheria Tundu lissu ameshinda mkajisifu Mawakili wa serikali ni vilaza mbele yake?si aende akamtetee jamaa yake?nyie ni wanafik tu kama hao viongozi wenu wa CDM!Acha asome namba za kisongo sasa!Nani anasifia mahakama zinazofanya kazi kwa maagizo toka juu? Ukiona mahakama imetenda haki kwa mpinzani basi ujue hakukuwa na jinsi nyingine ama shinikizo toka juu ni dogo.
Hakuna busara kwenye kudai haki ambazo zipo kisheria....Msando ampe ushauri wa kuwa objective na kutumia busara Mtukufu Rais, ambaye hana busara na siyo objective (he is tooo emotional)...
Kuna kipindi Mbunge muheshimiwa Esther Bulaya alipomshinda katika Rufaa bwana Tyson nilisema walipoisifu mahakama imetenda haki kwao ikija ya Mbunge muheshimiwa Godbless Lema au kesi yoyote ya mahakamni wasijekusema mahakama hazitendi haki,je mko wapi?mahakama inatenda haki kwenu tu watu wenu wakishinda kesi,mkibanwa mnaonewa!
Lema is not ok upstairs! nilimdharau alipofanya Mazungumzo ya faragha na SIMBACHAWENE Kaenda kuyaanika Bungeni! absurd.Tuache kumpa kichwa Lema hata kwenye facts. Lema ni mpambanaji kisawasawa lakini anajisahau sana na wakati mwingine hachungi kauli zake ambazo pengine zingetolewa na mwingine yeye akiwa madarakani angechukua hatua hizi hizi. Tufanye siasa na kudai haki bila kukwazana kwa matusi na lugha za hatari tena ukiwa kiongozi.
Apate dhamana ili atukane tena viongozi? Lema hastahili dhamana kwani kakiuka masharti yakeNani kasema LEMA hana kesi ya kujibu?
Kinachogomba hapa ni dhamana, kwanini inacheleweshwa kwa makusudi?
Lema anatakiwa apewe haki yake ya kikatiba.
Mkuu hayo maswali ni vyema ungemwelekezea Albert Msando wakili wa Lema.Acha kuwa kibendera wewe......
Wewe unayejua kuwa liko kisheria taja kisheria kivipi? Usibaki kusema kisheria za nchi fafanua ili uonyeshe huo uelewa wako na siyo kufata upepo tu.
Pia taja makosa yapi yanayofanya anyimwe dhamana
Kila siku mnaambiwa tumieni kichwa kufikiri
Mkuu hayo maswali ni vyema ungemwelekezea Albert Msando wakili wa Lema.
Na kama ungesoma Na kuyaelewa hayo maoni ya Wakili wa Lema nadhani usingetoa povu kiasi hiki sababu maswali yako yote yamejibiwa na Msando.!
Nadhani angejikita kueleza hizo techicalities, angalau tungemwelewa! Andiko la Msando (kama ni yeye kweli) linakosa mshindo kwa kuwa linajaribu kufanya comparison ya Lema na wabunge (au wanasiasa?) wengine wa Chadema katika ufanyaji siasa, huku mwenyewe Msando (?) akifahamu kuwa kuna mazingira tofauti sana baina ya wanasiasa mmoja mmoja, na sio tu ndani ya Chadema, bali kwa ujumla yanayozunguka utendaji wao. Hoja yake ni tenge kwa kuwa inajaribu pia kuonyesha kuwa Lema anastahili kuendelea kuwa mahabusu sio kwa sababu za kisheria bali kwa sababu tu ya namna anavyofanya siasa zake! Naona wakili huyo msomi anajaribu kutaka kutumia vibaya fursa ya Lema kuendelea kuwa mahabusu!Hakuna busara kwenye vitu ambavyo sheria imevitaja direct dhaman ni haki ya mtu kikatiba wala hakutaki busara apo kosa la lema lipo bailable kisheria sasa apo busara ya nn
Kama unajua zaidi hayo ambayo wakili wake hayajui ni vyema ukawasilisha Mahakamani ili umtoe Lema.So una maana wewe ulikuwa unarudia alichosema pasi kujua lolote?
Huo ndiyo unaitwa ubendera kama ulikuwa hujui
Hakuna mashart magum ktk kupewa dhamana sheria inaprohibit cambasum procedure zinazoweza kuchelewesha dhamana ya mtu na ktka mazingira ambayo unaweza kunyimwa dhamana though kosa lako ni vailable kesi ya lema haifallow kwenye mazingira hayo ni kesi ambayo inabidi awe amepewa dhamanaDhamana ni haki yenye masharti na vigezo vigumu.
Hata kama ni wazi kuwa huna hatia, na kuwa mashtaka dhidi yako ni ya kuchonga, bado unaweza kunyimwa dhamana kwa sababu za usalama wako mwenyewe au ule wa umma.
Kwenye ishu ya Lema ninaona tatizo kubwa linaloripotiwa kila siku na vyombo vya habari ni kuwa, wanasheria wa Lema wamekosea vifungu na taratibu. Hatujawahi kusikia wakikanusha japo ni wana jukwaa mahiri.
Na kila wakipata ushindi vitimbi vyao huonekana na kusikika.