Wakili Albert Msando: Issue ya Lema inahitaji Busara zaidi ya Ubishi na Ujuaji

Nimemwelewa sana Msando, umeongea ukweli kuwa kwenye sheria hakuna ushabiki kama wa Yanga Na simba.

Na Lema aangalie aina ya siasa zake, kwa nini yeye tu akae ndani Na sio wenzie.!

Acha kuwa kibendera wewe......
Wewe unayejua kuwa liko kisheria taja kisheria kivipi? Usibaki kusema kisheria za nchi fafanua ili uonyeshe huo uelewa wako na siyo kufata upepo tu.
Pia taja makosa yapi yanayofanya anyimwe dhamana
Kila siku mnaambiwa tumieni kichwa kufikiri
 
Nani anasifia mahakama zinazofanya kazi kwa maagizo toka juu? Ukiona mahakama imetenda haki kwa mpinzani basi ujue hakukuwa na jinsi nyingine ama shinikizo toka juu ni dogo.
AA wapi nyie juzi mliimba Musoma na kuisifu mahakama,Nikawaambia mtakuja kulia humu,yametimia,Tatizo lenu kila kitu mnataka kushinda,kubalini na kushindwa,kesi ngapi Muheshimiwa Mbunge mwanasheria Tundu lissu ameshinda mkajisifu Mawakili wa serikali ni vilaza mbele yake?si aende akamtetee jamaa yake?nyie ni wanafik tu kama hao viongozi wenu wa CDM!Acha asome namba za kisongo sasa!
 
huyu msando ni nilianza kumuona kanjanja tokea ile ishu ya zitto na chadema, anaongea kwa emotion na sio uhalisia!
 
duuu LEMA hadi birthday yangu ndio tutamuona, hahahahaaaa nakumbuka kale kawimbo 'MTOTO WACHA KUPIGA MAYOWE ..............."RAHA SANA ARUSHA TULIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!
 
Hakuna busara kwenye kudai haki ambazo zipo kisheria....Msando ampe ushauri wa kuwa objective na kutumia busara Mtukufu Rais, ambaye hana busara na siyo objective (he is tooo emotional)...

Who is Albert Musando by the way?
Wakili Musando anataka kutuaminisha kuwa kesi ya Mhe. Lema inahitaji BUSARA na siyo SHERIA? Huo utakuwa ni uchizi!
I am not a lawyer or advocate by profession, ukweli unabaki palepale kuwa kila mtuhumiwa ana HAKI ya kupewa DHAMANA kwa mjibu wa SHERIA kulingana na kosa alilotenda isipokuwa makosa yanayo angukia kwenye UHAINI,MAUAJI na UHUJUMU UCHUMI!
Kesi ya Lema haiangukii kwenye makosa hayo! Kila mtu anafahamu kuwa Lema yuko Mahabusu kwa kunyimwa dhamana kwa tuhuma za kusema ALIOTA NDOTO KUWA MUNGU ATAKATISHA MAISHA YA RAIS JPM kama ataendelea kutawala kama 'mungu'!
Sasa tunataka Albert Musando atuambie katika makosa ya Jinai sheria gani inayosema mtu akiota ndoto kuhusu jambo fulani litakalompata Rais ashtakiwe na asipewe dhamana! Ni kesi gani,mwaka gani na nchi gani raia alifunguliwa kesi akanyimwa dhamana au kufungwa kwa KUOTA NDOTO!
Kinachoendelea kuhusu kesi ya Lema ni UDIKTETA uleule wa kuminya HAKI,SHERIA na TARATIBU ili kuwakomoa Wapinzani!Na hayo ni maagizo toka JUU(JPM)!
Tujiulize maswali rahisi na tuyajibu kwa kutumia hekima:
  1. Je, hivi kesi hii ingelikuwa inamhusu Mbunge wa CCM angelinyimwa Dhamana?
  2. Je, mtu kuota ndoto kumhisu Rais na ukaisema hadharani ni kosa la jinai,uhaini,mauaji au nini?
  3. Je,watu waliosema/wanaosema kwamba mgombea Urais wa CHADEMA ATAKUFA wakti wa Kampeni za 2015 mbona hawakukamatwa na kunyimwa dhamana??
  4. Je, kati ya Mhe. Lema na wale jamaa wana CCM waliokamatwa na nyara za Serikali nani alistahili dhamana?
Albert Musando atakuwa ni moja ya Mawakili wanaotumiwa na Serikali ya JPM kama Toilet Papers! Kwamba TP inaonekana muhimu tu mtu anapokwenda chooni lakini baada ya haja ni rubbish!
Albert Musando ni sawa na TP!
 
Kuna kipindi Mbunge muheshimiwa Esther Bulaya alipomshinda katika Rufaa bwana Tyson nilisema walipoisifu mahakama imetenda haki kwao ikija ya Mbunge muheshimiwa Godbless Lema au kesi yoyote ya mahakamni wasijekusema mahakama hazitendi haki,je mko wapi?mahakama inatenda haki kwenu tu watu wenu wakishinda kesi,mkibanwa mnaonewa!
 
Tuache kumpa kichwa Lema hata kwenye facts. Lema ni mpambanaji kisawasawa lakini anajisahau sana na wakati mwingine hachungi kauli zake ambazo pengine zingetolewa na mwingine yeye akiwa madarakani angechukua hatua hizi hizi. Tufanye siasa na kudai haki bila kukwazana kwa matusi na lugha za hatari tena ukiwa kiongozi.
Lema is not ok upstairs! nilimdharau alipofanya Mazungumzo ya faragha na SIMBACHAWENE Kaenda kuyaanika Bungeni! absurd.
 
Nani kasema LEMA hana kesi ya kujibu?

Kinachogomba hapa ni dhamana, kwanini inacheleweshwa kwa makusudi?

Lema anatakiwa apewe haki yake ya kikatiba.
Apate dhamana ili atukane tena viongozi? Lema hastahili dhamana kwani kakiuka masharti yake
 
Acha kuwa kibendera wewe......
Wewe unayejua kuwa liko kisheria taja kisheria kivipi? Usibaki kusema kisheria za nchi fafanua ili uonyeshe huo uelewa wako na siyo kufata upepo tu.
Pia taja makosa yapi yanayofanya anyimwe dhamana
Kila siku mnaambiwa tumieni kichwa kufikiri
Mkuu hayo maswali ni vyema ungemwelekezea Albert Msando wakili wa Lema.

Na kama ungesoma Na kuyaelewa hayo maoni ya Wakili wa Lema nadhani usingetoa povu kiasi hiki sababu maswali yako yote yamejibiwa na Msando.!
 
Mkuu hayo maswali ni vyema ungemwelekezea Albert Msando wakili wa Lema.

Na kama ungesoma Na kuyaelewa hayo maoni ya Wakili wa Lema nadhani usingetoa povu kiasi hiki sababu maswali yako yote yamejibiwa na Msando.!

So una maana wewe ulikuwa unarudia alichosema pasi kujua lolote?
Huo ndiyo unaitwa ubendera kama ulikuwa hujui
 
Ifike mda hata Lema mwenyewe atumie busara. Si vibaya kuomba radhi akasema tu jamani naomba radhi siku ile nilitumia kijiti cha Morogoro, tutamulewa tu
 
Hakuna busara kwenye vitu ambavyo sheria imevitaja direct dhaman ni haki ya mtu kikatiba wala hakutaki busara apo kosa la lema lipo bailable kisheria sasa apo busara ya nn
Nadhani angejikita kueleza hizo techicalities, angalau tungemwelewa! Andiko la Msando (kama ni yeye kweli) linakosa mshindo kwa kuwa linajaribu kufanya comparison ya Lema na wabunge (au wanasiasa?) wengine wa Chadema katika ufanyaji siasa, huku mwenyewe Msando (?) akifahamu kuwa kuna mazingira tofauti sana baina ya wanasiasa mmoja mmoja, na sio tu ndani ya Chadema, bali kwa ujumla yanayozunguka utendaji wao. Hoja yake ni tenge kwa kuwa inajaribu pia kuonyesha kuwa Lema anastahili kuendelea kuwa mahabusu sio kwa sababu za kisheria bali kwa sababu tu ya namna anavyofanya siasa zake! Naona wakili huyo msomi anajaribu kutaka kutumia vibaya fursa ya Lema kuendelea kuwa mahabusu!
 
So una maana wewe ulikuwa unarudia alichosema pasi kujua lolote?
Huo ndiyo unaitwa ubendera kama ulikuwa hujui
Kama unajua zaidi hayo ambayo wakili wake hayajui ni vyema ukawasilisha Mahakamani ili umtoe Lema.

Kupiga kelele nyuma ya keyboard bila hoja za msingi hakumsaidii kwa namna yoyote ile Lema .
 
Dhamana ni haki yenye masharti na vigezo vigumu.
Hata kama ni wazi kuwa huna hatia, na kuwa mashtaka dhidi yako ni ya kuchonga, bado unaweza kunyimwa dhamana kwa sababu za usalama wako mwenyewe au ule wa umma.

Kwenye ishu ya Lema ninaona tatizo kubwa linaloripotiwa kila siku na vyombo vya habari ni kuwa, wanasheria wa Lema wamekosea vifungu na taratibu. Hatujawahi kusikia wakikanusha japo ni wana jukwaa mahiri.

Na kila wakipata ushindi vitimbi vyao huonekana na kusikika.
Hakuna mashart magum ktk kupewa dhamana sheria inaprohibit cambasum procedure zinazoweza kuchelewesha dhamana ya mtu na ktka mazingira ambayo unaweza kunyimwa dhamana though kosa lako ni vailable kesi ya lema haifallow kwenye mazingira hayo ni kesi ambayo inabidi awe amepewa dhamana

Ukisema mawakili wa lema waje wakanushe naisi ww ujui unachokiongea iko professionally kesi ikiwa mahakaman hurusiwa kwenda kwenye media na kuanza kuiongelea na kweli akilin mwako inaweza kukuingia akilin eti mawakil nguli wote wanakosea kuomba dhamana ishu ambayo ata mtoto wa certificate anaweza kuifanya kwa ufasaha maskin Tanzania yangu mahakama imewekwa mfukon
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom