Mkuu hizo ndizo sifa zetu watanzania wengi ambazo mojawapo ni kuamini amini tu bila hata kuhoji kwa nini unaamini.
Kuna watu hapa ukiwauliza sababu za kuwepo katika position na mtazamo fulani watakwambia wapo kwa sababu WANAANIMI kwa vile FULANI alisema hivi au vile.
Ndiyo maana utaona kwenye mikutano ya vyama vya siasa watu wanabadilisha kadi kama mzunguko wa pesa ulivyo na ukiwauliza kwa nini wanahama vyama, basi utakuwa na bahati sana kumpata yule anayeelezea sababu isiyojengwa na imani.
Watanzania wengi ni bendera fuata upepo, na ndiyo maana hata wanasiasa wanawatumia vizuri sana katika malengo yao.
Siyo bahati mbaya kwa Taifa kuwa hapa lilipo. Watu wa aina hii ni janga kwa taifa kwa sababu hawajitabui na usitegemee mtu asiyejitambua anaweza kumtambua mtu mwingine. NEVER!.
Mpaka pale wananchi wataweza kuyajongea mambo huku wametanguliza neno WHY, ndiyo tutaweza angalau kukimbia kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Ng'wama naungana mkono na wewe
kuna mtu leo anaamini kuwa eti Chadema au NCCR kuwa zikiingia ikulu ndio tutaendelea. I do hate CCM, oh I do
lakini tatizo letu liko deeped zaidi, tukiweza kujenga Familia zenye nguvu, taasisi zenye nguvu, ndio tutapata Taifa lenye nguvu
I cant imagine, kuwa someone ni baba wa familia lakini ni gullible, anaweza kudanganywa na wahuni wachache, akapelekeshwa kama upepo , yet these men are 'family men'
Ujinga wetu, na upofu wetu ni kama maiti, watu hawajiulizi, hawaulizi, wanapelekwa kama kundi la nyumbu, it is pity
I have been waiting over and over, mtu aje na incontrovertible truth kuwa ubaya wa zitto ni huu hapa. Hamna
just imagine starting from Lissu, lema, mnyika, n.k watu tuliowategemea kuwa watakuwa icon of changes, wamekuwa icon ya ujinga wa kutumika na wachache, yet these men we are expecting to lead us????? ney
ukiweza kudanganywa na kupumbazwa na Mbowe na Slaa kutimiza malengo yao; hao mababa wa uongo ( wazungu) utaweza vipi kuwapinga??
kwa nini tumekuwa so cheap wa kuaminishwa kitu, kama vile dini, ukakiamini na kukiingiza kabisa moyoni na ukaishi katika huo uongo??
Wale wana CCM tuliokuwa tunawaona wame hehuka kwa Kikwete kuwa chaguo la Mungu, baada ya Kikwete kuwadanganya over ten years; ndiyo tunaowaona chadema kwa style nyingine wakiwa wameaminishwa over just 4 years kuwa zitto ni msaliti
Kosa letu ni nini? kwa nini wanasiasa wahuni?? ukienda nyumba za ibada nako utawakuta wahuni wahuni tu, YET we are royal followers of these thieves; whom we can never QUESTION THEM?? any question??
Ng'wama huwa najaiuliza naumia sana, kama jamii yetu hatuwezi kujiuliza, tukauliza, tukakataa kupumbazwa na kuendeshwa kwa hisia, nani wa kutuokoa??