Wakili afungua kesi kupinga polisi kuajiri wachina kwenye jeshi la polisi

Ingelikuwa mizungu hapo msingelaumu..na hilo liwakili nalo libaguzi tu...pumbaff kabisa...mbona nchi za uarabuni na ulaya wanajeshi/polisi wa kiafrika wamejaa tele tu!! Sisi waafrika ni wabaguzi sana tena sanaaa.
 
jamaa wamechukua reli, shirika la umeme sa na polisi wanataka wachkue pia?? mwishowe watachkua na urais ss
 
Watu weusi tu walalamishi by default - kujitia ujuaji,tubapoteza wakati hatun
a hata ethics za utendaji kazi, tunapoza muda mwingi kupika majungu na fitina na kuzungumzia nasuala ya kandanda/ZOKA!.

Chukulia mfano mdogo wa Serikali ya Zambia kuajili kwa mkataba Wachina wachache kwenye Wizara ya mambo ya ndani - si kelele hizo, mnalahumu Serikali ya Zambia as if imefanya kitendo cha uhaini!! Mnaleta maigizo hapa kwa ku-shade crocodile tears kujifanya mnasikitishwa sana na kitendo cha Serikali ya Zambia kuajili Wachina.

Swali: Je,mnajua kwa nini Serikali ya Zambia imefikia uhamuzi wa kuajili Wachina kwenye vitengo Fulani ndani ya Wizara ya mambo ya ndani? Kinacho wauma ni kitu gani hasa, wakati hata sisi hapa kwetu Utendaji kazi wa baadhi ya wafanya kazi ndani ya Wizara ya mambo ya ndani ndio unalalamikiwa sana na wananchi wengi, kwani nyinyi hilo hamlijui - tukubali utendaji kazi na uwajibikaji wetu una walakini sana,ndio maana tulishindwa ku-run Viwanda vya UMMA tulivyo taifisha,Mashirika ya UMMA karibu yote yalihujumiwa na sisi wenyewe kwa kuendekeza nepotism na vices nyingine hatarishi - tulivyo wa ajabu akija mgeni akasimamia Shirika waswahili wanafanya kazi kwa bidii na kujituma - na hicho ndicho kitakuja kutokea huko Zambia baada ya kuajili Wachina - mambo yatabadirika 4 the better.

Mwisho nawakumbusha kwamba mbona hapa kwetu kuna madaktari kutoka Cuba na Uchina wameajiliwa kwa mkataba na Wizara ya Afya - mbona amuhadamani kupinga ujio wa wageni kwenye Wizara ya afya,TaneSco wakati Fulani iliwahi kusinamia na Mzungu kutoka South Africa mbona mlikaa kimya.
 
Tafadhali weka source ya habari yako manake maTamaso wengi humu!
 
Wakili mmoja nchini Zambia Bw.Dickson Jere amefungua kesi ya kikatiba kwenye mahakama kuu ya nchi hiyo, kupinga polisi nchini humo kuajiri raia wa Kichina katika jeshi hilo.

Hivi karibuni jeshi la polisi nchini Zambia limeajiri raia nane (8) wa Kichina na kuteua wawili kati yao kushika vyeo vya juu, ambao ni Mkuu wa Kamandi ya Polisi wa akiba, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP.Zhang Ming, na Msaidizi wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP.Wu Ming.

Maofisa hao wapya 8 waliapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, Inspekta Jenerali Kakoma Kanganji, ambapo pia alipokea magari 10 yaliyotolewa na serikali ya China kama msaada kwa jeshi hilo.

Wakili Jere amesema kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi nchini Zambia ni cha aibu na ni kinyume na katiba. IGP Kanganji alijitetea kuwa maofisa wote 8 walioajiriwa ni raia wa Zambia pia kwa sababu wana uraia pacha (wa Zambia na China).
_
Hata hivyo Wakili Jere ametaja ibara ya 194 (a) ya Katiba ya nchi hiyo kuwa hairuhusu raia yeyote wa Zambia mwenye uraia wa nchi nyingine (uraia pacha) kuajiriwa katika nafasi yeyote kwenye majeshi. "Mtu mwenye uraia pacha anaweza kuajiriwa katika idara nyingine za serikali lakini si kwenye majeshi. Polisi wamevunja katiba" amesema Jere.

Hivi karibuni serikali ya China ilitangaza kuutaifisha uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda mjini Lusaka, siku chache zilizopita, ili kufidia deni ambalo Zambia imeshindwa kulilipa kwa muda mrefu.

Nchini Afrika Kusini raia wa kichina Bi.Jianling Wu aligombea udiwani katika kata namba 118 jijini Johannesburg, kupitia chama cha ANC.

Wimbi la raia wa Kichina kuingia katika nchi za Afrika na kupewa nafasi vyeo mbalimbali limeibua wasiwasi kwa baadhi ya wananchi wakidai China ndiye mkoloni mpya barani Afrika, kutokana na nchi nyingi za Kiafrika kudaiwa madeni makubwa na China yasiyolipika.

Nini maoni yako?View attachment 872053
Maoni yangu ni haya
Ukikubali kuolewa usikatae kulala uchi... Mke hana ridhaa ya kupinga matakwa ya mumewe... Afrika ni mke mpya wa China... Na mchina anaoa mitala
 
Dooh afadhali wakili...apambane kuondoa hiyo aibu.....rais wa Zambia sijui analichukuliaje hili swala.....lkn pia natambua toka soko la shaba liyumbe duniani..... Zambia wapo taabani sana kifedha.....maana wao ndio walikuwa wauzaji wakubwa wa shaba kwenye soko la dunia.....
Yupo zake bar anakunywa Ofiser
 
Dooh afadhali wakili...apambane kuondoa hiyo aibu.....rais wa Zambia sijui analichukuliaje hili swala.....lkn pia natambua toka soko la shaba liyumbe duniani..... Zambia wapo taabani sana kifedha.....maana wao ndio walikuwa wauzaji wakubwa wa shaba kwenye soko la dunia.....
Ni kweli hata Kwacha yao imeporomoka sana dhidi ya dolla, hivyo kupelekea mfumko wa bei kwenye bidhaa..
 
.
IMG-20180921-WA0062.jpg
 
Imagine kama tunafikia kuambiana eti miundo mbinu haiji kwa sababu mmechagua upinzani, au sehemu walizochagua CCM no bomoa bomoa! Unategemea nini?

Bora tutawaliwe tu.
 
Back
Top Bottom