moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,900
- 4,865
Wakili mmoja nchini Zambia Bw.Dickson Jere amefungua kesi ya kikatiba kwenye mahakama kuu ya nchi hiyo, kupinga polisi nchini humo kuajiri raia wa Kichina katika jeshi hilo.
Hivi karibuni jeshi la polisi nchini Zambia limeajiri raia nane (8) wa Kichina na kuteua wawili kati yao kushika vyeo vya juu, ambao ni Mkuu wa Kamandi ya Polisi wa akiba, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP.Zhang Ming, na Msaidizi wake, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP.Wu Ming.
Maofisa hao wapya 8 waliapishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, Inspekta Jenerali Kakoma Kanganji, ambapo pia alipokea magari 10 yaliyotolewa na serikali ya China kama msaada kwa jeshi hilo.
Wakili Jere amesema kitendo kilichofanywa na jeshi la polisi nchini Zambia ni cha aibu na ni kinyume na katiba. IGP Kanganji alijitetea kuwa maofisa wote 8 walioajiriwa ni raia wa Zambia pia kwa sababu wana uraia pacha (wa Zambia na China).
_
Hata hivyo Wakili Jere ametaja ibara ya 194 (a) ya Katiba ya nchi hiyo kuwa hairuhusu raia yeyote wa Zambia mwenye uraia wa nchi nyingine (uraia pacha) kuajiriwa katika nafasi yeyote kwenye majeshi. "Mtu mwenye uraia pacha anaweza kuajiriwa katika idara nyingine za serikali lakini si kwenye majeshi. Polisi wamevunja katiba" amesema Jere.
Hivi karibuni serikali ya China ilitangaza kuutaifisha uwanja wa ndege wa Keneth Kaunda mjini Lusaka, siku chache zilizopita, ili kufidia deni ambalo Zambia imeshindwa kulilipa kwa muda mrefu.
Nchini Afrika Kusini raia wa kichina Bi.Jianling Wu aligombea udiwani katika kata namba 118 jijini Johannesburg, kupitia chama cha ANC.
Wimbi la raia wa Kichina kuingia katika nchi za Afrika na kupewa nafasi vyeo mbalimbali limeibua wasiwasi kwa baadhi ya wananchi wakidai China ndiye mkoloni mpya barani Afrika, kutokana na nchi nyingi za Kiafrika kudaiwa madeni makubwa na China yasiyolipika.
Nini maoni yako?