WaKenya wazidi kuvamia ajira Tanzania

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,921
31,161
Heshima kwenu wanajamvi,

Siku hizi ukiingia katika ofisi mbali mbali kuanzia banks,Insurane ofisi,kampuni za utalii limekuwa jambo la kawaida kukutana na vijana wa kikenya wakifanyakazi ambazo zingefanywa na waTanzania.

Wiki mbili zilizopita nilipita TANELEC na SERENA nilichojionea huko hakifahi hata kuandikwa hakika iko siku waTanzania watapigania kujitoa EAC kama hali hii itaachwa iendelee hivi.Nafasi zote muhimu na kubwa zimeshikwa na waKenya,mishahara na marupurupu yamelundikwa kwa wageni wafanyakazi wa KiTanzania wamebaki wanyonge katika nchi yao hakuna sera mkakati wa kulinda ajira zao.Hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyosonga mbele siku hizi hata wasambaza barua wa DHL ni waKenya !.
 
Ni kweli kabisa nafasi nyingi za kazi Tanzania zimeshikwa na wa Kenya na huu na mwanzo tu,
fuatilia mabasi yanayotoka Kenya kila siku yanavyokuja na vijana wengi wa kenya ndo utaelewa
hii nchi haina mwenywe.Na tatizo kubwa zinapotolewa nafasi za kazi na watu kuitwa kwenye
interview watanzania tatizo kujieleza kingereza,Mkenya anaongea kingereza,makampuni mengi hayaangalii
uraia yanaangalia uelewa na pia uchapa kazi,na serikali haina mpango wowote juu ya hilo.Tuendelee
kudumisha kiswahili lugha ya Taifa hayo ndiyo madhara yake.
 
Udokozi ni kwa ajili ya kubeef up wages wanazopewa badala ya salaries!
Ata wewe kama walipwa mshahara laki 2 kwa mwezi lazima uwe mvivu!
Kwa taarifa yako hao hao unaowaita wavivu uko Botswana ni hotcake
 
hii mentality ambayo mwajidanganya et watz ni wavivu ni uhuni mtupu. Almost sector zote wamaejipenyeza na kinachowaokoa ni majungu sana sio kwamba ni wachapa kazi kivile. Wakenya ni wabinafsi sana ukifanya nao kazi hata kama utakesha lazima wakuwekee majungu ufukuzwe.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Siku hizi ukiingia katika ofisi mbali mbali kuanzia banks,Insurane ofisi,kampuni za utalii limekuwa jambo la kawaida kukutana na vijana wa kikenya wakifanyakazi ambazo zingefanywa na waTanzania.

kiomgozi m
Wiki mbili zilizopita nilipita TANELEC na SERENA nilichojionea huko hakifahi hata kuandikwa hakika iko siku waTanzania watapigania kujitoa EAC kama hali hii itaachwa iendelee hivi.Nafasi zote muhimu na kubwa zimeshikwa na waKenya,mishahara na marupurupu yamelundikwa kwa wageni wafanyakazi wa KiTanzania wamebaki wanyonge katika nchi yao hakuna sera mkakati wa kulinda ajira zao.Hali inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyosonga mbele siku hizi hata wasambaza barua wa DHL ni waKenya !.

kiongozi huwez kuamn kuwa juzi nilienda kwenye ofisi ya Omar packaging nilikuta salaes officer na and public relation offficer ni wakenya. niliumia sana na sikuwa na cha kusema nikakaa kimya. sasa leo bora umetoboa

lakini haya yana mwisho wake hatutakubali kuendelea kunyanyasika katika nchi yetu
 
Vuta pumzi ndo ushirikiano huo wa East Africa Community kwa hiyo na sie tuwapeleke wakwetu Kenya kama tuna ubavu huo
 
mkuu hata wasanifu majengo (architects) wamejaa tele hapa nchini, wanafichwa kwenye majumba ya wakenya wenzao,
huko arusha ndo usiseme
 
Lets be real, the human resource pool in Tanzania is wanting, the education system is flawed, the inherent laziness and ujamaa hangover are not helping either. Kenya is not the cause of Tanzania's problems, how can you employ a half baked graduate, who can't even answer basic/general knowledge questions in an interview, who can't communicate fluently in another language other than Swahili? you need to change your education system to fit the job market, msipochunga mtakuwa mnaexport wafanyi kazi wa nyumba tu.. true story
 
Why do the employers prefer Kenyans over Tanzanians?
Work on answers to my question then OUR problem(coz i think Kenyans getting jobs in Tanzania is a problem to some people) will be solved
 
Sera peke yake haitoshi kulinda ajira ya mzawa; watanzania wanasifa ya uvivu na udokozi ukfananisha na raia wengine wa EA........ Pambana na hili kwanza.

Hilo ni kweli kabisa, hata mimi natafuta mkenya wa kumpa kambi watanzania tuna hulka ya uvivu na wizi. Ukimpatia kazi, kitu cha kwanza anafikiria atatokaje! Sio atafanyaje kazi kampuni ipate faida na mshahara wake uongezeke.
 
Lets be real, the human resource pool in Tanzania is wanting, the education system is flawed, the inherent laziness and ujamaa hangover are not helping either. Kenya is not the cause of Tanzania's problems, how can you employ a half baked graduate, who can't even answer basic/general knowledge questions in an interview, who can't communicate fluently in another language other than Swahili? you need to change your education system to fit the job market, msipochunga mtakuwa mnaexport wafanyi kazi wa nyumba tu.. true story

Truth hurts.....
 
Duh hadi nimechoka leo nilikuwa nalipia DStv nikakumbana na vishoka toka Kenya wamejazana MultChoice wanavizia wateja wapya wakawafungie madish !.
 
Kwa maoni yangu nikwamba sisi watanzania tumejijengea mazingira ya kutoaminiana sisi kwa sisi kifikra, kwamba mtanzania anda shot cut zaidi, hatujitumi kwenye kazi na tunajali maslahi binafsi, wenzetu wako kikazi zaidi kuliko bla bla kama sisi, pia Lugha ya biashara ( Eng ) inaonekana ni kikwazo kwa wengi wetu.
 
Tatizo kubwa ni nchi imeendekeza siasa! Kila siku serikali ipo mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya kiswahili. Lakini ukienda kwenye soko la ajira hata hiyo serikali yenyewe inaajiri kwa kutumia lugha ya kiingereza! Sasa hapo tutamlaumu nani?

Nafikiri si sawa kuwalaumu waajiri kwa hili. Wewe kama mwajiri huna njia nyingine ya kumpima na kujiridhisha kama unayemwajiri ni mtu mwenye umahiri kwenye hilo eneo unalomtaka,zaidi ya kumsikiliza anavyoweza kuelezea mambo ya eneo hilo. Sasa kwa mswahili uliyezoea kutumia kiswahili muda wote na pengine lugha ya kabila lenu,ina maana kiingereza itakuwa ni lugha ya 2 au ya 3 kwako! Hivyo utakuwa na kazi ya kutasfiri hizo lugha zako kwenda kiingereza na wakati huohuo ukipambana na technicallity ya hicho unachopaswa kukieleza!Na hapo ndo inapokuwa tatizo,mwisho wa siku (kwa mwajiri kushindwa kukuelewa vizuri) unaonekana huna utaalamu,hufai,watatafuta mwenye kunyoosha maelezo sawasawa kwa kidhungu.

Nafikiri hizi sera zetu zinapaswa zilenge mahitaji ya soko.
 
Ngongo unayoongea ni kweli kabisa! Kuna baa moja mtaani huwa nakunywaga saa za jioni baada ya kazi nimejionea kuna wahudumu wa Kikenya wanatoa huduma! Kweli hamna rangi tutawacha kuona kwenye jumuia hii ya East Africa.
 
Back
Top Bottom