Wakazi na wenyeji wa wilaya ya Bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakazi na wenyeji wa wilaya ya Bagamoyo

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Sanda Matuta, Oct 19, 2008.

 1. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kutakua na Mkutano siku ya Jumamosi tarehe 25/10/2008 pale Urafiki Social Hall Shekilango/Nyuma ya Urafiki Police kuanzia saa Tisa jioni.

  Mkutano ni kwa ajiri ya kuzindua taasisi kwa Maendeleo ya Wilaya ya Bagamoyo ( BADEI ).

  Wageni wa waalikwa ni wabunge wetu wa wiliya,Bagamoyo mjini na Bagamoyo vijijini Mh.Kawambwa na Mh.Khalfani.

  Mnakaribishwa wote,mpe mwenzio ujumbe huu,kufika kwenu ndio mafanikio ya mkutano huu.
   
 2. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  it's about time you went back home and told your people to wake up, the rest of the country is trying to move on. Waache kukaa vibarazani na kufunga kanga vifuani, wafanye kazi!!
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jamani huko vijijini watu wanachapa mzigo sana si utani.
  Wale wavuvi wanavua kikweli kweli. Wale wa jembe wanashika jembe kikweli kwelil akini Mbona bei ya mazao ni ndogo kiasi hiki? Hata ukilinganisha na vinchi jirani utaona bei zetu ziko chini as if sisi tuna soko letu katika dunia hii tofauti na wengine. Mafundi wanafanya kazi zao lakini shida ni je where is a reward? Walimu wanafundisha kweli kweli. Madaktari kila siku wako mzigoni usiku na mchana. Na wengi kweli wako katika kazi.
  Mbona wanaofanya kazi kwa bidii kama walimu na madaktari wanalipwa pesa kidogo hata haitoshi kutumia kwa siku kumi wakati wanasiasa wao wanalipwa mamilioni kwa mamilioni! Sasa kazi kwa bidii ipi mnataka wafanye? Hapa hamuoni kwamba mnawabebesha hizo mnazoziita siasa nyinyi?
  Be fair hacheni siasa kwenye maendeleo yetu wajamani.
  Watu wanapiga mzigo kweli kweli! lakini pesa yao haina thamani. Hawana barabara zinazopitika vizuri kubeba mazao yao. Hawana zahanati na kama zipo hazina dawa. Hawana maji salama. Hawana umeme wa uhakika. Hawana mawasiliano ya bei rahisi ya simu maana bei ni kubwa kweli kweli. Wao wanaona wanavyofukuzwa katika mashamba na ardhi yao kwa compesation kidogo kwa kisingizio cha uwekezaji. Shule mpaka wajijengee wenyewe huku kodi wanalipa kama kawaida tena kubwa kuliko nchi jirani. Wanaona jinsi ambavyo sasa kwao kupata maendeleo yoyote ni hisani ya wanasiasa wala si haki yao. Ni hao hao ambao wanalazimishwa kwa kutumia vyombo vya dola kuchagua vyama tawala la sivyo wanaishia kupata vipigo tena kutoka kwa wana wao wanaolipwa kwa kutumia kodi zao. Mafuta yamekuwa yakipanda kila siku kwa kisingizio cha kuwa yamepanda katika soko la dunia lakini yakipungua bei katika soko hilo hilo hapa kwetu hayapungui! na kwa kweli matatizo ni mengi kuyaorodhesha.
  Hakuna kisingizio. Watanzania wanafanya kazi kweli kweli.
  Naona kilichobaki sasa watu kwakukata tamaa wanaona vema kujipangia na kujiamasisha kuchangia maendeleo ya makwao. Lakini wanaweza kufanya kiasi kipi? Ni kidogo maana hata wakichanga kiasi gani yako mambo mengi ya kufanya ambayo hawawezi kuyafanya yote kwa kuwa pesa hawawezi kuwa nazo za kutosha.
  Serikali haiwezi kujivua kwa majukumu yake maana serikali makini siku zote ndiyo nyenye majukumukwa watu wake.
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Sanda,

  There are many of us who are new residents of Bagamoyo. Some of us might not be in a position to be physically present at the meeting, but we would like to contribute ideas..

  The meeting should not focus on raising funds. It should focus instead on how to develop our district. To be sure, throwing money at a problem can alleviate it, but solving developmental problems requires a more holistic approach.

  I propose that a “Bagamoyo Development Association” be formed to agitate for the following concrete objectives:

  • We should tap into the conference tourism potential that we are so much blessed with. Towards this end, land should be set aside and tenders should be floated internationally for partners to join us in the construction of a major international conference center in Bagamoyo. As a sweetener, the selected area should be declared a special investment zone. It is not difficult for Bagamoyo to become the Cancun of Tanzania, but it requires initiative.
  • Land should be set aside for commercial scale horticultural investments. We live near Dar. It is time we realized that we, the people of Bagamoyo, can produce all the vegetables and fruits that the hungry masses in Dar require. Some Chinese entrepreneurs have already shown some interest in this, but there is room for national and other international investors in this.
  • We must push for a speedy implementation of that project of having all busses and trucks that ply the Dar – Arusha road pass by our town. This will open up many parts of our district. There is not just money to be made from the travelers in this, but above all, there will be exchange of ideas and added mobility of our people.
  • We must multiplicate the achievements of Marian High School. We need to encourage the Church and other institutions to build more such schools in our district, by giving them land, and by generally supporting them. We should have a committee on education. Its mandate should include making Bagamoyo the destination of choice for the education of the children of upwardly mobile young families.
  • We must agitate for an end to the situation where water pipes and power transmission lines pass by us while studiously avoiding being useful to us. We need to water and power in our villages. It can be done, and it is being done in several villages in Tanzania. Having clean water is a life and death issue. We must have it, period.
  Bwagamoyo ni kivutio kama Mombasa na Zanzibar. Ni kitega uchumi cha nguvu lakini tumekikalia tu!

  Augustine Moshi
   
 5. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mkuu Sanda je haya ni kweli,kwamba kazi yenu kukaa vibarazani na kufunga khanga?

  Ni swali tu.?
   
 6. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nia ni kuweka Tangazo,na nashukuru mmelisoma na nadhani mtawafahamisha wale wote ambao katika njia moja ama nyingine hawatoweza kufikiwa na njia hii ya mtandao.
  Pia wazaliwa wa wilaya ya Bagamoyo waishio Dar es salaam na mikoa ya karibu mnakaribiswa na hasa ndio walengwa.
  Kama hamtoweza kufika basi michango yenu ya mawazo manaweza kuweka hapa kama alivyo fanya ndugu AGUSTINO MOSHA ,na nitaiwakirisha panapo husika.


  Maswali na majibu yatapatikana hapa pia.
   
 7. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Ndugu Sanda Matuta,

  Umeniogopesha pale unaposema walengwa wa mkutano hasa ni “wazaliwa wa Wilaya ya Bagamoyo” waishio mikoa ya karibu. This sounds very parochial! Huoni huu ni wakati wa kuwa wapana zaidi kwenye mitazamo yetu?

  Wako wenyeji wa Bagamoyo ambao hawakuzaliwa Bagamoyo. Hao si “walengwa hasa”? Wako pia wazaliwa wa Bagamoyo ambao sio wenyeji wa Bagamoyo.

  Bagamoyo itajengwa na wale wanaoipenda. Baadhi ni wazaliwa wa Bagamoyo, wengine ni wenyeji tu wa Bagamoyo, na wengine wanaweza wasiwe hata Watanzania.

  Na definition yako ya "mzaliwa wa Bagamoyo" ni ipi hasa? Ni mtu ambaye umbilical chord yake ilipokatwa alikuwa Bagamoyo? Hawapo wazaliwa wa Bagamoyo ambao hawakuzaliwa Bagamoyo?
   
 8. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Asante Ndg.Augustine Moshi (ni samehe kwa kutolitamka vizuri mwanzo)

  Umesema vyema,ni kweli niliweka msisitizo kwa WAZALIWA ila kama utasoma vizuri Bandiko la kwanza ni kwa wakazi na wenyeji wa wilaya yetu.Usipate shaka kwa huo msisitizo kwani utakubaliana na mimi kwamba, in order tupate suruhisho la pamoja la maendeleo yetu na wilaya kwa ujumla lazima tupate msaada wa WAZALIWA wa sehemu usika.
  Bagamoyo have been lag behind kwa muda mrefu na tunawahitaji hao jamaa watuambie wapi wamekuwa wakikwama na sisi kama kizazi kipya kutoka sehemu zote za Tanzania tusaidie katika kuleta maendeleo.

  Karibuni wote.

  Nimesikia kutoka kwa Muasisi kwamba wengi wanataka kujaa,basi njooni wote tafadhali
   
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Vigezo gani vinatumika kumtofautisha mkazi na asie mkazi wa Bagamoyo? I mean kuna aina ya vitambulisho au ukifika unaingia tu maana wengine tuna mashamba Bagamoyo lakini tunaishi Dar hii vp inakubalika?
   
 10. M

  Mama JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Bagamoyo ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii Afrika mashariki. Potential ya maendeleo ya utalii ni kubwa sana kwa mji huu ila tatizo kubwa ni miundo mbinu na hali duni ya wakazi wake, jambo linalorudisha nyuma msisimko katika mji huu.

  Kwa sasa tatizo la miundombinu linakaribia kufukia tamati, kwa mfano kuna barabara ya lami inayounganisha mji huu na ule wa Dar es Salaam. Pia kuna mpango wa barabara ya lami itakayounganisha mji huu na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania kupitia Segera. Je ule mradi port ya kimataifa hapo Bagamoyo, mradi huu unafadhiliwa na serikali ya Tanzania au kuna mfadhaili? Kama yupo mfadhili ni nani huyo?

  Pia Nawatakia kila la heri katika mkutano huu.
   
 11. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Mama,

  Bandari ya kimataifa itahitaji kuweko kwanza na reli na barabara za nguvu. Maana huwezi ukashusha mizigo ya Rwanda, Burundi, Uganda, na Zaire mahali ambapo hakuna reli na barabara za kuiondolea.

  Muungwana wetu ana tatizo la "maneno mengi, matendo hakuna"! Ajenge viunganisho vya reli, barabara na kiwanja kikubwa cha ndege hapo kwetu Bagamoyo kabla hajazungumzia bandari ya kimataifa.

  Mji wa Bagamoyo ni sehemu ndogo ya Wilaya ya Bagamoyo. Ni tumaini langu kwamba mkutano utazungumzia namna ya "kuifungua" Bagamoyo yote. Misingi ni Elimu, Maji, Barabara, Umeme na Kilimo cha umwagiaji.

  Mradi wa awali ambao unaweza kuongeza sana mzunguko wa fedha Bagamoyo ni huo wa conference tourism. Makampuni na mashirika ya Dar, ya sehemu nyingine za Tanzania, na hata ya kimataifa yangependa kufanya mikutano yao Bagamoyo. Kunahitajika conference center ya nguvu. Wawekezaji watapatikana, maana kipo chakula hapo. Wapewe mwaliko na vivutio tu, na utawaona.
   
 12. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Umeonyesha kwamba unaweza kuwa sehemu ya ufumbuzi,karibu.
   
 13. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Nitasikitika nikikukosa mkutanoni,but i hope you can make it.
  However,nitachukua hizi proposal /maono yako na tutaanzia hapo katika kuweka mipango.

  Wengine wote hata kama si Wabagamoyo na mnaufahamu mji na mngependa kuona ukiendelea na wakazi wake wakajikwamua katika hari ngumu,tafadhali kama mna na mipango kabambe mnaweza kuweka hapa.
   
 14. Sanda Matuta

  Sanda Matuta JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 950
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna vitambulisho Mkulu,

  Njoo tena njoo kifua mbele
   
 15. Kipunguni

  Kipunguni Senior Member

  #15
  Oct 24, 2008
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa sifahamu kwamba Bagamoyo ina wabunge wawili!
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono, mwaka 2008 hii tabia ya Watanzania kubaguana inabidi ipigwe vita. UDSM nasikia wamepiga marufuku kabisa hivi vikundi vya kikabila. Pamoja na kuwa kuna umuhimu wa mikutano kama hii, lakini badala ya walengwa kuwa ni 'wazaliwa' tu wa sehemu husika pia wakazi waliohamia katika sehemu hiyo pamoja na kuwa si wazaliwa wa hapo wahusishwe maana na wao wanaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine katika kuleta maendeleo ya haraka ya eneo hilo. Tuweke mbele Utanzania badala ya ukabila. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
   
 17. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2008
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ningekua mchaga mjasiriamali ningeenda na kusikiliza mikakati yao halafu nawa overtake. Wahini vihamba huko jamani, manake jamaa hawa maneno mengi matendo kiduchu. Ila nachukia kweli mambo ya ukabila huu, zile zama za kusafiri Dar-Mwanza bila kuulizwa kabila na jirani yako katika seat (unless you have some salient features of a certain tribe) sijui zinapotea au?
   
Loading...