py thon
JF-Expert Member
- Sep 11, 2016
- 2,471
- 4,424
Serikali ya CCM chini ya Rais Samia inajitahidi kuipa vipaumbele Simba na Yanga kwa kuwaahidi million 10 kwa kila goli lakini inaendelea kuua vipaji kwa watoto
Eneo la Mtoni Mashine ya maji /Mtongani
Mkuu wa wilaya pamoja na halmashauri wapo kwenye mpango wa kuua uwanja wa mpira au open space na wanataka waugeuze uwanja kuwa eneo la mashimo ya mavi.
Wakazi wa mtoni mashine ya maji wamepinga kwa umoja suala hilo wakisema kwanza kuweka mashimo ya maji taka kwenye uwanja huo kuhatarisha afya ya wakazi na watoto haswa kipindi cha mvua
Pili watoto na vijana walikuwa wanatumia uwanja huo kufanyia mazoezi na kucheza mpira hivyo vijana watakosa sehemu ya kuchezea
Uwanja wa mashine ya maji complex imetoa vipaji vingi vya mpira tokea miaka na miaka na pia ndio viwanja vichache vilivyobakia eneo la azimio na mtongani.
Mkuu wa wilaya aliahidi kuitisha tena mkutano na wakazi wa eneo hilo mara baada ya kuona upingaji mkubwa wa suala hilo kutoka kwa wananchi lakini siku ya mkutano awamu ya pili hakutokea bali yalisikika malalamiko tu kuwa wakazi wa mtoni mashine ya maji ni wasumbufu
Mheshimiwa Rais tusaidie wakazi wa Mtongani Mtoni mashine ya maji uwanja wetu pekee wa mpira unataka uporwe na ugeuzwe kuwa mashimo ya mavi.