DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 161
- 200
WAKAZI wa Mbopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wameshangazwa na rafu wanazofanyiwa na Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) hali ambayo inawashangaza na kutojua hatma yao.
Wakazi hao wanalakamika hivyo ingawa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule na kamati ya ardhi lakini baadhi ya wajanja wanafanya mambo nje ya makubaliano na wakazi hao.
Walisema mikutano hiyo mitatu na Mkuu wa Mkoa ilifanyika mara tatu kuanzia Januari, Mei na Julai, 2025
Chalamila aliagiza wakazi hao waendelee na maisha yao ila walipe gharama kwa Square meter moja ni shilingi 3000.
Chalamila akaagiza maeneo ya wazi yauzwe kwa mtindo wa serikali (TAUSI) square meter moja kwa shilingi 15,000, 17,000 na 20,000 na hakuna mkazi aliyekataa, lakini wakazi hao wanashangazwa na viwanja hivyo kuuzwa mara mbili mbili 'Double allocations'.
Changamoto nyingine wanalazimishwa kujenga vibanda kwa maana ya uhalali. Changamoto nyingine ni uboreshaji wa miundombinu ya barabara inayoendelea kwa sasa.
Ukubwa wa barabara ukubwa wake mita 30, ukubwa huo unaathiri baadhi ya maeneo ya wakazi ambako wanatakiwa kutumia busara.
Wanashukuru miundombinu mingine kama maji, shule na umeme.
Aidha wakazi hao wanaeleza kwamba watu wenye maeneo yao wapewe kipaumbele kwa mujibu wa sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu cha 44-55, ambacho kinaeleza kwamba wapewe taratibu zinazohusiana na malipo watakaoshindwa, serikali ichukue sheria yake.