Wakatoliki, hiki ni nini kinachofanyika hapa?

Wakatoliki, hiki ni nini kinachofanyika hapa?

Kwa hiyo unasemaje sasa, kinachofanyika hapo ni ibada ya sanamu kama vile kurusha jiwe unaona ni ibada ya sanamu? Kama kurusha jiwe ni ibada ya sanamu kunahalalishaje kukiramba hicho kisanamu?

Kumbuka pia, kuramba kisanamu kulianza kabla ya kurusha jiwe.
Basi vyote sawa usirushie mawe watu na unajua unaishi nyumba ya vioo
 
Kama wewe siyo mkatoliki, ibada yaoa inakuhusu nini?
Aaah, kumbe kuna wakati wa kusema tunaabudu Mungu mmoja na wakati wa kusema ibada yao inakuhusu nini.

Ikiwa Mungu aliekataza kuabudu sanamu upande mmoja ndie huyo huyo alieruhusu kuabudu sanamu upande wa pili, basi sisi ni watu wa kuhurumiwa sana. Tule, tunywe, tuishi maana kesho tutakufa na hakuna Mungu.

Mungu angekuwapo asingetokeza confusion zote hizi.
 
Hizo ni ibada za sanamu, sema tinaheahimu watu na ibada zao coz kila mtu ana uhuru na kile anachoamini.
 
Aaah, kumbe kuna wakati wa kusema tunaabudu Mungu mmoja na wakati wa kusema ibada yao inakuhusu nini.

Ikiwa Mungu aliekataza kuabudu sanamu upande mmoja ndie huyo huyo alieruhusu kuabudu sanamu upande wa pili, basi sisi ni watu wa kuhurumiwa sana. Tule, tunywe, tuishi maana kesho tutakufa na hakuna Mungu.

Mungu angekuwapo asingetokeza confusion zote hizi.
Kumwabudu Mungu ni kitu kimoja; modaities za kuabudu ni kitu tofauti kabisa. Kila dini wana modalities zao.
 
Kuna mtu anaweza kunishawishi kwamba hii sio ibada ya sanamu?
Kama haikuhusu wewe inakuwasha nini? Waislam wanavyozunguka kule macca na kumpiga shetani wala hainisumbui kwa sababu hainihusu!
 
Kama haikuhusu wewe inakuwasha nini? Waislam wanavyozunguka kule macca na kumpiga shetani wala hainisumbui kwa sababu hainihusu!
Yesu aliumia alipoona wakazi wa Yerusalemu wakipotezwa na shetani. Akalia laiti mngelijua yapaswayo kufanywa. Sasa kama wewe ni mfuasi wake kweli, m-Kristo, ikiwa unaona watu wanapotea katika imani zao na utasema haikuhusu? Kwa hiyo Yesu alipaswa kusema haimhusu kama unavyosema wewe, au wewe ungemwambia Yesu inakuwasha nini hadi uwalilie watu wa Yerusalem wakipotea katika imani yao?

Huna dini wewe, unajisemea Bwana Bwana tu lakini ulishakataliwa.
 
Katika madhehebu ya kikristo , wanaojitambua zaidi ni wakatoloki , nafikiri wao wanaelewa zaidi ya wanachokifanya , na pia wana elewa madhebu mengine yote kuliko hata wao wenyewe wanavyojielewa
 
Mimi mwenyewe Mkatoliki kweli na wala sihangaiki na mtu anayebeza imani za wenzake. Wewe hapo unaona wanaabudu sanamu kumbe Sisi tunajua tunachokiabudu hapo. Sisi tunajua kwamba ni wokovu ndio uliotundikwa juu ya huo mti wa msalaba! Ndiyo maana Padre anapouleta altareni anatualika kwamba "Huu ndio mti wa msalaba ambao wokovu wa dunia umetundikwa juu yake njooni, njooni, njooni tuuabudu". Tunauabudu kwa sababu juu yake kumetundikwa wokovu wa dunia! Kwa hiyo ndugu huna nafasi ya kuwahukumu Wakatoliki maana hiyo ndiyo imani yao!
 
Katika madhehebu ya kikristo , wanaojitambua zaidi ni wakatoloki , nafikiri wao wanaelewa zaidi ya wanachokifanya , na pia wana elewa madhebu mengine yote kuliko hata wao wenyewe wanavyojielewa
Min-me asante sana kwa huo msumari!
 
Kwa kila mtu , ukiongelea ukristo umegusa katoliki wengine ni waasi
Ukristo uliingia Roma karne ya nne baada ya Mtawala wa Roma Constantine kukubali kuwa Mkristo na kuifanya dini ya Kikristo kuwa dini ya taifa, na kuieneza kwa lazima katika milki yake yote. Kabla ya hapo Roma waliua na kunyanyasa Wakristo, kuwatumia kwenye michezo kwa kuwapambanisha na wanyama wakali kama simba nk. Hata Yesu mwenyewe aliuwawa na askari wa Roma, sio Wayahudi kama wengi wanavyodhani. Waliompigilia misumari na kumtundika ni askari wa Roma, Wayahudi walishabikia tu kwa kelele. Malmala ya kukataa Yesu asiuwawe au kusulubiwa yalikuwa kwa Waroma.

Sasa wengine watakuaje waasi dhidi ya Romans Catholics wakati Waroma ndio walikuwa wauaji wa wakristo kisha "wakaokoka"?
 
Ukristo uliingia Roma karne ya nne baada ya Mtawala wa Roma Constantine kukubali kuwa Mkristo na kuifanya dini ya Kikristo kuwa dini ya taifa, na kuieneza kwa lazima katika milki yake yote. Kabla ya hapo Roma waliua na kunyanyasa Wakristo, kuwatumia kwenye michezo kwa kuwapambanisha na wanyama wakali kama simba nk. Hata Yesu mwenyewe aliuwawa na askari wa Roma,sio Wayahudi kamawengi wanavyodhani. Waliompigilia misumari na kumtundikani askari wa Roma, Wayahudi walishabikia tu kwa kelele.

Sasa wengine watakuaje waasi dhidi ya Romans Catholics wakati Waroma ndio walikuwa wauaji wa wakristo kisha "wakaokoka"?
Katoliki ni ukristo wenyewe na ukristo ni ukatoliki.

Mfumo wote wa siku ya ibada , ishara zote za kiibada, biblia, sakramenti , ubatizo , ndoa, ekarisilti , sikuu zote za kikristo, haya yote makanisa mengi yamepokea tu kutoka kanisa la katoliki.

Hivyo kanisa katoliki linajua wanachokifanya , na hata wangekuwa wameamua wangeweza kuongeza wanayotaka ndani ya Biblia, na kila mmoja angefuata tu
 
Mimi mwenyewe Mkatoliki kweli na wala sihangaiki na mtu anayebeza imani za wenzake. Wewe hapo unaona wanaabudu sanamu kumbe Sisi tunajua tunachokiabudu hapo. Sisi tunajua kwamba ni wokovu ndio uliotundikwa juu ya huo mti wa msalaba! Ndiyo maana Padre anapouleta altareni anatualika kwamba "Huu ndio mti wa msalaba ambao wokovu wa dunia umetundikwa juu yake njooni, njooni, njooni tuuabudu". Tunauabudu kwa sababu juu yake kumetundikwa wokovu wa dunia! Kwa hiyo ndugu huna nafasi ya kuwahukumu Wakatoliki maana hiyo ndiyo imani yao!
In short, mnaalikwa mkaabudu sanamu,ambayo mnaipa utukufu mkubwa.

Kama hamuabudu sanamu naweza kumpa mtoto kile kisanamu achezee kama toi? Kwani Yesu aliposema anatafuta watu wanaomuabudu kwa imani alimaanisha nini? Au alipomwambia Tomaso hadi uniguse ndio uamini?

Kama ili kuabudu Wakatoliki lazima watumie hicho kisanamu kwa kukigusa, basi hawana tofauti na Tomaso!
 
Back
Top Bottom