Wakati wa Utawala wa Mobutu huyu mzee alikuwa mtu wake wa karibu sana

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Pichani ni aliyekuwa mshauri mkuu wa rais wa Zaire kwa sasa DRC MOBUTU SESESEKO.

Wakati wa Utawala wa Mobutu huyu mzee alikuwa mtu wake wa karibu sana na alikuwa na kazi ya kumpa ushauri ambapo aliweza kumshauri mambo mengi sana,

Alimshauri Mobutu ajilimbikizie mali, alimshauri Mobutu amuue kikatili Pierre Mulele eti kwa kuwa tu alikuwa ni rafiki wa Lumumba na pia kwa hofu ya kupatikana mtu wa kuwaletea Upinzani madarakani.

Aliishi maisha ya starehe yeye na Mobutu Seseseko huku wakila bata vilivyo kwenye makasri na kutembezwa kwenye meli yao ya mv KAMANYOLA

Walikula maisha huku wananchi wakiogelea kwenye umasikini wa kutupwa, Watu wengi sana waliuwawa kinyama chini ya Ushauri wa huyu mzee.

Sasa baada ya Mobutu kupinduliwa huyu mzee alikosa wenyewe alirudi mtaani na kwenda kuishi na zile familia alizokuwa akizionea wakati akiwa Ikulu na Mobutu, alikwenda kuishi na familia ambazo zilipoteza wapendwa wao kwa ushauri wake wa kidhalimu.

Hata hivyo bado yupo hai Mungu ameamua kumuadhibu kwa njia hii, anapatikana jijini kinshasa ambapo ni Masikini fukara na anaishi kwa maisha ya kuombaomba mitaani

Yaani Kutoka Ikulu alipokuwa anakula pweza na mivinyo ya Ufaransa hadi mitaani ambapo anaishi kwa taabu na kulishwa kwa masimango.

Tukio hili ni funzo sana kwa watu wenye Madaraka, wakumbuke kuishi vizuri na watu kwani ipo siku Mungu atakushusha kutoka huko ulipo hadi mitaani ambapo utaenda kuishi na Wale wanyonge uliokuwa unawaona siyo kitu mbele zako.

wakumbuke kuwa...

ALIYE JUU MGOJE CHINI

DUNIA NI TAMBARA BOVU

.... LISSU anatosha...
FB_IMG_1598521121023.jpg
 
Watu wengine sijui pesa wanaichukuliaje, unakuta mtu anamiliki 1bilion kisha baada ya miaka 10 au 20 anafirisika.

Huu ni upuuzi, akili ni ndogo kabisa bii. Huyu mzee kabla hatujafika kwa Mungu ila na yeye pia akili hana.

Utajiri wa Mobutu ulikuwa ni mkubwa mno, bila shaka huyu mzee na yeye hata 10bilion zilikuwa hazimpigi chenga.
 
Mobutu alikuwa kibaraka wa mabeberu kama hii leo alivyo Lissu.ona mwisho wa vibaraka ulivyo,hata Lissu urais atopata na mwisho wake utakuwa mbaya sana.
 
Huyu Mzee hana tofauti na wale wanaobeza maendeleo ya Tanzania na hasa miundo mbinu. Kwa mfano Hospitali na vituo vya afya vimejengwa vingi sana na awamu ya 5. Lakini ati anatokea mtumishi wa serikali awamu za huko nyuma anakashifu.

Huyu anaye kashifu anasahau tukiweka mizania ya watu wa Tanzania waliokufa kwa magonjwa na kwa sababu ya uzembe wake na ufisadi alioshiriki na kuuendekeza wakati akiwa ofsini wanawazidi waliouwawa na Mabutu na Iddi Amini.
 
Kama ni kweli, hata mtoa mada anapaswa kuishi maisha matakatifu, maana maisha ya kuwatendea wengine mema inaanza na nafsi kisha iende Kwa unayewanyoshea vidole

Wasaidie wasiojiweza, wape chakula wasio nacho, wavishe wasio na nguo, wahudumie wahitaji Kwa ule Uwezo wako na Baada ya hapo, wakumbushe na kuwanyoshea vidole na wengine

Maisha haya tunapita tu, kifo cha masikini na tajiri Bado ni kilekile, kaburi ni lilelile

Mkabidhi Mungu maisha yako nawe utathibitika njia zako
 
Back
Top Bottom