Fahamu jinsi Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga alivyo wahadaa Maafisa wa CIA

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,222
53,039
Ni mwaka 1974 kulitarajiwa kuwa na pambano kubwa sana kati ya Muhammad Ali na George Foreman. Wakati huo, promota aliyekuwa akija kwa kasi, Don King alikuwa amekwishaandaa kila kitu kuhusu pambano hilo.

Kwa ajili ya msalahi yake, Don King alitaka mtu yeyote atakayejitolea kulidhamini pambano hilo basi atoe dola milioni sita ambazo kwa kipindi kile kilikuwa kiasi kikubwa sana cha pesa. Jamaa akaanza kusubiri wadhamini lakini wapi. Hakuna aliyejitokeza.

Usiku mmoja wa Ijumaa ya tarehe 21 mwezi Desemba, simu yake ikaanza kuita, kwa uchovu akaamka na kwenda kuipokea, sauti aliyoisikia ilikuwa ya mwanaume ambaye hakumtambua alikuwa nani, ilikuwa sauti ya mwanaume mwenye pesa nyingi, rais kutoka nchini Zaire, Mobutu Seseko.

Mwanaume huyo akajitambulisha, wakaanza kuzungumza, alichomuuliza ni kitu kimoja tu, je, umekwishapata mdhamini wa pambano hilo? Don King akajibu hapana. Basi rais huyo akataka kuwekeza.

“Toa dola milioni sita na gharama zote utagharamia wewe,” alisema Mobutu.
“Haina shida. Badala ya dola milioni sita, nitakupa dola milioni kumi,” alisema Mobutu kwa majigambo.

Hakukuwa na kitu kilichoshindikana. Kipindi hicho kumbuka huyu Mobutu alikuwa akitafutwa sana na maofisa wa CIA ili wammalize. Walitumia kila njia kufanikisha suala hilo lakini ilishindikana, walifanya kila kitu lakini wapi.

Moburu alilifahamu hilo, alichomwambia Dok King ni kwamba anataka pambano hilo likafanyikie nchini Zaire. Don King akashangaa, iliwezekanaje hilo litokee? Ila kwa sababu huyu mwanaume aliahidi kutoa kiasi kikubwa cha pesa, akakubaliana naye.

Pambano likafanyike nchini Zaire? Kila mtu aliyesikia hilo alishangaa sana, ilikuwaje pambano kubwa la ndondi likafanyikie barani Afrika? Kwani Marekani tumekosa ulingo bora? Mbona hili likifanyikia Marekani litakuwa poa sana, sasa mdhamini alitaka pambano hilo likafanyikie huko.

Haraka sana akachukua simu na kuwapigia mameneja na wapigaji na kuwapa taarifa kuhusu pambano hilo kufanyikia Zaire, hakukuwa na aliyepinga, wao walichokitaka ni kupigana na kuingiza pesa.

Siku zikakatika na hatimaye siku ya pambano hili lililoitwa The Rumble In The Jungle likaanza kufanyika huko Zaire pale Kinshasa. Siku hiyo waliingiza watu elfu sitini. Kila mmoja alikuwa na shauku la kulitazama pambano hilo la ubingwa wa dunia.

Muda ulikwenda, aliyekuwa akisubiriwa ni rais wa Zaire ambaye alikuwa mgeni rasmi afike hapo ukumbini. Mobutu akaamua kumuagiza kijana wake aende kuwaambia tu waendelee na mchezo kwani yeye hatokuwepo, naye atafuatilia pambano hilo kwenye televisheni.

Hilo likamshangaza kila mtu lakini yeye alijua anamaanisha nini. Wakati huo tayari CIA walikwishaandaa wadunguaji wao kwa lengo la kummaliza rais huyo. Walitaka kumuona akienda ukumbini, wammalize lakini baada ya kuambiwa kwamba hatokwenda, kila mmoja alichoka.

Walipanga mpango mkali sana wa kummaliza lakini hilo halikufanikiwa. Rais hakuibuka ulingoni hivyo kila mkakati wao waliokuwa wameupanga kwa muda ulifeli usiku huo.

Pambano lilifanyika, Mohamed Ali alishinda na kumpa umaarufu zaidi kwenye mchezo wa ndondi.
FB_IMG_16859759581951522.jpg
 
Ni mwaka 1973 kulitarajiwa kuwa na pambano kubwa sana kati ya Muhammad Ali na George Foreman. Wakati huo, promota aliyekuwa akija kwa kasi, Don King alikuwa amekwishaandaa kila kitu kuhusu pambano hilo.

View attachment 2647046
Pambano lilifanyika 1974..
 
Unge acknowledge Mtoa hii Taarifa maana ni muda ipo kwenye mitandao. Whatsapp na Twitter.
 
Back
Top Bottom