Today on history: Rais wa Zaire Mobutu Seseko alifanya maamuzi ambayo yaliishangaza dunia

Mohamedex121

JF-Expert Member
Jan 27, 2022
1,688
3,139
Tarehe 21 ya Desemba 1973, Rais wa Zaire Mobutu Seseko alifanya maamuzi ambayo yaliishangaza dunia. Siku hiyo ya Ijumaa, majira ya saa tatu na nusu usiku akiwa kwenye jumba lake la kifahari, akachukua simu na kupiga masafa marefu. Mpokeaji akawa mmarekani Don King, promota maarufu zaidi wa mchezo wa Ngumi za kulipwa.

Don?

Ndiye. Nani mwenzangu?

Mobutu Sese Seko!

Ooh Mr. President!? Don King akashindwa kuficha mshangao wake.

Nimesikia unahitaji mfadhili wa pambano la Mohamed Ali na George Foreman? Akahoji Mobutu. Hakuwa mtu wa maneno mengi.

“Ndiyo, lakini Hadi sasa hakuna aliyefika bei.....”

Bei yake ikoje? Akahoji Mobutu, hakutaka maongezi marefu na Don.

“Dola milioni 6, halafu unagharamia kila kitu kwa ajili ya maandalizi....”

“Haina shida, nitakupa dola milioni 10. Halafu nitagharamia kila kitu, ila pambano lipigiwe hapa Kinshasa. Hapo vipi? Alisema Mobutu kwa mkato.

“Unataka pambano lifanyike lini?

“Hata kesho! Akajibu Mobutu.

“Hapana. Tutafanya mwakani!

Pambano likaitwa The Rhumble in the Jungle! Inasemwa kuwa pengine ndiyo pambano maarufu zaidi la karne iliyopita. Likitazamwa na watu zaidi ya bilioni moja kwa njia ya TV. Hiyo bilioni moja ni mwaka 1974.

Siku ya pambano ikifika. Ilikuwa Octoba 29 ya mwaka 1974. Unaambiwa TV ilianza kuonyesha matukio kuanzia saa nne asubuhi, huku pambano lenyewe likipewa jina THE RHUMBLE IN THE JUNGLE. Pambano ambalo kwa mara ya kwanza Mohamed Ali alichukua ubingwa wa dunia kwa kumpiga George Foreman. Ndilo pambano lilimtambulisha haswa Mohamed Ali kwenye ulimwengu wa masumbwi. Mtu mweusi huyu alichezea pambano hilo kwenye ardhi yake ya asili, kwa hisani ya mbabe Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga

Lengo kubwa la kukusimulia kisa hiki ni kukufunulia tukio moja lililotokia siku ya pambano. Tukio ambalo wengi hawalijui. Tukio ambalo kama lingeenda kama baadhi walivyokuwa wamepanga, pengine lingekuwa kubwa kuliko lile la pambano la Ngumi.

Wakati imebaki saa moja pambano lianze, Mobutu alikuwa bado hajaondoka nyumbani kwake. Nyumba iliyokuwa kilomita chache sana toka ulipokuwa ukumbi ambao ungetumika. Ukumbi umeshajaa watu zaidi ya 60,000, huku maelfu ya vituo vya televisheni duniani kote yameshatega macho yao kuwaonyesha watu zaidi ya bilioni moja ile miamba hao wangefanyana ulingoni. Kila mmoja alikuwa tayari kutazama pambano la raundi 15.

Wakati kila kitu kiko tayari, mgeni rasmi anangojewa, Mobutu Sese Seko akamwita mtu wake wa mawasiliano. Akataka amuoneshe picha ambazo yeye Mobutu amepiga na mabondia wote wawili, wakiwa maeneo mbalimbali ya Kinshasa, tangu walipowasili. Akazingalia, akatabasamu. Alijiridhisha kuwa, alishakamua picha za kutosha tu, alitaka nini kingine?

Waambieni waendelee na mpambano, sitaenda ukumbini, nitaangalia pambano kutokea hapa sebuleni kwangu! Alisema huku akiwa amekumbatia mtoto wa Chui.

Mobutu kulipa dola milioni 10, halafu kugharamia kila kitu kwa ajili ya pambano ili tu lipigwe Kinshasa halafu siku ya pambano unatazama kwenye runinga?!!

Uamuzi huu si tu uliwaacha hoi waandaaji na maafisa wa Ikulu, bali uliwaudhi sana shirika la ujasusi la Marekani na makundi ya waasi ya Congo. Maana kwa nyakati tofauti na mazingira tofauti wadunguaji (Snipers) wa CIA na waasi wa Congo walikuwa wameshajiandaa kwa muda mrefu, tayari walikuwa kwenye maeneo yao kuhakikisha Mobutu Sese Seko anauaa siku hiyo kwenye ukumbi wa pambano la ngumi. Uamuzi huu wa Mobutu ulimaanisha kuwa maandalizi yao na mikakati ya ilikuwa imepigwa chenga ya mwili.

Na kweli, Mobutu alitazama The Rhumble in the Jungle akiwa kwenye sebule ya nyumbani kwake!

Tembea uyasikia na kuyapata mambo matamu ya Afrika yetu hii! Ndiyo maana napenda kuizunguka Afrika yetu, ana mazuri mengi na watamu wengi kuliko upande uleeeeeee!

Pichani: Mobutu akiwa na mabondia wote wawili na Don King
1684415787564.jpg

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Duuuhh, alikuwa na intelligence kali au uchawi ulimjulisha? Mbona tunaambiwa Mobutu alikuwa Rafiki mkubwa wa Marekani?
Mobutu alikuwa ana urafiki mkubwa na CIA na ikulu ya Washington.

Sema tu alikuwa haamini watu wake wa karibu na ndio maana haishangazi alikuwa akisafiri kwenda nje ya nchi aliambatana na Mkuu wa shirika la ujasusi, mkuu wa majeshi, igp na funguo za maghala ya silaha zilikuwa kwenye briefcase yake
 
Tarehe 21 ya Desemba 1973, Rais wa Zaire Mobutu Seseko alifanya maamuzi ambayo yaliishangaza dunia. Siku hiyo ya Ijumaa, majira ya saa tatu na nusu usiku akiwa kwenye jumba lake la kifahari, akachukua simu na kupiga masafa marefu. Mpokeaji akawa mmarekani Don King, promota maarufu zaidi wa mchezo wa Ngumi za kulipwa.

Don?

Ndiye. Nani mwenzangu?

Mobutu Sese Seko!

Ooh Mr. President!? Don King akashindwa kuficha mshangao wake.

Nimesikia unahitaji mfadhili wa pambano la Mohamed Ali na George Foreman? Akahoji Mobutu. Hakuwa mtu wa maneno mengi.

“Ndiyo, lakini Hadi sasa hakuna aliyefika bei.....”

Bei yake ikoje? Akahoji Mobutu, hakutaka maongezi marefu na Don.

“Dola milioni 6, halafu unagharamia kila kitu kwa ajili ya maandalizi....”

“Haina shida, nitakupa dola milioni 10. Halafu nitagharamia kila kitu, ila pambano lipigiwe hapa Kinshasa. Hapo vipi? Alisema Mobutu kwa mkato.

“Unataka pambano lifanyike lini?

“Hata kesho! Akajibu Mobutu.

“Hapana. Tutafanya mwakani!

Pambano likaitwa The Rhumble in the Jungle! Inasemwa kuwa pengine ndiyo pambano maarufu zaidi la karne iliyopita. Likitazamwa na watu zaidi ya bilioni moja kwa njia ya TV. Hiyo bilioni moja ni mwaka 1974.

Siku ya pambano ikifika. Ilikuwa Octoba 29 ya mwaka 1974. Unaambiwa TV ilianza kuonyesha matukio kuanzia saa nne asubuhi, huku pambano lenyewe likipewa jina THE RHUMBLE IN THE JUNGLE. Pambano ambalo kwa mara ya kwanza Mohamed Ali alichukua ubingwa wa dunia kwa kumpiga George Foreman. Ndilo pambano lilimtambulisha haswa Mohamed Ali kwenye ulimwengu wa masumbwi. Mtu mweusi huyu alichezea pambano hilo kwenye ardhi yake ya asili, kwa hisani ya mbabe Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga

Lengo kubwa la kukusimulia kisa hiki ni kukufunulia tukio moja lililotukia siku ya pambano. Tukio ambalo wengi hawalijui. Tukio ambalo kama lingeenda kama baadhi walivyokuwa wamepanga, pengine lingekuwa kubwa kuliko lile la pambano la Ngumi.

Wakati imebaki saa moja pambano lianze, Mobutu alikuwa bado hajaondoka nyumbani kwake. Nyumba iliyokuwa kilomita chache sana toka ulipokuwa ukumbi ambao ungetumika. Ukumbi umeshajaa watu zaidi ya 60,000, huku maelfu ya vituo vya televisheni duniani kote yameshatega macho yao kuwaonyesha watu zaidi ya bilioni moja kile miamba hao wangefanyana ulingoni. Kila mmoja alikuwa tayari kutazama pambano la raundi 15.

Wakati kila kitu kiko tayari, mgeni rasmi anangojewa, Mobutu Sese Seko akamwita mtu wake wa mawasiliano. Akataka amwomyeshe picha ambazo yeye Mobutu amepiga na mabondia wote wawili, wakiwa maeneo mbalimbali ya Kinshasa, tangu walipowasili. Akazingalia, akatabasamu. Alijiridhisha kuwa, alishakamua picha za kutosha tu, alitaka nini kingine?

Waambieni waendelee na mpambano, sitaenda ukumbini, nitaangalia pambano kutokea hapa sebuleni kwangu! Alisema huku akiwa amekumbatia mtoto wa Chui.

Mobutu kulipa dola milioni 10, halafu kugharamia kila kitu kwa ajili ya pambano ili tu lipigwe Kinshasa halafu siku ya pambano unatazama kwenye runinga?!!

Uamuzi huu si tu uliwaacha hoi waandaaji na maafisa wa Ikulu, bali uliwaudhi sana shirika la ujasusi la Marekani na makundi ya waasi ya Congo. Maana kwa nyakati tofauti na mazingira tofauti wadunguaji (Snipers) wa CIA na waasi wa Congo walikuwa wameshajiandaa kwa muda mrefu, tayari walikuwa kwenye maeneo yao kuhakikisha Mobutu Sese Seko anauawa siku hiyo kwenye ukumbi wa pambano la ngumi. Uamuzi huu wa Mobutu ulimaanisha kuwa maandalizi yao na mikakati ya ilikuwa imepigwa chenga ya mwili.

Na kweli, Mobutu alitazama The Rhumble in the Jungle akiwa kwenye sebule ya nyumbani kwake!

Tembea uyasikia na kuyapata mambo matamu ya Afrika yetu hii! Ndiyo maana napenda kuizunguka Afrika yetu, ana mazuri mengi na watamu wengi kuliko upande uleeeeeee!

Pichani: Mobutu akiwa na mabondia wote wawili na Don KingView attachment 2626507

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
Naona Don King yuko pembeni anawaza hela.
 
57 Reactions
Reply
Back
Top Bottom