Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Aisee, nakumbuka chuo boom limekata maisha magumu mno, nikafikiria nifanyaje, nikapata mawazo ya biashara nikaanza...
kuuza bubblegum/bigijii hizi super golila @500, nikanunua 8000 pakti ukiuza faida ni 5000 hivi, nashukuru ilikua tukienda class kabla lecture haijaanza nawatangangizia nnazo so wanachukua fresh,namaliza hata pkt 2 per day.

Nikaona niongeze biashara ya biscuits fulani hivi tamuu, nilikua nanunua pakti ya biscuit sh 900 nakuja kuuza 2000/=

Nikaongeza biashara ya crips za ndizi, nilikua napika mwenyewe nakumbuka nilikua nakaa hostel na hamruhusiwi kupika, so nikamuomba rafiki yangu alikua amepanga nje ya hostel nikawa napikia huko, nakumbuka siku ya kwanza nimepika crips hazikukauka vizuri dah,lainii kufika nazo hostel roommates wakanichekaa ila nilikomaa nikaziuza zingine nikawapa wale tu, siku 2, nikapika zimeungua nilikua nashindwa kukadiria moto, baada ya hapo nikawa napika vizurii, nikapeleka hadi blocks za wakaka faster zinaisha, napigiwa simu nipeleke zingine kama zipo hadi raha, faida ilikua ni nusu kwa nusu.

Nakumbuka nilikusanya faida hadi nikapata mtaji wa viatu flani vya kimasai ambao ulinisaidia hadi nilivomaliza chuo nikaendelea nao, nikafanikiwa kusave hadi sh 70,000/= per week kwa hiyo biashara,nakumbuka nilikua namsaidia hadi babe wangu vihela kidogo vya vocha,kabla hajapata kazi, japo alikuja akaniacha mfyuuu zake. Changamoto humpa mtu akili aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mjasiriamali wa asili na kama ungejikita huko ungepata mafanikio makubwa kibiashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piga gereji za kutosha nimekuwa konda sana mpaka nikaweza endesha gari nilijifunza kupitia hapo hapo baadae nilifanikiwa kupata leseni nikaenda piga mishe za udereva haice bado ilikuwa changamoto japo nashukuru mubebe alikuwa akinisapoti sana

ye aliwahi kuajiriwa mapema japo sikutaka awe na wasiwasi na huzuni na Mimi maana alikuwa akijitoa sana pindi Niko final year ukicheki hana baba hana mama wote tulijuana orphanage ktk mkoa x mapenz yalianza toka tuko msingi daah kweli nilikuwa baharia mdogo .

mi koz yangu ilikuwa ya miaka minne ye mitatu alipomaliza akapata bahat ya ajira baada ya chuo nikaamua niende mkoa x kutafuta life hakupenda uamuzi wangu wala sikumuaga na nilikuwa simtajii nipo wapi dah nimepiga dayworker sana hapo nishamaliza chuo

Kupiga pasi ndefu kwangu ilikuwa kawaida nakunywa chai nzito na cha usiku nilikuwa nakula kiporo cha ugali nauchoma na chai na viazi vitamu vya kuchemsha hapo nimechimba kwenye shamba la watu

Kupiga rondo au kutembea kwa miguu usiseme mpaka kuota masagamba sikuwaga na nauli mpaka kobazi zikaisha ila nilikuwa navaa hivohivo kibishi

Nilikuwaga na suruali mbili na mashat matatu in short nilizoeleka na zile nguo kuna shati nlikuwa navaaga wananitania shati LA kijiji maana hilo hilo nilikuwa nikionekana nalo kwa sana ama kweli nilidharaulika

Nilipanga nyumba haina umeme in short haijamalizika vzur bomba pia LA maji halijavutwa ila kulikuwa na kisima kwahyo getho ni mwendo wa kibatali siku nyengine nala nje kwenye baraza la jiran kufata mwanga sometimes akiniona barazani anazima taa au napika maeneo ya nje ambao mwanga unafika nikikosa hela ya maftataa yaani kulala Giza ilikuwa kawaida

Nyumba yenyewe madirisha jamaa hajaweka wavu ameweka nondo ikabidi nizibe na safleti sasa hao mbu walinipiga doso kisawasawa plus baridi sina godoro nalalia hzo nguo zangu chache kuna siku sikuonekana nje siku nzima kumbe Niko ndani naumwa yalikuwa malaria ktk vitu nilivyojifunza Cheka na kila MTU tenda mazur kuwa mtiifu ata kama Fulani anakushambulia sababu kuna vijana na watu walikuwa wakinikubali walikuwa hawanioni wakapata wasiwasi wakachungulia ndani wakaniona ktk ile hali walinisaidia kunipeleka hospital

Mtaani kuzushiwa wizi na kina mama,Dada,baba majirani ambao Niko nao karibu kuitwa kwa mwenyekiti daah we acha tu na Yale manywele yangu yamekuwa makubwa hayana afya sina ela ya kunyoa ukicheki na nguo zimechanika utasema muhuni

Kwenda kusaidia wavuvi kuna kipindi ngalawa au chombo chetu kilipigwa na wimbi yaani tulijua tunakufa tukaanza kutoa maji na visada we acha tu .ukitoka hapo unapewa buku mbili na kisado cha uono

Maisha yalivyonizidi nikasepa nikadandia fuso yaani kweli nilikuwa mpuuz nadandia fuso litakaponipeleka ndo hapohapo na kifuko changu cha nguo (zile adidas za mgongoni) nilishawahi fika mpaka huko singida mpaka shinyanga nilikuwa nalala stendi asubuh kazi na kutafuta vibarua nakumbuka kuna mzee nilizoeana nae hapo shy mjini akanikaribisha kwake nikawa House boy

Daah hiyo mikazi ni balaa baadae akanipa baiskeli niwe bodaboda nimletee ela ( boda boda za baiskeli ) sjui kama sahiv zipo mkoa kama dar hamna na tanga zilikuwepogo nilikuwa shy twn

Ila kuufatilia magezeti kuuliza connection na wale niliosoma nao nilikuwa sichoki baadae nikasave save nikaanzisha genge lilinipa ela sana nikaeka na kibanda cha chipsi pemben pia nikamwambia mke wa yule mzee awe anatengeneza juice nimuuzie hapo tayar nishajichomoa kwake nilipata faida sana

Mungu hamptupi mja wake nikapata nafasi kwenye kampuni x INA deal na mambo ya agribusiness genge na mtaji nikamuachia mzee nikamwambia undugu kufaana sio kufanana nikapotea shy na nauli na faida tu hapo ndo nilijiwekaza sana kwenye Hio kampuni sikufanya makosa inaitwa fungulia mbwa nilikula mema ya nchi halafu siku narudi natoka shy nakutana na mpenz wangu namuhadithia alilia sana na alinilaumu sana kwa nn sikutaka msaada wake wakat huo na yeye alipiga hatua sana mi baharia nilikuwa napigika tu

Nb: kama ningejua yaan kama ningejua nisingekubali kuajiriwa pale kwenye ile kampuni bora ningepiga mishe zangu hapo hapo paliniletea maumivu kuliko kote ...the rest is history

Nowdays Niko good sina shida sina stress laifu linaenda

Sent using Jamii Forums mobile app

And yes kujibu swali la Uzi nishawahi kuwaza niwe jambazi nitumie silaha kama panga visu nk
Duh, pole sana mlevi huo msoto si kitoto aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua 2013 wakati nasubiri matokeo ya kidato cha nne kama sikosei ilikua mwezi january.Kutokana na ukata wa kukaa home mda mrefu huku nikikosa hata pesa za vocha na bi mother akiwa amepigika nikawa nina njaa iliokithiri(sio njaa ya kula njaa ya hela).

Jioni ya siku moja kabala ya tukio mshikaji wangu Dullah akaniambia amepata kazi ya ukarani kwenye ghala la korosho kesho yake anaanza,nikamwambia basi nami anifanyie mpango akasema sawa atajaribu.

Siku ya tukio niko zangu home asubuhi kama saa 7 na dk kadhaa.,Dullah akaja kuniita nikatoka nje nikakutana na huyo mama tukawa watatu mimi,mama na dula,mazungumzo yalikua hivi.
Mama: hujambo?
Mimi: sijambo shikamoo
Mama: dulla ameniambia na wewe unataka kazi ndo nikamtum aje kukuita,kama upo tayari tuongozane.
Mimi : ndio mama nipo tayari na kwakua nimeshanawa ngoja nivae tu simpo twende(mpaka hapa nikajua ukarani)

Njiani yule mama akatuuliza "hivi mmekunywa chai?" Sisi tukamjibu kwa pamoja "bado"...mara akasema "eeee msije mkaniangukia huko,tukifika nitawanunulia chai"..nikauliza "kwani mama ni kazi gani,si kuandika tu"? Sikujibiwa ,mara paap nitakuwa tumefika kiwanda(ghala) cha korosho pale mbagala kokoto.Kweli akatuagizia chai na chapati mbili mbili,wakati nakunywa chai nilikuatana na jamaa mmoja anaitwa robert(nilimzoea kwa jina la jirani) ikabidi aniulize vipi dogo mbona uko hapa ? Nikamjibu "nimekuja kufanya kazi bro humo kiwandani" akasema utaweza ndugu yangu kubeba gunia za korosho ? Nikamjibu mimi sibebi gunia tumeambiwa tutakua makarani.

Mara saa 2:30 ikafika tukawa tumeingia tukaambiwa tubadilishe nguo tukavaa za kazi(hapa kichwani niakanza kujawa na masawali) Yule jirani akasema haya dogo karibu jilehanam..aisee gunia(kiroba) la kwanza likaenda la pili likaishia kati wahindi wakaanza kupiga kelelenimemwaga korosho na kuchana kiroba. Ikabidi nihamishe kwenye kupakia korosho maana kubeba siwezi huko nako ilikua balaa gunia zilikua nyingi balaa halafu hakuna vitendea kazi hakuna mask wala gloves mikono ilichubuka.Yule Dullah mara akapokea simu(ya uongo) ghafla nikamuona anaanza kulia akaulizwa kulikoni akasema amefiwa na babu yake doh ikabidi aruhusiwe asepe nikawa nimebaki mimi na wengine.Mpaka kufika saa 6 mchana niko hoi tukahamishiwa kiwanda kingine kubeba gunia tupu ili ziletwe huku zipakiwe aisee ilikua balaa gunia zina vumbi nikaishiwa nguvu kwa kukisa hewa ikabidi nitolewe nje ya stoo...

Baada ya hapo tukarudishwa kiwanda kile cha mwanzo kwa ajili ya kuendelea kupakia mpaka kufika huo muda nikikohoa natoa kohozi jeusi nikipenga kamasi hivyo hivyo nikasema hapa hapa ngoja nitoroke..walinzi wakaniuliza unaenda wapi nikasema nimeagizwa mmoja akauliza mbona u ebeba na nguo zako sikuangalia nyuma nikawa nishafungua mlango nikaondoka.Kufika home kifua na mwili unaniuma nakohoa balaa nikamuona Dullah aliponiona alicheka sana akasema yeye hakufiwa ila aliona kazi imemshinda alitafuta kisingizio.Ilipofika saa 1 usiku akaja yule mama kuniulizia akasema mbona nimeondoka sijaaga na hela sikuchukua,nikamuuliza hiyo hela hapo unayo? Akasema hana kaicha nikaifuate kesho yake nikamjibu hapana nimesamehe...wiki nzima niliumwa kifua na mwili na tangu siku hiyo nikaapa sitakuja kufanya kazi kwa muhindi wale jamaa ni wauwaji kazi kubwa vifaa hakuna au duni.

Ndefu samahani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii nimecheka hadi machozi yametiririka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jamaa huwa una visa vya kusisimua sana.ile story ya kung'atwa sikio na lile jitu huwa inanisimua
acha tu ndugu ni vijana wadogo tu lakini tumepitia mambo mazito mno,kusafirisha mercury nje ya nchi kuna taratibu zake ile mercury ilikuwa ni mercury halisi sema waliimix na vitu vyao ikaonekana ya rang nyekundu ndo hapo tukaingizwa chaka but ilikuwa nyekundu,kuhusu ni jinsi gani ilipita mpakani dah mungu mwenyewe ndo anajua,so wakati wa kurudi nilikuwa nategemea nlowaacha wakati napita ndo ntakutana nao na pia wakati wa kurudi kuna sheria za kupitisha madini mpaka + sikuwa na kibali hata kimoja kwaiyo ilikuwa ni mawili nipange gari niingie kituoni then mahakamani nipigwe nyundo au nijiongeze nlicho nacho kinisave,nilichonusurika ni kwamba hela zilikuwa kwenye mfuko wa chupi,nmeshndwa kuweka picha sababu kuna watu wengi huwa wanaweza unganisha doti nkaawaribia watu vibarua vyao but yote kwa yote tunaendelea kupambana,sema nilichokigundua nchi ya congo kuna biashara nyingi sana zinazoweza kukufanya mtu ukawa tajiri ndani ya mwezi sema kifo ndo nje nje,maana nakumbuka nilishawahi kuibiwaga iphone 4s dah yani aliyekuja kuniibia kanijia kabisa na smg kidogo nimwambie twende ukachukue na chaji nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha yalinipiga, sina pesa ya kula, wala ya vocha.

Nikaenda kwa wale jamaa wanakupa vitu ukawauzie(nilikuwa sijui kama kazi ndio hiyo). After kupigwa msasa na seminar za hapa na pale, tukapewa vitu tukauze (taa mbili za solar, taa unatikiwa kupeleka 10k kwa kila taa na sabuni @1k.

Nikaanza kutembeza maeneo ya town(Mwanza). Kufika saa tano nikaambulia kuuza sabuni moja 1k(ambayo ni pesa ya ofisi).
Hapo sina pesa ya kula wala ya nauli.

Nikapata wazo, la kwenda nje ya mji kidogo(igombe) nikatumia pesa ya office (1k)kama nauli. Nikijua huko nitapata watu wakuwapiga, niwauzie kwa bei ya juu.

Kufika igombe ndio nikajua kijijini kuna watu wagumu kutoa pesa. Kuliko mjini
Nilizunguka hadi saa tisa, nikawa nimeuza taa kwa 10k(loss), pamoja na sabuni kazaa kwa faida kama ya 1k.
Hii pesa ya 1k , ndio nililipa ile niliyotumia kama nauli.

Nikaona nimefail tayari, sijapata hata pesa ya kwenda nayo geto.
Na bado niko Igombe narudije?

Mida kama ya saa 10, Nikachukua ile 10k ya office nikarudi town. Kufika sehemu moja inaitwa Pasiansi nikashuka . ili nijaribu bahati yangu.

Nikatembeza nikauza sabuni tena, nikapata faida ya 500/=.
Mara nikakutana na Mama hivi, anahitaji but ana wasiwasi taa inaweza kuwa mbovu. Nikamshawishi akakubali kwa 15k(faida 5k).
Wakati tunatest kama inapeleka charge, ikawa imegoma. Na ilikuwa imebaki moja.

Ikabidi nirudi ofisini kubadilisha.
Ofisi ziko mitaa ya Ghana(jijini Mwanza). Kutoka Pasiansi-Ghana-Pasiansi, nikatumia 800/=.
Nikamuuzia taa yule Mama akanipa 15k. Nikampa na namba yangu, incase kukiwa na tatizo.
Nikatembea hadi ofisini, nikakabizi sabuni, zilizobaki pamoja na hela ya mauzo Nakumbuka nilibakiwa na buku 4.

Nikajongea maeneo ya Rock city mall. Nikachukua mishikaki ya 300/=@100 na juice ya 200/=. Nikaanza kurudi zangu gheto kwa Miguu.

Mara yule Mama niliyemuuzia taa akaanza kunipigia simu akilalamika taa ina Mwanga mkali , kama vipi nirudishe elfu 15 yake. Nikamuelekeza jinsi ya kupunguza Mwanga but still akawa analalamika(aliendelea kulalamika hadi siku alipokubali kapoteza 15k, lakini wakati wote nilikuwa nampa ushirikiano) .

Toka hapo nikaazimia sitorudi tena kwenye ile kazi.

Yaani unazunguka kama chizi, hulipwi mshahara ila commission. Na bado unaambulia lawama za wateja(kitu ambacho siwezi kuvumilia mtu akiwa analalamika kwa sababu yangu).

Nakumbuka nilirudi gheto na buku tatu nikaendelea na maisha.

Kuipata hii kazi nilitumia kama 15k(nilikopa, nikijua kuna mshahara wa 350k per Month).
But niliishia kuambulia 3500/= kwa hiyo siku. Kwa sababu sikurudi tena, itoshe kusema nilipata hasara.

Hii ndiyo mojawapo ya kazi nilifanya nikiwa nimepigika.

Lakini ilinifundisha kitu kikubwa

Mimi ni mtu mwnye aibu kiasi fulani. But nimepata uwezo wa kumface mtu na kumshawishi, kununua bidhaa ninayouza. Sujui ndio mnaita Confidence.

Kwasasa nikikumbuka najivunia nilichojifunza but siwezi kurudi kutembeza bidhaa zile labda maisha yanipige tena.

Sent using simu mbovu
Hii kazi ni ngumu na inataka kipaji na uvumilivu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hii post mkuu unaonekana upo real, post nyingine huwa masikhara mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha bwana unawexa kusema ww unahaghaika kumbe kuna wenzako wana ck mbili hawajaona kitu kinaitwa chakula ....,Mungu uguse watu wako ...wakati kuna wengine hawajui kitu kinaitwa shidah .....

Umenikumbusha mbali uwono ,nilikuwa nauoenda nikipata na mbilimbi mashalah ugali unashuka haswaa

Sent using i phone x
 
Piga gereji za kutosha nimekuwa konda sana mpaka nikaweza endesha gari nilijifunza kupitia hapo hapo baadae nilifanikiwa kupata leseni nikaenda piga mishe za udereva haice bado ilikuwa changamoto japo nashukuru mubebe alikuwa akinisapoti sana

ye aliwahi kuajiriwa mapema japo sikutaka awe na wasiwasi na huzuni na Mimi maana alikuwa akijitoa sana pindi Niko final year ukicheki hana baba hana mama wote tulijuana orphanage ktk mkoa x mapenz yalianza toka tuko msingi daah kweli nilikuwa baharia mdogo .

mi koz yangu ilikuwa ya miaka minne ye mitatu alipomaliza akapata bahat ya ajira baada ya chuo nikaamua niende mkoa x kutafuta life hakupenda uamuzi wangu wala sikumuaga na nilikuwa simtajii nipo wapi dah nimepiga dayworker sana hapo nishamaliza chuo

Kupiga pasi ndefu kwangu ilikuwa kawaida nakunywa chai nzito na cha usiku nilikuwa nakula kiporo cha ugali nauchoma na chai na viazi vitamu vya kuchemsha hapo nimechimba kwenye shamba la watu

Kupiga rondo au kutembea kwa miguu usiseme mpaka kuota masagamba sikuwaga na nauli mpaka kobazi zikaisha ila nilikuwa navaa hivohivo kibishi

Nilikuwaga na suruali mbili na mashat matatu in short nilizoeleka na zile nguo kuna shati nlikuwa navaaga wananitania shati LA kijiji maana hilo hilo nilikuwa nikionekana nalo kwa sana ama kweli nilidharaulika

Nilipanga nyumba haina umeme in short haijamalizika vzur bomba pia LA maji halijavutwa ila kulikuwa na kisima kwahyo getho ni mwendo wa kibatali siku nyengine nala nje kwenye baraza la jiran kufata mwanga sometimes akiniona barazani anazima taa au napika maeneo ya nje ambao mwanga unafika nikikosa hela ya maftataa yaani kulala Giza ilikuwa kawaida

Nyumba yenyewe madirisha jamaa hajaweka wavu ameweka nondo ikabidi nizibe na safleti sasa hao mbu walinipiga doso kisawasawa plus baridi sina godoro nalalia hzo nguo zangu chache kuna siku sikuonekana nje siku nzima kumbe Niko ndani naumwa yalikuwa malaria ktk vitu nilivyojifunza Cheka na kila MTU tenda mazur kuwa mtiifu ata kama Fulani anakushambulia sababu kuna vijana na watu walikuwa wakinikubali walikuwa hawanioni wakapata wasiwasi wakachungulia ndani wakaniona ktk ile hali walinisaidia kunipeleka hospital

Mtaani kuzushiwa wizi na kina mama,Dada,baba majirani ambao Niko nao karibu kuitwa kwa mwenyekiti daah we acha tu na Yale manywele yangu yamekuwa makubwa hayana afya sina ela ya kunyoa ukicheki na nguo zimechanika utasema muhuni

Kwenda kusaidia wavuvi kuna kipindi ngalawa au chombo chetu kilipigwa na wimbi yaani tulijua tunakufa tukaanza kutoa maji na visada we acha tu .ukitoka hapo unapewa buku mbili na kisado cha uono

Maisha yalivyonizidi nikasepa nikadandia fuso yaani kweli nilikuwa mpuuz nadandia fuso litakaponipeleka ndo hapohapo na kifuko changu cha nguo (zile adidas za mgongoni) nilishawahi fika mpaka huko singida mpaka shinyanga nilikuwa nalala stendi asubuh kazi na kutafuta vibarua nakumbuka kuna mzee nilizoeana nae hapo shy mjini akanikaribisha kwake nikawa House boy

Daah hiyo mikazi ni balaa baadae akanipa baiskeli niwe bodaboda nimletee ela ( boda boda za baiskeli ) sjui kama sahiv zipo mkoa kama dar hamna na tanga zilikuwepogo nilikuwa shy twn

Ila kuufatilia magezeti kuuliza connection na wale niliosoma nao nilikuwa sichoki baadae nikasave save nikaanzisha genge lilinipa ela sana nikaeka na kibanda cha chipsi pemben pia nikamwambia mke wa yule mzee awe anatengeneza juice nimuuzie hapo tayar nishajichomoa kwake nilipata faida sana

Mungu hamptupi mja wake nikapata nafasi kwenye kampuni x INA deal na mambo ya agribusiness genge na mtaji nikamuachia mzee nikamwambia undugu kufaana sio kufanana nikapotea shy na nauli na faida tu hapo ndo nilijiwekaza sana kwenye Hio kampuni sikufanya makosa inaitwa fungulia mbwa nilikula mema ya nchi halafu siku narudi natoka shy nakutana na mpenz wangu namuhadithia alilia sana na alinilaumu sana kwa nn sikutaka msaada wake wakat huo na yeye alipiga hatua sana mi baharia nilikuwa napigika tu

Nb: kama ningejua yaan kama ningejua nisingekubali kuajiriwa pale kwenye ile kampuni bora ningepiga mishe zangu hapo hapo paliniletea maumivu kuliko kote ...the rest is history

Nowdays Niko good sina shida sina stress laifu linaenda

Sent using Jamii Forums mobile app

And yes kujibu swali la Uzi nishawahi kuwaza niwe jambazi nitumie silaha kama panga visu nk
Huyo mpenzi wako bado upo nae?
au mliachana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom