Wakati umepigika kazi gani ya ajabu uliwaza kufanya?

Hakuna kazi niliyokuwa naichukia na siipendi mpaka kesho japo wanaoifanya nawapenda na nawaheshimu saana! Sitaitaja kiuwazi ila kimaudhui wenye ufahamu wataelewa! Nilikuwa graduate fani tofauti na hiyo lakini nikajikuta natembea na bahasha kuomba toka ofisi moja hadi nyingine mwisho wa siku nikapata kuwapa maharifa form1. I seee! Nilivyokuwa nimepigika na nimekonda nilishukuru saana kupata japo hiyokazi na ulikuwa ndo mlango wa kupambana nikapata kamtaji nikaacha hiyo kazi na kuanza biashara iliyoniwezesha kutoboa kiasi fulani namshukuru Mungu!
Hahah mkuu kwanini hupendi kazi ya ualimu?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Ambao bado tupo kwenye stage ya kupigika nadhani tunaruhusiwa hapa!

Ni mwaka 2017 tu hapo mzee katimuliwa kazi hapo ndipo kila kitu kilipoharibika na nipo chuo,hapo niliuza hadi viatu na nguo mradi tu kitabu kiemde.

Hapo deni la ada linasoma 2.3mil...nikauza kila kitu cha thamani deni likasoma 1.1mil..na mwaka wa kuhitimu 2018 march huu hapa!!...na hii ni mwezi February!!!

Sijakaa vizuri barua hii hapa tayari nishatupwa nje ya chuo aisew wiki 2 kabla ya final..nilipambana mno bila mafanikio ikabidi tu nirudi chuoni na kuwapigia magoti hadi wakaniruhusu kuattend final kwa sharti la kushikilia vyeti hadi niwalipe chao...

Kuingia kitaa pagumu mno pagumu kwelikweli...kuna muda mtu mnakaa hata two days no chakula..msoto zikawa sio pasi ndefu tena bali crosi kabisa!

Nikaanza na kubangua korosho kiwanda fulani hivi...ndoo ndogo hii ukishabangua ukaijaza bado wanachambua zile zilizojeruhiwa hata kuparuzwa tu hazihesabiwi unakuta umejaza ndoo ndogo ila znazopimwa ni nusu ndoo tu....mbaya zaidi ukute unajaza ndoo mpja na nusu kwa wiki hivyo mwisho wa wiki unakuta una 6000 taha on hand..hapo inakulazimu tu kuchapa mguu huwezi toa nauli kwenye 6000 tshs issue ya kula ni pasi ndefuuuu...


Ilikuja kunishinda baada ya kuwa natapika kila nikivuta hewa na fukuto la mafuta ya korosho hivyo nikafurushwa..hapa nikaanza kusomba mchanga na kuuza kwa tshs 200 kwa kiroba,kubeba tofali,saidia fundi...muda kidogo nakuta mwili unazidi kuwa dhaifu hivyo nikastop vibarua vya kutumia nguvu.


Kwa vile fieled yangu ni mwalimu nikaanza kufundisha tuition pale home kila kichwa ni tshs 200 kwa siku na nilibahatika kuwa na vichwa 12...kazi ikafanyika na maisha ilibidi yaendelee tu.

Hivi karibuni kuna mmama kanipa kibarua cha houseboy...natamani iwe stori tu lakini kumbe ndio nipo katikati ya stori!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuza ubuyu chuo. Wateja dharau mingi sana. Wanakopa kulipa deni mpaka ugomvi.

Nachukua ubuyu kwa babu issa packet moja 1000, naagiza packet 100 hiyo inakua tsh 100,000/=. Plus cost ya kusafirishia 20,000/=. Nikiuza mmoja 2000/= hapo faida napata kama 80,000/= it's alot faida nzuri. Sema nlikua nauza packet moja Hadi 4 kwa siku. Biashara ilikua slow lakini nikawa sikosi pesa ya kula kila siku

Changamoto niliokutana nayo kwenye hiyo biashara kuna mama mmoja nae alikua mwanachuo, mzanzibari yeye akamwambia mume wake amnunulie ubuyu nae awe ana uza. Akaja na mbwembwe eti anauza mmoja 1500/= mimi nikienda na wangu wa 2000/= wateja wanaleta dharau mbona flani anauza bei ya chini. Nikarudi zangu maskani nikakaa kuwaza sasa next step. Pesa naitaka lakini bei sitaki kushusha. Baada ya kuwaza na kuwazua nikaona sio mbaya nikaenda supermarket nikanunua vile vikopo vina mfuniko nikaja kufanya packaging, kwenye ile packet ya 2000/= mimi nikawa natoa vikopo vitatu, kila kopo nauza buku. So nikawa napata 3000/= nikamuacha yule shoct anauza 1500/= . Biashara ni akili asiee

Nilijaribu hadi kujifunza kupika kashata, nikanunua raw material zote , nikazama utube kucheki jinsi ya kupika kashata. Aisee hii ilinishinda kashata zilikua zinatoka ngumu kama mawe. Nikaachana nazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera sana mkuu napenda sana watu kama wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipitia kipindi kigumu sana hadi nguo ziliisha na ilibidi hata wakati wa kukaa Navizia maana ikipasuka tu, kiraka kitanihusu na pesa ya kiraka sina, muda huo huo suruali zilikuwa 2 na hapo ni graduate. Asiwaambie mtu wanajf, nilikuwa naamka ucku nawaza na ndugu pamoja na rafiki walinikacha kisa mkwanja. Niliwaza kufungua biashara ndogo ya kuuza half cakes kupitia vijana wanaotembeza maana naishi mjini. Nikande ngano na vijana wangu na waende kuuza na kuwalipa kitakachopatikana. Ila nilishindwa maana sikuwa na pesa na pia sina nyumba kwani nakaa kwa mama, na mama ananidharau na watoto wake. Ghafla nikapigiwa simu na rafiki yangu wa zamani sana kuwa nikafanye interview katika kampuni moja katika huo mji niliokuwa naishi, nikaenda na nilikuwa peke yangu, nikapigiwa simu kuanza kazi.
Unaambiwa ilikuwa saa 11 jioni mdada aliniambia..... nanukuu " When you expect to start your new job" Nilimjibu hata sasa hivi, mdada alicheka sana kwani ilikuwa jumamosi ila aliniambia tulia Mr. Baadae akaniambia utaanza jumanne ijayo na nimetuma offer kwa email yako, isaini na baada ya hapo uanze kazi. Sasa nashukuru nguo nimenunua, simu ninayo, dharau zimeisha home, nashukuru heshima imerudi.
Funzo: Usimdharau aliyesoma hasa mwenye elimu kuanzia degree 1, pia nikagundua kuwa nguo zikichakaa huwa zinawahi kuchafuka na zinachelewa kutakata unapozifua.
Tusomeshe watoto, huu ndio urithi pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ya kudharauliwa ilinikuta baada ya kumaliza mwaka na ushee bila kazi toka nimalize chuo. Usiombe yakukute,ni machungu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom