Wakati umefika Serikali iruhusu Ndoa za Mkataba, hizi zilizopo ni msalaba kwa kizazi hiki

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
WAKATI UMEFIKA SERIKALI IRUHUSU NDOA ZA MKATABA, ZILIZOPO NI MSALABA KWA KIZAZI HIKI.

Anaandika Robert Heriel
Yule Shahidi, kutoka Nyota ya Tibeli.

Hatuwezi kujidanganya tena, ndoa zilizopo ni mzigo na msalaba mzito Kwa kizazi hiki hasa Kwa watoto wakiume.

Waliopo kwenye ndoa wengi wenu mtanielewa, na vijana wachache mnaotaka kujiingiza ndoani pia mtanielewa, na Wale mnaoishi kiunyumba najua mtaelewa Taikon anazungumzia Jambo gani.

Ndoa ilikuwa muhimu Zama za kale, umuhimu wake uliletwa na Sababu kuu mbili,
1. Uzazi
2. Ushirika

Lakini zama za sasa mambo mengi yamebadilika,
Uzazi mtu anaweza kupata bila ya ndoa, halikadhalika na ushirika anauwezo WA kuupata vyema Kabisa pasipo ya ndoa.

Kwa Usalama wa kijana mwenye maono ya mbali, ndoa kwake haiwezi kuwa chaguo muhimu, ndoa huweza kumpotezea Focus kutokana na nature ya Karne hii tuliyonayo.

Nashauri ndoa iwe ya Mkataba, iwe ya miaka miwili au mitatu, au mwaka vyovyote Ila Watu wasilazimishwe kuishi maisha Yao yote. Huo utakuwa ni Msalaba.

Nasema hivyo Kwa sababu, ndoa haiendani na falsafa ya HAKI SAWA, ndoa za haki Sawa ni Msalaba mzito hujawahi ona. Kuoa haiwezi kuwa furaha kamwe Kwa Sera za haki Sawa. Ninauhakika na nikisemacho,
Furaha itakuwa Mwanzoni, lakini baadaye mambo hugeuka hasa Kwa mwanaume.

Sheria za kizamani ziondolewe Kama Ile inayosema "Mwanaume ndiye atakuwa na wajibu wa kumhudumia na kumtunza mke" lakini sheria hiyohiyo haizungumzii vipi Kama Mwanamke anafanya kazi,
Sheria hii ni yakizamani Kwa sababu zamani wanawake wengi walibaguliwa kwenye Ajira, lakini sasa Wanawake wanaajiriwa Kama ilivyo Kwa wanaume.

Dunia ya sasa ilivyo, Inatakiwa ndoa itaje kabisa kwa nini watu wanaoana, kama ni kuzaa watoto iandikwe kuzaa watoto, utaje watoto wangapi, cheti cha ndoa jieleze hayo yote, na mkataba wa muda gani.

Lakini kujidanganya hapa utaishi na mtu huyohuyo miaka yote ni uongo wa mchana, hasa Kwa Karne hii.

Serikali itoe Demokrasia katika hili, sio kulazimishana hapa, ndoa za mkataba ni nzuri Kwa kizazi hiki,
Mkiona mnaendana mna-renew mkataba Kwa miaka mitaji tena.
Ishu za Mali ziwe separate na mambo ya kindoa kuondoa migogoro isiyo ya lazima, Kama wanandoa wataamua kuwa na umiliki WA pamoja WA Mali hiyo iitwe biashara na itamkwe wazi mwenye share zaidi atalipwa kulingana na share zake.

Kama ndio mnataka kitu kinachoitwa haki Sawa kifanyike basi hiyo ndio Haki yenyewe.

Kila mtu apewe majukumu yake,
Mfano; Baba, kutoa pesa ya chakula, kulipa bill ya umeme, kulipa Ada ya watoto.

Mama; Kununua nguo za watoto, kulipia Bill ya maji, kuwanunulia watoto mahitaji.

Kuhusu ujenzi wa makazi, kila mtu atoe na iwekwe kumbukumbu ya kiasi kilichotolewa, kila mmoja alipwe haki sawa, Kama alivyochangia, ili siku mkataba ukiisha au mmoja akivunja mkataba vitu vigawanwe Sawasawa na mtu alivyochangia.
Kama Mwanaume alitoa Asilimia 40% atalipwa hizohizo, na Kama Mwanamke alitoa 60% alipwe hizohizo.
Hiyo ndio haki.

MAJUKUMU YA NYUMBANI
Majukumu kama Kufua, Kupika, Kuosha vyombo, na kazi zingine, mkataba ueleze wazi nani atafanya nini au watapokezana,
Maana kuna watu wanasingizia oooh! Nilikuwa napika, sijui namfanyia kazi za ndani hivyo nami na Mchango, ni kweli huo ni Mchango, sasa mupangiane zamu, au mtaamua muajiri Msaidizi wa kazi za ndani ambaye mtapokezana kumlipa, mwezi huu atalipa mume, mwezi unaofuata Mke, vivyo hivyo. Ili haki Sawa itendeke.

Haki Sawa mara nyingi haiangalii Furaha wala STAREHE, ukisema haki ziwe Sawa unavunja Wajibu na majukumu ya watu au viumbe, yaani kila mtu anakuwa Sawa na mwenzake. Iwe kimajukumu au kihaki.

KUWALEA WAZAZI
Mkataba uweke wazi kuwa kila mtu atalea mzazi wake mwenyewe, mwanandoa mmoja hatahesabika kuwa anaowajibu WA kutunza wazazi wa pili labda Kwa mapenzi na hiyari yake.

Mwanaume alee wazazi wake, mwanamke alee wazazi wake MWENYEWE. Na Kama itakuwa makubaliano ya kushirikiana Kulea wazazi Kwa pamoja basi mkataba useme wazi.

KULEA WATOTO
Mkataba ueleze kuwa mwenye jukumu la Kulea mtoto ni wazazi wote Kwa Asilimia 50% Kwa 50%. Hata baada ya Mkataba Kuisha.
Mtoto niwa wote, ni wababa na niwamama.

MTOTO ATAISHI WAPI?
Mkataba ueleze kuwa baada ya kuachana mtoto ataishi na Mama au Baba, mamlaka zitaangalia Nani anauwezo WA kumlea mtoto.
Mtoto pia akifikisha umri wa kuanzia miaka 10 apewe haki ya kuchagua upande wa kuishi.

MAJINA YA MTOTO
Mtoto atapewa majina kulingana na atakayetoa matunzo zaidi.
Haki Sawa ni mpaka kwenye Majina na Ubin wa watoto.
Hata Wanawake wapo wenye vigezo vya watoto kuchukua Ubin WA ukoo wa mama.

Hapa wanaume watajifunza kuchagua wanawake WA hadhi zao, sio mwanaume hadhi yako ya chini alafu unajitia ujuaji kuoa mwanamke WA hadhi ya juu, kwenye Hali Sawa hapo itakunyoosha, maana mwanamke atakuambia naye anahaki ya watoto kuitwa majina ya ukoo wake, na hautakuwa na uwezo wa kulizuia Hilo.

Hali sawa itaepusha wanawake wenye tamaa, kwani wataolewa na wanaume wa hadhi Yao. Ndipo Ile dhana ya kumpata wa kufanana naye itatawala.

Unakuta mwanamke ni fukara, familia yake fukara, alafu anataka kuolewa na Mwanaume Tajiri na kwenye familia Tajiri, baadaye bila haya na aibu linataka kugawana Mali na mumewe baada ya kuachana, huo ni upumbavu na wengi hujikuta matatizoni. Haiwezekani uje mikono mitupu na nguo zako zilizopauka alafu uondoke na jumba na magari, hiyo haiwezekan kabisa labda Kwa familia zisizojielewa.

Olewa na OA Saizi yako, mnayeendana, ili haki Sawa itende kazi;

Au unakuta mwanaume masikini Kabisa ameoa mwanamke mwenye uwezo alafu mwisho WA siku anataka wagawane Mali. Thubutu! Yaani uje na kaptura yako kauka nikuvae upambane na Mali za Mkeo, huo ni uzumbukuku!

Haki Sawa haiwezekan Kwa watu wasiofanana. Ili iwezekane basi ndoa za mkataba ni muhimu.
Serikali naiomba ianzishe ndoa za mkataba ili kusaidia Vijana na mabinti ambao wanapata tabu kwenye hizi ndoa za siku hizi ambazo zinafuata mifumo ya kizamani kwenye dunia iliyojaa tamaa, ubinafsi, uchu wa utawala.

Haki Sawa inavunja thamani ya mwanamke, mwanamke mwenye akili timamu hawezi kuikimbilia haki Sawa.
Kwani atakosa uthamani wake kama Mwanamke.
Ile dhana ya kuhudumiwa, kutunzwa na kupendwa kwenye Haki Sawa haipo.
Kwani hivyo navyo itampasa mwanamke amfanyie mumewe (mwanaume) Jambo ambalo wanawake wengi kiasili hawataki kulisikia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Pili....mali zote ninazopata (maana mm ndo mtaftaji yeye ni mkaa nyumbani)....nyumba,viwanja,gari na account bank vina majina ya mamaangu ili kama kuna shida yeyote itatokea mbeleni, mamaangu aliyenilea mimi anaweza fanya hivyo kwa familia yangu haijalishi ya mke yupi na mtoto yupi......Mwisho tuishi nao kwa akili
 
Ndoa za mkataba sio suluhu ya matatizo ambayo umeyaorodhesha,bali ndoa za mkatabazinazidisha matatizo hasa kwa wanawake.

Ni bora tuboreshe ndoa hizi hizi tulizokuwa nazo
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Hata ukioa mfanyakazi hataki kuweka Hela ya kupeleka kwenye maendeleo Bora na mwanaume ukatulia sababu ikifika wakati wa kugawana haitaangalia kuwa huyu hakutoa kitu inapigwa pasu kwa pasu

Sent from my Nokia 5.3 using JamiiForums mobile app
Utajilemaza na kuwa masikini bure kwa kuhofia kugawana na mkeo
........komesha ni hii kila mradi mkubwa unaouanzisha hakikisha jina la mmiliki halali ni mamaako maana baba zetu nao duuuh....
 
  • Kicheko
Reactions: _ID
Ndoa za mkataba sio suluhu ya matatizo ambayo umeyaorodhesha,bali ndoa za mkatabazinazidisha matatizo hasa kwa wanawake.

Ni bora tuboreshe ndoa hizi hizi tulizokuwa nazo
Hapana hazizidishi matatizo ila zinawapatia uhuru na haki pale yanaposhindikana......ndugu yangu vijana wanaogopa kuanzisha familia, waliofanikiwa kuingia ndani ya ndoa wanatafuta pakutokea maana wanayoyakuta ni tofauti...
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mkiambiwa Uislam ulishaliona hili ukaweka sheria kitambo mnaona mafala. We unaweza kuishi na mtu maisha yako yote wakati hamna tena upendo kati yenu?
 
Hapana hazizidishi matatizo ila zinawapatia uhuru na haki pale yanaposhindikana......ndugu yangu vijana wanaogopa kuanzisha familia, waliofanikiwa kuingia ndani ya ndoa wanatafuta pakutokea maana wanayoyakuta ni tofauti...
Talaka si zipo watu wakishindwana wanaachana au ?
 
watu wanataka vitu vya kipuuzi puuzi

weka uzi wa namna ya kusoma sms za mpenzi wako bila ya yeye kujua halafu weka uzi wa namna ya kutengeneza sabauni za kufulia nyumbani kwa gharama nafuu uone uzi upi utasomwa said.

mie mwenyewe na uzee wangu ntaanza na wa kusoma sms za mpenzi wako bila ya mwenyewe kujua
Huu uzi mbona watu hawausomi
 
WAKATI UMEFIKA SERIKALI IRUHUSU NDOA ZA MKATABA, ZILIZOPO NI MSALABA KWA KIZAZI HIKI.

Anaandika Robert Heriel
Yule Shahidi, kutoka Nyota ya Tibeli.

Hatuwezi kujidanganya tena, ndoa zilizopo ni mzigo na msalaba mzito Kwa kizazi hiki hasa Kwa watoto wakiume.

Waliopo kwenye ndoa wengi wenu mtanielewa, na vijana wachache mnaotaka kujiingiza ndoani pia mtanielewa, na Wale mnaoishi kiunyumba najua mtaelewa Taikon anazungumzia Jambo gani.

Ndoa ilikuwa muhimu Zama za kale, umuhimu wake uliletwa na Sababu kuu mbili,
1. Uzazi
2. Ushirika

Lakini zama za sasa mambo mengi yamebadilika,
Uzazi mtu anaweza kupata bila ya ndoa, halikadhalika na ushirika anauwezo WA kuupata vyema Kabisa pasipo ya ndoa.

Kwa Usalama wa kijana mwenye maono ya mbali, ndoa kwake haiwezi kuwa chaguo muhimu, ndoa huweza kumpotezea Focus kutokana na nature ya Karne hii tuliyonayo.

Nashauri ndoa iwe ya Mkataba, iwe ya miaka miwili au mitatu, au mwaka vyovyote Ila Watu wasilazimishwe kuishi maisha Yao yote. Huo utakuwa ni Msalaba.

Nasema hivyo Kwa sababu, ndoa haiendani na falsafa ya HAKI SAWA, ndoa za haki Sawa ni Msalaba mzito hujawahi ona. Kuoa haiwezi kuwa furaha kamwe Kwa Sera za haki Sawa. Ninauhakika na nikisemacho,
Furaha itakuwa Mwanzoni, lakini baadaye mambo hugeuka hasa Kwa mwanaume.

Sheria za kizamani ziondolewe Kama Ile inayosema "Mwanaume ndiye atakuwa na wajibu wa kumhudumia na kumtunza mke" lakini sheria hiyohiyo haizungumzii vipi Kama Mwanamke anafanya kazi,
Sheria hii ni yakizamani Kwa sababu zamani wanawake wengi walibaguliwa kwenye Ajira, lakini sasa Wanawake wanaajiriwa Kama ilivyo Kwa wanaume.

Dunia ya sasa ilivyo, Inatakiwa ndoa itaje kabisa kwa nini watu wanaoana, kama ni kuzaa watoto iandikwe kuzaa watoto, utaje watoto wangapi, cheti cha ndoa jieleze hayo yote, na mkataba wa muda gani.

Lakini kujidanganya hapa utaishi na mtu huyohuyo miaka yote ni uongo wa mchana, hasa Kwa Karne hii.

Serikali itoe Demokrasia katika hili, sio kulazimishana hapa, ndoa za mkataba ni nzuri Kwa kizazi hiki,
Mkiona mnaendana mna-renew mkataba Kwa miaka mitaji tena.
Ishu za Mali ziwe separate na mambo ya kindoa kuondoa migogoro isiyo ya lazima, Kama wanandoa wataamua kuwa na umiliki WA pamoja WA Mali hiyo iitwe biashara na itamkwe wazi mwenye share zaidi atalipwa kulingana na share zake.

Kama ndio mnataka kitu kinachoitwa haki Sawa kifanyike basi hiyo ndio Haki yenyewe.

Kila mtu apewe majukumu yake,
Mfano; Baba, kutoa pesa ya chakula, kulipa bill ya umeme, kulipa Ada ya watoto.

Mama; Kununua nguo za watoto, kulipia Bill ya maji, kuwanunulia watoto mahitaji.

Kuhusu ujenzi wa makazi, kila mtu atoe na iwekwe kumbukumbu ya kiasi kilichotolewa, kila mmoja alipwe haki sawa, Kama alivyochangia, ili siku mkataba ukiisha au mmoja akivunja mkataba vitu vigawanwe Sawasawa na mtu alivyochangia.
Kama Mwanaume alitoa Asilimia 40% atalipwa hizohizo, na Kama Mwanamke alitoa 60% alipwe hizohizo.
Hiyo ndio haki.

MAJUKUMU YA NYUMBANI
Majukumu kama Kufua, Kupika, Kuosha vyombo, na kazi zingine, mkataba ueleze wazi nani atafanya nini au watapokezana,
Maana kuna watu wanasingizia oooh! Nilikuwa napika, sijui namfanyia kazi za ndani hivyo nami na Mchango, ni kweli huo ni Mchango, sasa mupangiane zamu, au mtaamua muajiri Msaidizi wa kazi za ndani ambaye mtapokezana kumlipa, mwezi huu atalipa mume, mwezi unaofuata Mke, vivyo hivyo. Ili haki Sawa itendeke.

Haki Sawa mara nyingi haiangalii Furaha wala STAREHE, ukisema haki ziwe Sawa unavunja Wajibu na majukumu ya watu au viumbe, yaani kila mtu anakuwa Sawa na mwenzake. Iwe kimajukumu au kihaki.

KUWALEA WAZAZI
Mkataba uweke wazi kuwa kila mtu atalea mzazi wake mwenyewe, mwanandoa mmoja hatahesabika kuwa anaowajibu WA kutunza wazazi wa pili labda Kwa mapenzi na hiyari yake.

Mwanaume alee wazazi wake, mwanamke alee wazazi wake MWENYEWE. Na Kama itakuwa makubaliano ya kushirikiana Kulea wazazi Kwa pamoja basi mkataba useme wazi.

KULEA WATOTO
Mkataba ueleze kuwa mwenye jukumu la Kulea mtoto ni wazazi wote Kwa Asilimia 50% Kwa 50%. Hata baada ya Mkataba Kuisha.
Mtoto niwa wote, ni wababa na niwamama.

MTOTO ATAISHI WAPI?
Mkataba ueleze kuwa baada ya kuachana mtoto ataishi na Mama au Baba, mamlaka zitaangalia Nani anauwezo WA kumlea mtoto.
Mtoto pia akifikisha umri wa kuanzia miaka 10 apewe haki ya kuchagua upande wa kuishi.

MAJINA YA MTOTO
Mtoto atapewa majina kulingana na atakayetoa matunzo zaidi.
Haki Sawa ni mpaka kwenye Majina na Ubin wa watoto.
Hata Wanawake wapo wenye vigezo vya watoto kuchukua Ubin WA ukoo wa mama.

Hapa wanaume watajifunza kuchagua wanawake WA hadhi zao, sio mwanaume hadhi yako ya chini alafu unajitia ujuaji kuoa mwanamke WA hadhi ya juu, kwenye Hali Sawa hapo itakunyoosha, maana mwanamke atakuambia naye anahaki ya watoto kuitwa majina ya ukoo wake, na hautakuwa na uwezo wa kulizuia Hilo.

Hali sawa itaepusha wanawake wenye tamaa, kwani wataolewa na wanaume wa hadhi Yao. Ndipo Ile dhana ya kumpata wa kufanana naye itatawala.

Unakuta mwanamke ni fukara, familia yake fukara, alafu anataka kuolewa na Mwanaume Tajiri na kwenye familia Tajiri, baadaye bila haya na aibu linataka kugawana Mali na mumewe baada ya kuachana, huo ni upumbavu na wengi hujikuta matatizoni. Haiwezekani uje mikono mitupu na nguo zako zilizopauka alafu uondoke na jumba na magari, hiyo haiwezekan kabisa labda Kwa familia zisizojielewa.

Olewa na OA Saizi yako, mnayeendana, ili haki Sawa itende kazi;

Au unakuta mwanaume masikini Kabisa ameoa mwanamke mwenye uwezo alafu mwisho WA siku anataka wagawane Mali. Thubutu! Yaani uje na kaptura yako kauka nikuvae upambane na Mali za Mkeo, huo ni uzumbukuku!

Haki Sawa haiwezekan Kwa watu wasiofanana. Ili iwezekane basi ndoa za mkataba ni muhimu.
Serikali naiomba ianzishe ndoa za mkataba ili kusaidia Vijana na mabinti ambao wanapata tabu kwenye hizi ndoa za siku hizi ambazo zinafuata mifumo ya kizamani kwenye dunia iliyojaa tamaa, ubinafsi, uchu wa utawala.

Haki Sawa inavunja thamani ya mwanamke, mwanamke mwenye akili timamu hawezi kuikimbilia haki Sawa.
Kwani atakosa uthamani wake kama Mwanamke.
Ile dhana ya kuhudumiwa, kutunzwa na kupendwa kwenye Haki Sawa haipo.
Kwani hivyo navyo itampasa mwanamke amfanyie mumewe (mwanaume) Jambo ambalo wanawake wengi kiasili hawataki kulisikia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
bonge moja ya thread. nashangaa imepata wachangiaji wachache.

yote uliyoandika ni kweli tupu. ndoa kwa kizazi chetu hiki ni mzigo mkubwa.

zipo shuhuda nyingi za vijana wa kiume waliopoteza focus ya kimaisha kwa kusababishiwa na ndoa.
 
Moja ya nyuzi bora kabisa tangu kuijua JF!.

Kabla ya kuoa, utii, unyenyekevu, usikivu,uaminifu vinakuwa 100%.

Baada ya kuoa Kiburi sugu, jeuri yenye kutu na uzinzi vinastawi 100%!.
 
Baadhi ya wanawake ndio sababu ya haya yote, mpaka watu wanataka ndoa za mikataba .Yaani mtu anamfanyia mwezake vituko vya makusudi alafu akitishiwa kuachika anasema kwa makusudi kabisa tutagawana mali "pasu kwa pasu " sasa maneno haya yanawaumiza sana wanaume ,wakati flani unakuta mme hataki hata kumshirkisha mke katika mipango yake kuogopa hazama inayo weza kutokea
 
Back
Top Bottom