G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Pengine watu wanaweza kufikiri kuwa sisi baadhi yetu tunaisakama sana Serikali kuhusu COVID 19 kwa kutumwa na mabeberu, la hasha! Tunafanya hivyo kwa kuwa tunawapenda sana ndugu zetu na watanzania kwa jumla.
Inashangaza sana kuona serikali inayojiita serikali makini ikitoka hadharani na kuitambia dunia kuwa Tanzania COVID 19 imepungua sana na hitokaa itokee eti maambukizi yaongezeke. Matokeo yake watanzania wengi wameamua kuishi kwa namna ya ajabu kabisa. Haya ni matokeo ya kunyimwa ukweli na wakulaumiwa ni Serikali na Wizara ya Afya kwa jumla.
Ninasema hayo kwa kuwa nimeshuhudia ndani ya siku za hivi karibuni Watanzania wenzangu wakisimbuliwa na homa kali na kikohozi huku wakiwa na dalili nyingi za Corona! Serikali iko wapi?
Kama kwa hakika tutaendelea hivi na hii tabia ya kupuuza puuza kutokana na asili yetu watanzania na mbaya zaidi tunao sasa viongozi wanaoendana na asili yetu basi tutajikuta tuligharamika kwa kiwango kikubwa na matokeo yake ni nchi kuanza kupata midororo mikubwa ya kibiashara.
Nitoe Rai kwa serikali, kusema kuwa baadhi ya Wataznania wanasumbuliwa na Corona si dhambi, kutoa tahadhari na kuhimiza watu kujikinga si dhambi. Dhambi ni mwenenndo ambao kwa sasa tumeamua kusafiri nao.
Tuweke kumbukumbu ili siku moja tuje kusemezana bila haya