Ukweli kuhusu Watanzania kuombeana mabaya, hizi si siasa nzuri

Jack Daniel

JF-Expert Member
Sep 23, 2021
2,167
10,455
Ni siku nyingi zilipita tangu Makamu wa Rais Mh:Isdor Mpango, kuwa kimya, kutoonekana kwenye hafla yoyote, bila kujulishwa yuko wapi.

Zama hizi za mitandao ya kijamii ni nzuri zikiamua kukupamba na ni mbaya zikiamua kukuchafua iwe kwa makusudi ama ukweli.

Wengi wameandika kuhusu kiongozi wao kutoonekana, wengi wamehoji wapo walioenda mbali zaidi na kutabiri yale yanayowajia vichwani mwao.

Wanasiasa wasiyoiombea mema serikali walienda mbali zaidi hadi kutupostia mambo ya ajabu ili tu kujijengea utabiri usiokuwa na maana yeyote ile.

Ukichunguza hoja zote, maswali yote, madai yote pamoja na kelele kibao, wengi wao walitaka wasikie kiongozi wetu amefariki ili kutimiza utabiri wao hili nimelifanyia uchunguzi siku zote mpaka Mheshimiwa alipojitokeza mwenyewe kututoa hofu ile jana.
inasikitisha sana.

Ndugu wapendwa Watanzania wenzangu, licha ya serikali kuwa na mapungufu na mengineyo lakini si vyema kucheza na uhai wa mtu, ni mara ya pili hii Mpango anazushiwa jambo kubwa na la hatari kama hili.

Nini nia yenu mnataka maadui wasimame na nyie wamdhuru huyu kiongozi?

Mtapata faida gani? na kwanini mumuombee mtu mabaya?

Mpango hataishi milele atakufa, kama ambavyo nafsi nyingi zimeonja na zitaonja mauti. wakati ukifika hakutakuwa na namna yeyote ile.

Mungu mbariki Mh: Mpango
Mungu ibariki Serikali yetu
Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom