Wakati nchi ikiwa uchumi wa kati, mradi wa anwani za makazi "Post Code" ukamilishwe haraka

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
512
500
Nimesikia Mkoa wa Kagera umezawadiwa kuhusu utekelezaji wa mradi wa anwani za makazi mwaka huu nikapata hamasa kutoa maoni yangu kuhusu umuhimu wa kukamilisha mradi huu nchi nzima kwa haraka iwezekanavyo ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mradi huu unaonekana kwenye macho ya wananchi kama ni kitu kidogo lakini ni kitu muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Utambuzi wa NIDA utakuwa na maana sana kama utaendana na Mradi huu. Lakini pia suala la ulinzi na usalama, ugawaji na matumizi ya raslimali za nchi, idadi sahihi ya watu, mikopo ya mabenki nk ni vitu vinavyotegemea sana anwani sahihi za makazi.

Mamlaka zinazohusika zifanyie kazi mradi huu kwa kasi ili kufikia malengo yaliyowekwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom