Wadau wahamasishwa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi kutoa huduma kwa jamii

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
WADAU WAHAMASISHWA MATUMIZI YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI KUTOA HUDUMA KWA JAMII

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojhia ya Habari imekutana na wadau wa Mfumo wa Anwani za Makazi katikati ya wiki hii jijini Dodoma kwa lengo la kuwapitisha hatua za utekelezaji wa mfumo huo na kuhamasisha matumizi ya mfumo huo katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi

Akizungumza katika kikao kazi hicho Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO wa Wizara hiyo, Bwana Gerson Msigwa ametoa rai kwa wadau hao kushirikiana na Wizara kuutangaza na kuhamasisha watanzania kutumia miundombinu ya Mfumo wa Anwani za Makazi pamoja na mfumo wa kidijitali wa NaPA kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii

“Niwahakikishie kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari muda wote tutakuwa tayari kusikiliza na kupokea maoni ya wadau wetu wote wanaoutumia mfumo wa Anwani za Makazi kutoa, kutafuta au kupokea huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi, hivyo tushirikiane kuutangaza na kuhamasisha watanzania kutumia mfumo huu”, amezungumza Msigwa

Amesema kuwa Mfumo huo ni moja ya miradi mikubwa inayotekelezwa na Wizara hiyo na baadae kutolewa maelekezo ya kutekelezwa kwa njia ya operesheni, ili usaidie kuboresha takwimu za Sensa ya Watu na Makazi inayofanyika mwezi Agosti mwaka huu wa 2022

Msigwa ameipongeza timu nzima ya Wizara pamoja na wataalamu kwa kazi nzuri ya uratibu na kutengeneza mfumo wa kidijitali wa utambuzi wa NaPA ambao utasaidia kuboresha utoaji wa huduma na kuifungua nchi katika uchumi usio na mipaka uchumi wa kidijitali

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, Mhandisi Clarence Ichwekeleza amesema kuwa takwimu zinaonesha utekelezaji wa operesheni ya Anwani za Makazi umefikia asilimia 106. 9 na Wizara inaendelea na zoezi la kuhakikina kuswafisha taarifa zilizokusanywa za Anwani za makazi ambapo mpaka sasa jumla ya Anwani 12,381,383 imeshakusanywa.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Back
Top Bottom