Mpango wa kuanza kutumia jamii namba (namba ya kipekee) kufikia uchumi wa kidigitali

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
Mpango wa kuanza kutumia jamii namba (unique number) kwa ajili ya utoaji wa huduma nchini katika ujenzi wa mfumo wa utambulisho wa kidigitali kufikia uchumi wa kidijitali

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR MUUUB) inaratibu utekelezaji wa mradi wa Tanzania ya Kijiditali (DTP). Mradi huu unajumuisha uanzishwaji wa Vituo vya Huduma Pamoja/Jamii ambao ni Mpango wa Serikali wa utoaji Huduma kwa Mwananchi katika sehemu moja (One Stop Service Centre -OSSC).

Mradi wa OSSC unatekelezwa kupitia serikali zetu zote mbili (Tanzania Bara na Tanzania Visiwani).Lengo la Serikali kwenye OSCC ni kuwezesha huduma zote kupatikana katika dirisha moja yaani “One Roof Single Window-”. Adhma hii ya Serikali itafikiwa kwa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuunganisha mifumo, kuboresha michakato ya utoaji huduma, kuandaa namba maalumu ya mpokea huduma ili kukidhi mahitaji ya vituo pamoja na kufanya mapitio mbalimbali ya Sheria zinazoguswa na utoaji wa huduma hizi sehemu moja.

Katika kuhakikisha kunakuwa na mashirikiano mazuri ya Sekta Binafsi na Sekta za Serikali kwenye kutoa huduma kwa mwananchi na kubadilishana taarifa kupitia mifumo mbalimbali ya TEHAMA, Serikali imeanza utekelezaji wa uunganishaji wa mifumo ya TEHAMA ili kusomana.

Hata hivyo, kufikiwa malengo haya kwa ufanisi, ujenzi wa mfumo wa “Digital Identity” ambao ndio utakaofanya shughuli muhimu za awali za usajili wa watu Nchini hauna budi kutekelezwa. Ili kufanikisha hili Serikali imeanza kwa kuunganisha mifumo ya ZCSRA, NIDA, RITA, UHAMIAJI, na NAPA ambayo ndio mifumo muhimu ya utambuzi wa watu Nchini.

Mfumo wa Digital Identity utatumia namba ya kipekee yaani Jamii Namba (Unique number) ambayo itatumika na mifumo mingine ya Serikali na mifumo ya sekta binafsi katika kuwatambua wapokea huduma. Matumizi ya Jamii Namba ya tafanikisha uunganishaji wa taarifa mbalimbali za utambuzi kama vile NIDA, RITA, Idara ya UHAMIAJI na ZCSRA na mifumo mingine ya Serikali na Sekta binafsi kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ubora bila kujali umri, uraia au hali ya Uhamiaji wa mtu. Mfumo wa Digital Identity ni moja ya mfumo ambao utatekelezwa kupitia mkakati wa uchumi wa Kidijitali (Tanzania Digital Economy Strategic Framework 2022/2033) kuwezesha na kurahisisha shughuli za kiuchumi za kila siku kati ya Serikali, Sekta Binafsi na mtu mmoja. Matumizi ya Jamii Namba itawezesha usalama (cyber security) na kuaminiana (digital trust) katika kubadilishana taarifa, kutoa na kupokea huduma mbalimbali ambazo kwa pamoja zinajenga uchumi wa Kidijitali. Jamii Namba itasaidia kupunguza utambulisho bandia na idadi ya vitambulisho vinavyotumika kututambulisha.Kikao cha leo, kinalenga kukubaliana na kutoa mwelekezo wa kufanikisha matumizi ya Jamii Namba.

Hivyo, wadau wakuu wa mfumo wa “Digital Identity” ambao ni WHMTH, OR MUUB, OR-ikulu, OR TAMISEMI, Uhamiaji, NIDA, RITA, ZCSRA na e-GA kujadili masuala msingi ya uunganishaji wa mifumo hiyo na kufanikisha utoaji wa Jamii Namba uchambuzi wa mifumo ya taasisi zinazohusika na unique number ili kufanikisha Tanzania kuwa na namba moja ya kipekee (Unique number) katika utoaji wa huduma, na kusaidia kuwepo na mfumo wa Digital Identity ambao ndio utakuwa msingi wa kumtambua mpokea huduma.

Taasisi zifuatazo zinahusika katika hatua ya awali ili kufanikisha mpango huu: ZCSRA – Mfumo huu ni wa utoaji wa namba ya mzanzibari Mkaazi na uthibitisho wa kuzaliwa kwa upande wa wapokea huduma Tanzania Visiwani (Zanzibar).

Kwakuwa mfumo huu ni kwa wakazi wa Zanzibar pekee, pamoja na shughuli nyingine za matumizi ya mfumo huu, mfumo utasaidia kumtambua mpokea huduma ndani ya mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunganisha na mfumo wa NIDA, mfumo wa UHAMIAJI na mfumo wa NAPA. Uunganishaji mifumo hii utasaidia kufanikisha mfumo wa “Digital Identity”.

RITA- Mfumo wa vizazi na vifo wa RITA ni mfumo muhimu katika kuwatambua wapokea huduma. Mfumo huu ndio uanaowezesha kutambua maeneo na tarehe ya kuzaliwa ya mpokea huduma kwa upande wa Tanzania Bara. Mfumo huu pia ni muhimu katika kutoa taarifa kwa mifumo mingine pale mtu anapofariki.

Uunganishaji wa mfumo huu na mfumo wa NIDA, UHAMIAJI na NAPA utakuwa ni wenye kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza mfumo wa “Digital Identity”, ambao utasaidia kuhakikisha kuwa Unique number inatolewa wakati wa utoaji wa namba/cheti cha kuzaliwa na pia taarifa zinahuishwa kwenye mfumo wa “Digital Identity” pale ambapo mpokea huduma anafariki.

UHAMIAJI: Mfumo wa UHAMIAJI ni mfumo muhimu katika kutambua Uraia wa mpokea huduma sambamba na utoaji wa huduma kwa wageni wakazi kama vile vibali vya kuishi na kufanya kazi Nchini, watalii na wakimbizi ambao kwa nyakati tofauti wawapo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaweza kupokea huduma mbalimbali.

Mfumo huu ni muhimu kuunganisha na mfumo wa ZCSRA, NIDA, RITA na NAPA katika kufanikisha utengenezaji wa mfumo wa “Digital Identity” na kutoa namba ya kupokelea huduma katika maeneo mbalimbali hususan ya mipakani.

NAPA: Mfumo wa NAPA ni mfumo wa kusaidia utambuzi wa wapokea huduma kwa kuyafahamu maeneo wanapoishi, au kutambua makazi yao ya kudumu. Mfumo huu ni kiungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mfumo wa “Digital Identity”. Kuunganisha mfumo huu na mifumo ya RITA, NIDA, UHAMIAJI na ZCSRA utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uboreshaji wa utoaji huduma kwa kupitia namba ya kipekee (unique number).

NIDA: Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa pia ni mfumo muhimu katika kufanikisha utengenezaji wa mfumo wa “Digital Identity”, mfumo huu ni muhimu kwakuwa ni mfumo unaotumika katika pande zote mbili za muungano, na unasaidia katika kuwa na taarifa za wapokea watanzania, wageni wakaazi, na wakimbizi.

Mfumo huu ndio utakaotumika kutoa “Unique Number” na kuunganishwa na mifumo ya RITA, UHAMIAJI, ZCSRA na NAPA. Ili mpokea huduma aweze kupata Unique number inayotoka kwenye mfumo wa NIDA kwasasa atapaswa kujulikana alipozaliwa, makazi yake, hali yake ya Uraia.
 
Attachments

  • Screenshot_20230717-113440.jpg
    Screenshot_20230717-113440.jpg
    71.9 KB · Views: 16
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR MUUUB) inaratibu utekelezaji wa mradi wa Tanzania ya Kijiditali (DTP). Mradi huu unajumuisha uanzishwaji wa Vituo vya Huduma Pamoja/Jamii ambao ni Mpango wa Serikali wa utoaji Huduma kwa Mwananchi katika sehemu moja (One Stop Service Centre -OSSC)
Kwahiyo wale wenye akili butu ya kwamba ofisi za serikali zijengwa mbali na miji tena kwa kutapakaa kwa kisingizio cha kupanua na kufungua miji wamepruvu failure

Kadhalika wale wenye akili ya hovyo ya kutoa huduma kwa watu wanaokuja na tie shingoni, miwani na suti nao imekula kwao
 
Mpango wa kuanza kutumia jamii namba (unique number) kwa ajili ya utoaji wa huduma nchini katika ujenzi wa mfumo wa utambulisho wa kidigitali kufikia uchumi wa kidijitali

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WHMTH) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR MUUUB) inaratibu utekelezaji wa mradi wa Tanzania ya Kijiditali (DTP). Mradi huu unajumuisha uanzishwaji wa Vituo vya Huduma Pamoja/Jamii ambao ni Mpango wa Serikali wa utoaji Huduma kwa Mwananchi katika sehemu moja (One Stop Service Centre -OSSC).

Mradi wa OSSC unatekelezwa kupitia serikali zetu zote mbili (Tanzania Bara na Tanzania Visiwani).Lengo la Serikali kwenye OSCC ni kuwezesha huduma zote kupatikana katika dirisha moja yaani “One Roof Single Window-”. Adhma hii ya Serikali itafikiwa kwa kutekeleza mambo mbalimbali ikiwemo kuunganisha mifumo, kuboresha michakato ya utoaji huduma, kuandaa namba maalumu ya mpokea huduma ili kukidhi mahitaji ya vituo pamoja na kufanya mapitio mbalimbali ya Sheria zinazoguswa na utoaji wa huduma hizi sehemu moja.

Katika kuhakikisha kunakuwa na mashirikiano mazuri ya Sekta Binafsi na Sekta za Serikali kwenye kutoa huduma kwa mwananchi na kubadilishana taarifa kupitia mifumo mbalimbali ya TEHAMA, Serikali imeanza utekelezaji wa uunganishaji wa mifumo ya TEHAMA ili kusomana.

Hata hivyo, kufikiwa malengo haya kwa ufanisi, ujenzi wa mfumo wa “Digital Identity” ambao ndio utakaofanya shughuli muhimu za awali za usajili wa watu Nchini hauna budi kutekelezwa. Ili kufanikisha hili Serikali imeanza kwa kuunganisha mifumo ya ZCSRA, NIDA, RITA, UHAMIAJI, na NAPA ambayo ndio mifumo muhimu ya utambuzi wa watu Nchini.

Mfumo wa Digital Identity utatumia namba ya kipekee yaani Jamii Namba (Unique number) ambayo itatumika na mifumo mingine ya Serikali na mifumo ya sekta binafsi katika kuwatambua wapokea huduma. Matumizi ya Jamii Namba ya tafanikisha uunganishaji wa taarifa mbalimbali za utambuzi kama vile NIDA, RITA, Idara ya UHAMIAJI na ZCSRA na mifumo mingine ya Serikali na Sekta binafsi kuhakikisha huduma zinatolewa kwa ubora bila kujali umri, uraia au hali ya Uhamiaji wa mtu. Mfumo wa Digital Identity ni moja ya mfumo ambao utatekelezwa kupitia mkakati wa uchumi wa Kidijitali (Tanzania Digital Economy Strategic Framework 2022/2033) kuwezesha na kurahisisha shughuli za kiuchumi za kila siku kati ya Serikali, Sekta Binafsi na mtu mmoja. Matumizi ya Jamii Namba itawezesha usalama (cyber security) na kuaminiana (digital trust) katika kubadilishana taarifa, kutoa na kupokea huduma mbalimbali ambazo kwa pamoja zinajenga uchumi wa Kidijitali. Jamii Namba itasaidia kupunguza utambulisho bandia na idadi ya vitambulisho vinavyotumika kututambulisha.Kikao cha leo, kinalenga kukubaliana na kutoa mwelekezo wa kufanikisha matumizi ya Jamii Namba.

Hivyo, wadau wakuu wa mfumo wa “Digital Identity” ambao ni WHMTH, OR MUUB, OR-ikulu, OR TAMISEMI, Uhamiaji, NIDA, RITA, ZCSRA na e-GA kujadili masuala msingi ya uunganishaji wa mifumo hiyo na kufanikisha utoaji wa Jamii Namba uchambuzi wa mifumo ya taasisi zinazohusika na unique number ili kufanikisha Tanzania kuwa na namba moja ya kipekee (Unique number) katika utoaji wa huduma, na kusaidia kuwepo na mfumo wa Digital Identity ambao ndio utakuwa msingi wa kumtambua mpokea huduma.

Taasisi zifuatazo zinahusika katika hatua ya awali ili kufanikisha mpango huu: ZCSRA – Mfumo huu ni wa utoaji wa namba ya mzanzibari Mkaazi na uthibitisho wa kuzaliwa kwa upande wa wapokea huduma Tanzania Visiwani (Zanzibar).

Kwakuwa mfumo huu ni kwa wakazi wa Zanzibar pekee, pamoja na shughuli nyingine za matumizi ya mfumo huu, mfumo utasaidia kumtambua mpokea huduma ndani ya mipaka ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuunganisha na mfumo wa NIDA, mfumo wa UHAMIAJI na mfumo wa NAPA. Uunganishaji mifumo hii utasaidia kufanikisha mfumo wa “Digital Identity”.

RITA- Mfumo wa vizazi na vifo wa RITA ni mfumo muhimu katika kuwatambua wapokea huduma. Mfumo huu ndio uanaowezesha kutambua maeneo na tarehe ya kuzaliwa ya mpokea huduma kwa upande wa Tanzania Bara. Mfumo huu pia ni muhimu katika kutoa taarifa kwa mifumo mingine pale mtu anapofariki.

Uunganishaji wa mfumo huu na mfumo wa NIDA, UHAMIAJI na NAPA utakuwa ni wenye kuleta mafanikio makubwa katika kutekeleza mfumo wa “Digital Identity”, ambao utasaidia kuhakikisha kuwa Unique number inatolewa wakati wa utoaji wa namba/cheti cha kuzaliwa na pia taarifa zinahuishwa kwenye mfumo wa “Digital Identity” pale ambapo mpokea huduma anafariki.

UHAMIAJI: Mfumo wa UHAMIAJI ni mfumo muhimu katika kutambua Uraia wa mpokea huduma sambamba na utoaji wa huduma kwa wageni wakazi kama vile vibali vya kuishi na kufanya kazi Nchini, watalii na wakimbizi ambao kwa nyakati tofauti wawapo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania wanaweza kupokea huduma mbalimbali.

Mfumo huu ni muhimu kuunganisha na mfumo wa ZCSRA, NIDA, RITA na NAPA katika kufanikisha utengenezaji wa mfumo wa “Digital Identity” na kutoa namba ya kupokelea huduma katika maeneo mbalimbali hususan ya mipakani.

NAPA: Mfumo wa NAPA ni mfumo wa kusaidia utambuzi wa wapokea huduma kwa kuyafahamu maeneo wanapoishi, au kutambua makazi yao ya kudumu. Mfumo huu ni kiungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mfumo wa “Digital Identity”. Kuunganisha mfumo huu na mifumo ya RITA, NIDA, UHAMIAJI na ZCSRA utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uboreshaji wa utoaji huduma kwa kupitia namba ya kipekee (unique number).

NIDA: Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa pia ni mfumo muhimu katika kufanikisha utengenezaji wa mfumo wa “Digital Identity”, mfumo huu ni muhimu kwakuwa ni mfumo unaotumika katika pande zote mbili za muungano, na unasaidia katika kuwa na taarifa za wapokea watanzania, wageni wakaazi, na wakimbizi.

Mfumo huu ndio utakaotumika kutoa “Unique Number” na kuunganishwa na mifumo ya RITA, UHAMIAJI, ZCSRA na NAPA. Ili mpokea huduma aweze kupata Unique number inayotoka kwenye mfumo wa NIDA kwasasa atapaswa kujulikana alipozaliwa, makazi yake, hali yake ya Uraia.
Kama Dubai.

Ahsante Dubai World.

Mama Samia ndipo anaponikosha hapo, anajibu kwa vitendo tu.
 
Mpango aliozungumzia mleta mada upo kitambo infact kuna msaafu umeweka wazi juu ya hii kitu na ni suala la wakati wake kuwa umefika ili andiko litimie wala havina uhusiano na Dubai World wala samia hata angekuwepo nani mpango huo ungetekelezwa tu.
 
Mipango bila kutekelezwa ipo mingi sana.
.Mazao ya Dubai World hayo.
 
Wacha we..... huenda kwenye ile 35% ya hisa za watanzania unazo za kwako weye maana si kwa mahaba haya kwa wadubei......wakati huu mama....
 
Back
Top Bottom