BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Wakaguzi wa dhahabu wagundua upungufu
Raymond Mihayo, Kahama
Daily News; Monday,November 17, 2008 @20:00
Kitengo cha Ukaguzi wa Dhahabu (GAP), kimebaini upungufu mkubwa katika mikataba ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika migodi ya Bulyanhulu, Geita ambayo imekuwa ikiipatia serikali hasara.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Utawala cha Ukaguzi wa Dhahabu katika migodi mikubwa nchini, Bruno Mteta alipozungumza na viongozi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Bulyanhulu.
Alizungumza hayo katika Kijiji cha Kakola wilayani hapa juu ya programu ya uelimishaji wa umma mkoani Shinyanga juu ya migodi mikubwa ya dhahabu. Mteta alikuwa akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi hao waliowawakilisha wananchi wao walipohoji mikataba na upungufu uliokwishabainika kupitia ukaguzi wa kitengo hicho kilichoanzishwa Agosti mwaka jana.
Alisema baada ya kitengo hicho kuanza ukaguzi katika mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick Gold Corporation na Geita Gold Mine mali ya Anglo Gold Ashanti, imebainika kumekuwapo na taarifa zisizo sahihi huku wawekezaji hao wakidai kuwa wanapata hasara, jambo alilosema si la kweli.
Alisema pamoja na kuwa ujenzi wa mgodi hauhitaji fedha nyingi na huchelewa kupata faida, lakini baadhi ya maeneo yamekuwa yakitolewa taarifa zisizo sahihi. Akitoa mfano katika mgodi wa Geita, alisema GAP imebaini kuwapo kwa taarifa za uongo juu ya matumizi ya uendeshaji wa mgodi, hali iliyosababisha mwekezaji huyo kukiri upungufu na kuahidi kulipa Sh bilioni 30 zilizokuwa zisilipwe serikalini kwa madai tu ya kugharamia shughuli za uendeshaji wa mgodi, jambo ambalo baada ya ukaguzi, iligundulika siyo kweli kwa vile haliingiliani na mkataba.
Aidha, katika ukaguzi huo imebainika kuwa wawekezaji hao wamekuwa wakijiamulia kujinunulia vitu ovyo kutoka nje ya nchi licha ya kuwa baadhi ya vitu hivyo vinapatikana nchini. Pia katika mgodi wa Bulyanhulu imebainika wazi kuwa yapo matumizi mengine ya uendeshaji wa mgodi yamekuwa yakisomeka isivyo na baada ya GAP kukagua vitabu vya mwekezaji huyo ambaye ni Barrick Gold Corporation, walikiri kuwapo kwa makosa na wameanza kuyarekebisha.
Kitengo hicho kinachosimamiwa na Wizara ya Nishati na Madini, kina kazi ya kuhakiki wingi na ubora wa dhahabu inayozalishwa na kusafirishwa nje na migodi mikubwa ili kujua thamani yake halisi na kiwango cha mrabaha kinachostahili kuingia serikalini. Kimeanzishwa baada ya Kampuni ya kigeni ya Alex Stewart (Assayers) iliyokuwa ikijihusisha na ukaguzi huo kwa niaba ya serikali. Ukaguzi huo utaendelea katika migodi mingine ikiwamo ya Tulawaka, North Mara na Golden Pride Mine