Wakaazi wa Mang'ola Arusha kumwadhibu JK kwa ahadi hewa ya barabara ya 2005... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakaazi wa Mang'ola Arusha kumwadhibu JK kwa ahadi hewa ya barabara ya 2005...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Oct 18, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  katika pita pita zangu huko Mang'ola Arusha nimekutana na wapigakura wengi ambao wanaghadhabu kubwa na JK kwa ahadi hewa ya mwaka 2005 ya kuwajengea barabara ya lami inayokadiriwa kuwa kilometa 35 hivi ambayo hata upembuzi wake wala haujaanza na hakuna fedha ambazo ziliwahi kutengwa kwa mradi huu.

  Mkaazi mmoja ambaye alijawa na hamaki, alidai JK mwaka 2005 alikuja kwenye kampeni za kusaka URAISI na kuwaahidi barabara hiyo ambayo ndicho kikwazo kikubwa cha uendelezaji wa kilimo cha zao la vitunguu. Mkaazi huyo alilalama..........."Huyu bwana ni tapeli wa kutupwa kabisa. Baada ya kutuhadaa sisi na ahadi zake hewa ambazo hana hata mpango wa kuzitekeleza sasa baada ya kufanikiwa mwaka 2005 sasa anafikiria atatumia mbinu hizo hizo kuhadaa umma wote wa watanzania kwa kuja na ahadi mlima kabisa...............Sisi hapa Mang'ola tunasubiri uchaguzi tumwonyeshe cha moto huyu jamaa ambaye hana hata aibu safari hii hata hakuja kutuona hata kutuomba msamaha na kutuelezea alishindwa wapi............."

  Nilipomuuliza ni yupi chagua lao safari hii wote niliowahoji walisema bila kificho ya kuwa ni Dr. Slaa na Chadema isipokuwa kibosile mmoja wa CCM aliyekuwa anamnadi mgombea udiwani wa chama chake.

  Kiongozi mmoja wa kitongoji wa CCM alisema safari hii wanashindwa kukipigia chama chao debe maana wataonekana kama wehu kutokana na upepo unavyovuma vibaya dhidi ya chama chao........................Nilipomuuliza kuhusu JK na ahadi zake nchi nzima jamaa huyu alikuja juu na kusema kuwa kama JK ameshindwa hizi kilometa chache tu sasa ataweza nchi nzima?

  Nilipomuuliza atamchagua nani alisema Uraisi ni Dr. Slaa na ubunge ni Chadema lakini diwani wake ni wa chama chake..............Ipo kazi kwa CCM safari hii..........
   
Loading...