Wana Rorya tumkatae Chege kama barabara ya Mika mpaka Ruari Port kwa kiwango cha lami haitakamilika

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
382
764
Moja ya ahadi ya Mhe. Chege tulipomchagua alituahidi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha barabara hii inakamilika kwa asilimia mia moja. Ujenzi wa barabara ulianza mwaka 2005 na mpaka sasa umejengwa kwa kilomita 14 tu.

Maeneo mengine ya nchi hii kila kukicha barabara za lami zinakamilishwa kasoro barabara hii iliyochukua miaka 19 bila kukamilika. Hii ni dharau kubwa sana kwa wana Rorya.

Bora tumrudishe Ndugu Wenje kama kukosa tukose wote. Kila ukisimama Bungeni ni kusifia tu unasifia nini. Hakuna mtu anyetoa fedha mfukoni mwake kwa maendeleo ya nchi.

Fedha ni za umma na hata kama ni mkopo italipwa na Watanzania. Wana Rorya tumkatae Mhe. Chege kama barabara hii haitakamilika.
 
Mleta mada ninyi ndiyo wakunyang'anywa vitambulisho vya kupigia kura. Kwa sababu mnadanganywa kirahisi sana na wanasiasa. Yaani mlimuamini mgombea ubunge kuwa atajenga barabara ya lami kwa fedha zipi alizonazo...!!!kufanya hiyo kazi?
 
Yeye alihaidi kuisimamia Serikali Sasa kama Serikali wao wameshindwa kutatua Hilo tatizo la Barabara miaka nenda Rudi, yeye kama MB atoe pesa zake mfukoni ..?
No ....Rorya mpeni Kijana Muda afanye kazi kadri Serikali inavyompa sapoti.
 
Huyu mwamba kumbe bado yupo bungeni. Jaribuni hata kubadilisha na wengine waule kidogo. Najua hakuna wa kukutetea lakini wapeni na wengine riziki
 
Bora tumrudishe Ndugu Wenje kama kukosa tukose wote.
Wenje hajawahi kuwa Mbunge wa Rorya, unavyosema 'kama ni kukosa tukose wote' ukose nini hasa?
oja ya ahadi ya Mhe. Chege tulipomchagua alituahidi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha barabara hii inakamilika kwa asilimia mia moja. Ujenzi wa barabara ulianza mwaka 2005 na mpaka sasa umejengwa kwa kilomita 14 tu.

Fedha ni za umma na hata kama ni mkopo italipwa na Watanzania. Wana Rorya tumkatae Mhe. Chege kama barabara hii haitakamilika.

Ujenzi wa barabara ulianza mwaka 2005 na mpaka sasa umejengwa kwa kilomita 14 tu.

Unaandika kwa chuki, jazba, giriba, mihemko na ukabila bila kuwa na fact zozote, Unakiri ujenzi wa Barabara umeanza 2005 ambapo Mbunge alikuwa Prof. Philemon Sarungi akaondoka 2010, akafuata Lameck Airo 2010/2020, kisha Jafari Chege 2020/24. Wote hao wamekuwa wabunge wa CCM wameshindwa kusimamia Serikali yao 'ya CCM' ijenge hiyo barabara kuanzia 2005/24.

Ndio ni wajibu wa Serikali kujenga barabara sio Mbunge, wa kuwajibishwa ni Serikali sio Mbunge na binafsi nitakupa milioni moja ukinionyesha kosa la Chege hapo.
 
Mleta mada ninyi ndiyo wakunyang'anywa vitambulisho vya kupigia kura. Kwa sababu mnadanganywa kirahisi sana na wanasiasa. Yaani mlimuamini mgombea ubunge kuwa atajenga barabara ya lami kwa fedha zipi alizonazo...!!!kufanya hiyo kazi?
🆒👍👌👏👊🤝🙏
 
Back
Top Bottom