Wajuzi wa biashara hii ya taulo za kike na pampas za watoto

eximpesa

New Member
Oct 30, 2020
3
7
Nina wazo ambalo nadhani nahitaji msaada zaidi wa kuongeza ufahamu nina kibanda tayari na kuna biashara kadhaa naendelea nazo kama mpesa ila kibanda kiko wazi nimepata wazo niweke shelf kisha nianze kuuza hizi pedi za kike na pampasi hizi za watoto na vingine vinavyo endana na hivyo.

Eneo kibiashara kuna mzunguko wa watu wa kutosha. Ombi langu ni kwa wajuzi wenye ufahamu wa hii biashara ugumu wake ni upi na pia uendeshaji wake uko vipi kuanzia mtaji na faida yake.
 
Nina wazo ambalo nadhani nahitaji msaada zaidi wa kuongeza ufahamu nina kibanda tayari na kuna biashara kadhaa naendelea nazo kama mpesa ila kibanda kiko wazi nimepata wazo niweke shelf kisha nianze kuuza hizi pedi za kike na pampasi hizi za watoto na vingine vinavyo endana na hivyo.

Eneo kibiashara kuna mzunguko wa watu wa kutosha. Ombi langu ni kwa wajuzi wenye ufahamu wa hii biashara ugumu wake ni upi na pia uendeshaji wake uko vipi kuanzia mtaji na faida yake.
eximpesa

Kwenye biashara zote kwa ujumla; ukitaka kujua kama biashara inalipa ama la, angalia uwingi wa wateja. Je demand ipo ya kutosha? Na kama ipo, je kuna competition ambayo inaweza ikasababisha demand kushuka? Kama swali la kwanza ni ndiyo na la pili ni hapana, then there you are,... ni biashara unayoweza kuifanya pasipo shaka yoyote na
ikakulipa pasipo tatizo lolote.

Labda nyongeza yangu tu kuhusiana na biashara ya bidhaa hii ambayo matangazo yake yamekuwa unnecessarily AMPLIFIED kiasi kwamba pengine labda kuna haja ya mamlaka zinazohusika kufanya RECTIFICATION ili amplifaya hizi zisije zikatengeneza UNWANTED SIGNALS ambazo hazihitajiki. Mimi kwa upande wangu ningependa kushauri yafuatayo, maana sasa tunakoelekea ni kwamba watoto wanaonekana kuanza kuhamasishwa na kuzoeshwa kutamka maneno magumu magumu pasipo kujali hata maadili. Nashukuru sana kwamba jana kiongozi wetu mkubwa wa kiroho, MUFTI MKUU alionekana kuongelea swala hili la maadili. Concern yangu hasa mimi ni kwenye hii mushrooming ya maongezi yanayohusiana na TAULO ZA KIKE (TK), kwenye media, especially kwenye TV.
Nadhani sasa tuna zaidi ya mwaka, kila siku ukiwasha TV huwezi hukosi kukutana na maneno haya, yanatamkwa tena na watoto wadogo wamefundishwa kuyatamka katika namna ambayo hadi wakati mwingine yanatia aibu. Mwanzoni yalianza kama kampeni, lakini nadhani kwa sasa hivi yameshagueuka na kuwa MATANGAZO YA BIASHARA KWA MGONGO WA KAMPENI. Sasa mimi naanza kujiuliza swali, HOW LONG DOES A COMPAIGN SUPPOSED TO LAST???.

Kawaida kampeni huwa ina muda, baada ya hapo inaisha. Na kama pengine
swala linalokuwa compaigned ni endelevu, basi kampeni hizo zinatakiwa kuwa PERIDUCAL, sawa tu na kama wanavyofanya viongozi wetu wa kisiasa

Kwa upande wangu mimi, mpaka muda huu nimeshabaini matatizo kadhaa yafuatayo kuhusiana na haya maswala ya TAULO ZA KIKE (TK)

MOJA: Ilianza kampeni ya TK, sasa hivi imeshageuka na kuwa matangazo yabiashara
MBILI: Maneno yanayotumika kwenye matangazo yake ni makali, ILA KWA BAHATI NZURI NI KWAMBA YANARUHUSIWA. Hata hivyo, pamoja na kwamba maneno haya yanaruhusiwa, basi yalitakiwa yatumike kwa kiasi, na si kwa frequency ambayo eshafikiwa hadi muda huu
TATU: Wanaotumika na kampeni au matangazo haya ni watoto ambao rika lao
bado halijafikia hatua ya kuwa wanatamka tamka maneno makali mara kwa mara mbele ya hadhira ya watanzania, tena kwenye media kubwa kama TV
NNE: Kama swala la TK ni kampeni, basi inabidi lifikie mahali lipumzike kwa muda, litaendelea tena huko mbele ya safari. Mfululizo wa kampeni hii yenye maneno makali unaweza ku-compromise maadili ya watoto na ambao hasa ni walengwa wa kampeni hii
TANO: Kama kampeni ilishabadilika na kuwa ni matangazo ya biashara, ushauri wangu ni kwamba watoto wasitumike tena kwenye matangazo hayo, haukna ulazima wowote wa wao kuendelea kutumika

MWISHO NA MUHIMU KABISA, kampeni hii inatumia SLOGAN au kauli mbiu ya "NINAMTHAMINI". Slogani hii ina kasoro moja kubwa kwamba haiendani na
Kampeni husika kwa sababu lengo lake ni kuwahamasisha wa-Tanzania wote kwa ujumla wao, kuwajali watoto kuhusiana na TK bila kujali ni watoto walio majumbani mwao ama la. SLOGANI ya NINAMTHAMINI inaonyesha kama inawahamasisha watazania kuwajali watoto wao individually; yaani watoto wale walionao majumbani mwao tu basi; na kama mtu hana mtoto basi SLOGANI inambagua asihusike.

Mbali na hilo, SLOGANI ya NINAMTHAMINI inaendana zaidi na watu ambao ni wachumba au wapenzi ambao mara nyingi uhusiano wao unakuwa ni wa watu wawili tu na si zaidi; yaani mvulana mmoja tu na msichana mmoja tu. Swala la uchumba huwezi ukakuta uhusiano ambao ni MULTIPLE kwamba mchumba mmoja wa jinsia moja ana wachumba wawili au zaidi wa jinsia nyingine tofauti na ile ya kwake
Kinyume na ilivyo kwa kampeni hizi za TK, uhusiano wake unaonekana ni MULTIPLE, kwamba hata yule ambaye hana watoto anaweza kuchangia.

Kutokana na hoja hizi hapa juu, mimi kwa upande wangu ningependa kushauri mambo MAWILI makuu yafuatayo

MOJA: KAMPENI HII IWE PERIODICAL, ISIWE INAKWENDA TU MOJA KWA MOJA; INAKUWA MONOTONOUS NA INAWEZA KUSABABISHA KUVURUGIKA KWA MAADILI YA
WATOTO. NI KWA SABABU INATUMIA MANENO MAKALI MUNO AMBAYO HAYASTAHILI
KUKAA YANASIKIKA SIKIKA MASIKIONI MWA WATU MARA KWA MARA, ACHILIA
MBALI KWA WATOTO WENYEWE AMBAO NDIYO WAHUSIKA WAKUU. SIGNAL YA MATANGAZO HAYA IMEKUWA TOO AMPLIFIED, INAHITAJI KUWA RECTIFIED.

MBILI: SLOGAN YA KAMPENI IBADILIKE KUTOKA "NINAMTHAMINI" NA KUWA

"TUNAWATHAMINI"

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Back
Top Bottom