Janeth Mahawanga agawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike 700

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
MH. JANETH MAHAWANGA AGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE 700.

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Elias Mahawanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tisha Mama Foundataion Kwa kushirikiana na Taasisi ya T-MARC Tanzania amekabidhi taulo za Kike kwa wanafunzi 700 katika shule ya Sekondari Makumbusho kuelekea kilelele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani tarehe 08/03/2023.

Mhe. Mahawanga ameipongeza sana T-MARC Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha Watoto wa Kike wanaendelea kupata hedhi salama ili kulinda afya zao maana hakuna maisha bila hedhi salama.

Vile vile, Mhe. Mahawanga ameipongeza sana Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa inayofanyika kuhakikisha sekta ya Elimu inaboreshwa sambamba na kutengeneza mazingira rafiki kwa Wanafunzi kupata elimu bora ikiwemo ujenzi wa madarasa, Elimu bure kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kufundishia kwa Walimu.

Katika zoezi hilo Mhe. Mahawanga alipata wasaa mzuri wa kuzungumza na Mkuu wa shule na baadhi ya Walimu ambao ndio walezi ili kubaini changamoto za kiutendaji ambapo ameahidi kuziwasilisha mahali husika ili ziweze kushughulikiwa. Kwa upande wao Walimu hao wametoa shukurani zao kwa msaada wa taulo hizo kwani zitapunguza ongezeko la utoro shuleni.

Lakini pia Mhe. Mahawanga alikuwa ni wasaa mzuri sana kuzungumza na Wanafunzi wote wakike na wa kiume ambapo amewataka Wanafunzi hao kutochanganya mapenzi na masomo pia amewasisitiza zaidi kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia baina yao na kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie ili wote kwa pamoja wawe salama, wawe watoto wenye maadili na kulinda utu wao.

Sambamba na hayo Mhe. Mahawanga amewakumbusha Wanafunzi hao kusimamia malengo na ndoto zao na kuwasisitiza kuwa hawawezi kufikia malengo yao bila ushirikiano, juhudi binafsi na nidhamu. Vile vile amewasihi wazingatie kilichowapeleka shule na si mambo yasiyohusiana na masomo kwani wanajukumu kubwa la kupambania ndoto zao maana kila kitu kinawezekana.

Mwisho, Mhe. Mahawanga amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwani uhitaji kwenye jamii bado ni mkubwa mno hususani kwa vijana walio mashuleni ambao ndio Taifa la kesho.

WhatsApp Image 2023-03-02 at 11.33.46.jpeg

WhatsApp Image 2023-03-02 at 11.39.50.jpeg

WhatsApp Image 2023-03-02 at 14.58.00.jpeg

WhatsApp Image 2023-03-02 at 14.58.00(2).jpeg

#TishaMama.
#MamaVikoba

#ItazameDarKiutofauti

#KaziIendelee.​

Pedi zinauzwa hadi 1500 afu hao wanapeleka pc 1 wapate picha, warushie Donors ili wapewe misaada.
Mhe. Mahawanga anawakaribisha washikadau kama wewe pia uweze kufanya kwa sehemu yako ili watoto wa kike wasaidiwe zaidi.
 
amekabidhi taulo za Kike kwa wanafunzi 700 katika shule ya Sekondari Makumbusho
thawabu halisi ya kujinyima au kujitoa ni kuwapa wenye uhitaji hasa, kwa shule kama makumbusho i dont think kama ni kweli wanafunzi idadi hiyo wote wana uhitaji hasa ule tunaosema uhitaji. alichofanya hapo Janeth ni SIASA kutafuta popularity.

Kama anahitaji popularity angezama kando kando huko Chanika, Kimbiji na maeneo mengine ya pembezoni kama issue ni Dar, lakini angeenda hata huko kwao Kilombero kutoa assistance bado angeeleweka,. Kikubwa angebebana na habari na same mesage kwamba ame assist ingefika na ingekuwa kwa maana halisi!!
 
MH. JANETH MAHAWANGA AGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI WA KIKE 700.

Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janeth Elias Mahawanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Tisha Mama Foundataion Kwa kushirikiana na Taasisi ya T-MARC Tanzania amekabidhi taulo za Kike kwa wanafunzi 700 katika shule ya Sekondari Makumbusho kuelekea kilelele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani tarehe 08/03/2023.

Mhe. Mahawanga ameipongeza sana T-MARC Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha Watoto wa Kike wanaendelea kupata hedhi salama ili kulinda afya zao maana hakuna maisha bila hedhi salama.

Vile vile, Mhe. Mahawanga ameipongeza sana Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa inayofanyika kuhakikisha sekta ya Elimu inaboreshwa sambamba na kutengeneza mazingira rafiki kwa Wanafunzi kupata elimu bora ikiwemo ujenzi wa madarasa, Elimu bure kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita na kuhakikisha inaweka mazingira mazuri ya kufundishia kwa Walimu.

Katika zoezi hilo Mhe. Mahawanga alipata wasaa mzuri wa kuzungumza na Mkuu wa shule na baadhi ya Walimu ambao ndio walezi ili kubaini changamoto za kiutendaji ambapo ameahidi kuziwasilisha mahali husika ili ziweze kushughulikiwa. Kwa upande wao Walimu hao wametoa shukurani zao kwa msaada wa taulo hizo kwani zitapunguza ongezeko la utoro shuleni.

Lakini pia Mhe. Mahawanga alikuwa ni wasaa mzuri sana kuzungumza na Wanafunzi wote wakike na wa kiume ambapo amewataka Wanafunzi hao kutochanganya mapenzi na masomo pia amewasisitiza zaidi kujiepusha na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia baina yao na kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzie ili wote kwa pamoja wawe salama, wawe watoto wenye maadili na kulinda utu wao.

Sambamba na hayo Mhe. Mahawanga amewakumbusha Wanafunzi hao kusimamia malengo na ndoto zao na kuwasisitiza kuwa hawawezi kufikia malengo yao bila ushirikiano, juhudi binafsi na nidhamu. Vile vile amewasihi wazingatie kilichowapeleka shule na si mambo yasiyohusiana na masomo kwani wanajukumu kubwa la kupambania ndoto zao maana kila kitu kinawezekana.

Mwisho, Mhe. Mahawanga amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwani uhitaji kwenye jamii bado ni mkubwa mno hususani kwa vijana walio mashuleni ambao ndio Taifa la kesho.

View attachment 2534804
View attachment 2534805
View attachment 2534806
View attachment 2534807
#TishaMama.
#MamaVikoba

#ItazameDarKiutofauti

#KaziIendelee.​

Hii nchi bado sana
Hata uchumi wa kati sijui tulifikaje kipindi kile
 
Kama lengo ni kutoa msaada kwa watoto wa kike waliopo shuleni, kuna haja gani ya kwenda na waandish wa habari?
 
Back
Top Bottom