Lengo ni mbowe aachie uenyekiti. Mbowe ndio kikwazo cha kuisambaratisha cdm .Na nafikiri ccm wana mtu wao ,pandikizi limeandaliwa tayari. WAKISIKIA MBOWE KAACHIA UENYEKITI BASI WATASHEREHEKEA.Mambo mawili yatatokea mosi kupandikuza mgogoro ktk mchakato wa kumpata mkitI mpya au kuhakikisha wanaweka mtu wao. TUSUBIRI!
Sio kweli Mbowe asidanganye watu kuwa eti CCM ndio wanasababisha migogoro .
Migogoro anaisababisha yeye kwa akili yake kuona kuwa yeye ndio pekee ndani ya Chadema mwenye uwezo wa kuongoza.
Hata CCM siku mwenyekiti wao atakaposema kuwa yeye ndiye pekee na anakaa madarakani milele ndio siku chama kitakapo sambaratika. Dunia ya leo na akili za binadamu wenye maarifa walishaona kuwa Demokrasia ndio suluhu ya kila kitu kwenye siasa katika karne hii yenye watu wengi wenye maarifa ,wakati huo huo wengi wanataka kuwa vingozi. Utapataje mmoja kwa amani bila demokrasia?
UDP na TLP zimekufa kwa sababu ya utaratibu wa kuwaabudu wenyeviti wao na kuona hakuna Mwingine mwenye uwezo.
Demokrasia ni kitu muhimu sana popote sio kwenye serikali tu hata ndani ya vyama.Ni lazima watu waone Mabadiliko.
Hebu kumbuka jinsi uchaguzi wa TLS serikali ilivyotumia kila Mbinu kuweka pandikizi lao lakini walishindwa kwa sababu ya kuheshimu Demokrasia. Kama wangelazimisha kuwa uchaguzi usifanyike na Rais wao aendelee kuwa Lisu tu hakika wangekua na migogoro wa ndani!
Sasa kama walishindwa kupandikiza pandikizi lao TLS iweje waweze kwa Chadema kikuu cha Upinzani ?
Huo woga wa Mbowe ndio utakaoharibu na kuua chama.
Ni Ukweli ulioko wazi wala tusiilaumu serikali wala CCM kuwa kuwa wanataka kuweka pandikizi .
Hebu tuangalie jambo moja linaloweza kutokea kwa sababu lipo na litafikia mwisho kwenye Kesi za Mbowe inaweza kutokea kwa mfano akala mvua ya miaka gerezani na kazi ngumu sana. Hilo ni jambo ambalo linaprobability ya kutokea mana kesi zake ziko ni za jinai zote na serikali ya awamu hii haikurupuki kufungua kesi kitoto kitoto.
Sasa badala ya Mbowe kujiweka Pembeni na kuitisha uchaguzi ambao atausimamia yeye kama Mwenyekiti mwenye uchungu na chama anaacha Siku inatokea mara paa Kesi ya Mbowe na wenzake wamehukumiwa Kwenda gerezani mfano kifungo cha miaka mitatu(Ni mfano tu na tahadhari kwa nia njema kabisa).Je, hapo kwa MTU mwenye akili kubwa sio za kubisha bisha na kupinga pinga tu, haoni kuwa chama kitaingia kwenye Mgogoro mkubwa wa kugombea Madaraka kwa sababu wote watakua ni makambale yasiyo na msimamizi wa uchaguzi.
Hapo ndipo CCM itaweka mamluki mana hakuna mtu wa kuratibu uchaguzi.
Mbowe na viongozi wenzake hebu kaeni chini muitishe mkutano mkuu mujadili kwa kina na kutoa uhuru na uwazi kuhusu mustakabali wa chama bila kuwanyoishea wenzenu vidole.
Toeni nafasi kwa watu wenye maono mapana wajitokeze ili kila mmoja aeleze maono yake na nini mipango sahihi ya kukiongoza chama.
Chama kinasambaratika na ruzuku inapungua kila siku na viongozi wapo bize na kesi zinazowakabili.
Lazima aje mtu Mwingine atakayekivusha Chama.
Siamini kuwa chama hakina watu zaidi ya Mbowe. Siamini kabisa . Wapo ila tunachelewa kuwapa nafasi . Kwa sasa wabunge wote watapukutika kwa sababu ya Mbowe kuingilia Uhuru wa Wabunge hata kwenye shughuli za Kimaendeleo ambazo ni kosa kubwa analofanya.Sio demokrasia kushindwa kuwapa wawakilishi wa wananchi fursa ya kushirikiana na serikali kuleta maendeleo.
Uchaguzi wa serikali za mitaa unakuja mwakani huku chama kikizidi kupoteza majembe ya kazi kwa Vifo ,kushambuliwa na kuhama chama; Tumepoteza watu mahiri kama Tambwe Hiza (Mungu amrehemu ), Waitara, Lisu (kwa kuumizwa hataweza mikiki mikiki ile ya mwanzo kwa kipindi kirefu) na wengine wengi kwa sababu zile zile tunazozipigia kelele za udikteta na kulazimishana kupinga mambo hata yale yanayohusu maendeleo ya watu kwenye majimbo yao.
Mbowe ana Kesi kubwa kubwa ambazo kwa misingi ya sheria na utawala wa sheria anaweza akaionja na kuila Jela (Sifurahii ila naona jinsi anavyoshindwa kuliona hili na kuweka Chama kwenye mikono ya mtu salama mapema).
TUKUMBUKE KUWA NCHI IKIKOSA DEMOKRASIA YA KWELI INAKUA NA VURUGU NA MGAWANYIKO halikadhalika CHAMA KIKIKOSA DEMOKRASIA PIA KINAINGIA KWENYE MIGOGORO ISIYOISHA NA MWISHO WAKE KINASAMBARATIKA KAMA NCHI YA LIBYA.
MAHALI AMBAPO HAKUNA DEMOKRASIA ADUI ANAINGIA KWA WEPESI KULIKO MAHALI PALIPO NA DEMOKRASIA.