Walioingia bungeni kwa ‘Upepo wa Lowassa’ waanza kuaga majimboni. Wamo Waitara, Komu, Kubenea, Mdee na wengine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,543
141,351
JK alisema za kuambiwa changanya na za kwako.

Baadhi ya wabunge ambao walibahatika kuingia bungeni kwa kubebwa na kura za " mahaba" kwa mzee Lowassa wameanza kujitafakari kama wagombee tena au wavute mafao yao na kusepa.

Mwita Waitara ameshaliachia jimbo la ubungo kwa kisingizio cha kwenda Tarime kumkomesha Heche wa Chadema lakini wadadisi wanasema amemkimbia boss wa jiji la Dsm mh Makonda.

Wengine wanaofungasha virago majimboni ni pamoja na Halima Mdee wa Kawe Kubenea wa Ubungo na Komu wa Moshi vijijini.

Mchungaji Msigwa bado anapigania jimbo lake pale Iringa japokuwa inaelezwa anapoteza muda wake bure kwani Salim Asas anakubalika na wanyalu wa itikadi zote.

Jumamosi njema!

Maendeleo hayana vyama!
 
Taka taka kabisa
Mdee ni Mbunge wa Kawe wakati Mzee Lowassa ni PM wa TZ,Iweje useme kaingia Bungeni kwa upepo wa Ngoyai?
Taka=taka

2005-2010 Halima alikuwa Mbunge wa Viti maalum

Mbunge wa Kawe wakati huo alikuwa Rita Mlaki ambae pia alikuwa Naibu waziri wa Ardhi chini ya Ndugu John Magufuli

Kaanza kuwa Mbunge wa Jimbo 2010 yeye na Mnyika

Vijana wa siku hizi sijui mnakula nini kinachotoboa memory zenu
 
CCM akili wanakabidhi kwa Polepole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom