Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by dudus, Jan 3, 2012.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,749
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  • Kukutana Diamond Ijumaa
  • Mikoa Yote Nchini Kushiriki
  • Abas Syskes, Masheikh Kuunguruma
  Gazeti la LULU la leo Jumanne - 03 Januari 2012 linaripoti:

  Kongamano la Kitaifa la Uzinduzi wa Jukwaa la Katiba la Waislamu nchini linatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Habari za kuaminikia ..... zinafahamisha kuwa, kongamano hilo la siku moja linaloelezwa kuwa la kihistoria litafunguliwa na Abbas Syskes ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ...

  Pia wanasheria, masheikh mbalimbali wa jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake, pamoja na ujumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani watashiriki.

  Akithibistihs habari hizo, ...., Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema hatua zote za maandalizi ya shughuli hiyo zimekamilika. ...

  Akizungumzia maudhui ya kongamano hilo, Sheikh Ponda alisema kuwa ni pamoja na kuzindua rasmi chombo kitakachojishughulisha na utoaji elimu ya katiba kwa jamii ya Waislamu nchini.

  "Chombo hicho ambacho tumekubaliana kitaitwa Jukwaa la Katiba la Waislamu, kitakuwa na jukumu la kuhakikisha Waislamu kote nchini wanakuwa na kauli moja juu ya masuala yanayohusu dini na maisha yao amabayo wangependa yawemo kwenye katiba mpya", alisema.

  Akifafanua namna Jukwaa hilo litakavyofanya kazi hiyo, Sheikh Ponda alisema kuwa, kabla ya kutazama yanayohitajika kuwemo kwenye katiba mpya, watatangulia kutoa elimu juu ya katiba ya sasa ...

  "Baada ya hapo ndipo Jukwaa litaketi na kutafakari kwa kina mahitajio ya waislamu tunayodhani ni muhimu yakaainishwa ndani ya katiba ya nchi", alizungumza Sheikh Ponda.

  ...


  Wakuu kwa muhtasari ni hayo - full stori, tafadhali pata nakala yako ya LULU.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  sawa! ms aje na vihoja vyake
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Haki ya Kwanza, wapewe Jukwaa la Kukutana na Rais Ikulu kama "Wenzao" ili kusiwe na upendeleo!
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,749
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Kwanza, heko kwa waislamu kwa uamuzi ambao binafsi nadhani ni mzuri wa kutoa elimu kwa jamii ambayo kimsingi inahitaji sana elimu ya katiba ili kuweza kufikia maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa katiba mpya.

  Pili, wasiwasi wangu ni kwamba msije kuwa mnakwenda kinyume na sheria ya katiba mpya iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni. Kama wataalamu wenu wameipitia na kujiridhisha haina tatizo basi no problem. Vinginevyo, ingekuwa vizuri kama mgeanza na kuipinga sheria husika kabla ya kujikita kwenye kutoa elimu ya katiba kwa waumini wenu.

  Tatu, MNACHOELEKEA KUKIFANYA NI SIASA. Hivyo tafadhalini makundi mengine ya kijamii kama Vyama vya Siasa au madhehebu mengine nao watakapoanza kuielimisha jamii pana yaani watanzania wote (na sio waumini wao tu kama ninyi) msisimame upande wa watawala dhidi ya makundi hayo.

  Nne, ingependeza kama elimu mtakayoitoa ingekuwa kwa jamii nzima badala ya watu wenu tu. Hebu jitahidini sana kupunguza u-sisi.

  Tano, bado nashindwa ku-link sawasawa makala za Mohamed Said, familia ya Sykes, na siasa za nchi yetu. Hili linanipa shida sana.

  Nawasilisha.
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Katiba ipi :
  1. Ya Bakwata
  2. Ya JMT
   
 6. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  At least hiyo ni hatua moja sahihi ya kuelekea right direction. Hili lilitakiwa lifanyike mapema na sio ktk kujadili katiba tu ispokua kujadili mengi ambayo waislam yanawahusu kama waislam na yanayowahusu kama raia wa kawaida.

  Kwa hakika hasa hii ni picha ndogo ya picha kubwa ya kazi ambazo bakwata ilitakiwa kufanya. Wengi wanawasiwasi kua waislam kama wataachiwa kupanga mambo yao wanaweza kua tishio kwa jamii nyingine ingawaje hawaelezi hasa kwanini wana wasiwasi huo.

  Nature ya uislam haihamaisishi kumfanyia uadui mtu mwengine yoyote. Lakin mpaka waislam watakapopewa nafasi na wao wenyewe watakapo jipanga na kupuuza tofauti zao ndogondogo ambazo hazina msingi watakua ktk position ya kulionyesha hilo kama reality.

  Wakati umefika Bakwata ifanye kazi zake kwa ufanisi na kila mtu apewe jukumu linalostahili na vigezo vinavyostahili. Kwa mfano ni muhimu ktk kujadili swala la katiba wakapatikana wataalam ambao wanaifahamu vizuri sheria ya nchi na wanafahamu vizuri sheria let say ya kiislam. Hapo wataweza kufanya balance kua kitu wanachojaribu kukiproposal kinaweza kweli kikafanyiwa kazi ktk secular government?
  Vinginevyo busara itumike ktk kuyaadress marekibisho yanaykusudiwa ktk njia ambazo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Hao yote ni magumu kufanyika bila ya elimu ya kutosha. Jaribuni kuwahusisha wataalam mbalimbali ili juhudi hizi muhimu zisipotee bure. Good luck
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,947
  Likes Received: 1,272
  Trophy Points: 280
  3. Ya Tanganyika
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hii BAKWATA si ndio wakina flani hawataki kuisikia? Hii si ndio iliundwa na 'marehemu' Nyerere?

  Ngoja tuone sasa.
  Binafsi nafikiri ni jambo jema tu.
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  habari njema kila kitu kitapendeza kama kila kundi likiungana ma kutafakari kwa pamoja na kutoka na kauli moja.
  sio hawa waje na maandamano na wengine wayazuie.
  jamii ya wakosa ajira nasi tutafute jukwaa letu ili tuunde timu ya kushughulikia mambo yetu.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mapanya mengi shimo halitachimbika na asili ni asili tu .Lini maji yalipanda mlima ? Kuongea sawa ilakutenda mh .Naangalia tu
   
 11. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wataalam mbali mbali, very good. Naunga mkono 100%. Nachotia shaka ni msimamo wa Waislamu, je wanapenda maoni ya watu wengine, hususan wataalam? Hotuba ya Mh.Dokta pale Masjid Gadaffi, kwenye baraza la idi iligusia jambo moja la mahakama ya kadhi na hapo nilisikia Mh.Dokta akiongelea ushiriki wa Prof....(simkumbuki jina) ambaye ni mtaalamu wa sheria na sharia. Hilo waislamu hawakulipenda na ndio hasa msingi wa kufanywa kongamano hili ambalo dhahiri litaendeshwa kwa hisia na si hali halisi.

  Mimi nachoona hapa ni kama wanataka kuwa wa kwanza kuhukumiwa na sheria ambayo waliishangilia juzi juzi tu hapa iliposainiwa na Mh.Dokta. Unaposhangilia mvua milimani kumbuka maji huelekea bondeni, sasa tuliodhani itawabana CDM kufanya harakati sasa ndio tuone ugumu wa kuchekelea dhambi.

  Na mwisho nikukosoe kidogo (hapo kwenye red). Nature ya Uislamu ni kinyume kabisa na maoni yako. Utanibishia kisiasa au kwa kuchelea usionekane mbaya lkn ukweli hubakia kuwa ukweli. Soma Quran 9:5
   
 12. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,749
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye green: anaitwa Prof. Juma Mikidadi ni gwiji la Sharia.

  Hapo kwenye
  red ya kwanza: Hata mimi nina mashaka hayo. Kama kuna kitu ambacho hawa jamaa hawakukitarajia na kimewaudhi ni hilo la JK juu ya mahakama ya kadhi. Naamini kabisa HISIA badala ya HOJA zitatawala; kama watu wenyewe ni akina Basaleh et. al, sijui!

  Hapo kwenye
  red ya pili: Kanuni za asili ziko wazi; ukimnyoshea mwenzio kidole, vinne vanakuelekea wewe.

  Hapo kwenye
  maroon: Naamini kabisa Bi Faiza Fox atatusaidia hilo tena kwa ufasaha.
   
 13. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  mkuu kwa kukusaidia tu waislamu tatzo lao kubwa ni hierarchy ya uongozi.
   
 14. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Nawatakia kila la heri ila wasigeuze suala hilo kuwa la Waislam Vs Wakristu...liwe suala la kujadili katiba ya JMT.
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Lisikupe shida, ni vema ukasubiri mpaka hiyo siku ikifika, na busara zaidi ujue nini kimezungumzwa halafu una haki ya kuwa na wasiwasi na mimi nitakuunga mkono kabisa ...so let us stay tuned
   
 16. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  BAKWATA ni WANAFIQ tu wapo kwa maslahi yao !
   
 17. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tuwe na subira watakachojadili tutakisikia live
   
 18. K

  Kinyenyefule Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu,hakuna haja ya kutoa maneno ya kuudhi,ni vizuri kujadili mada kwa hoja.
   
 19. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,749
  Likes Received: 6,021
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimekusoma ila kwa uzoefu anybody can guess mada zitakazotawala. Sidhani kama watajikita sana kwenye hayo yaliyoripotiwa na gazeti badala yake tegemea mada za ajabu ajabu.

  Frankly speaking; hebu tusubiri halafu uone kitakachojadiliwa then linganisha, kwa mfano, na Waraka wa Kanisa kwa Watanzania siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana then see the differences.

  Sisemi kwamba ni lazima maazimio yafanane na waraka wa kanisa la hasha bali wakati Waraka ulilenga watanzania wote wao, japo ni katiba ya nchi, "watajipendelea wao tu" wengine aghalabu wakitajwa itakuwa kwa "ubaya". Wait and see.
   
 20. c

  chama JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Acha kashfa za kidini, kama huna jema la kusema kaa pembeni, waislamu hatuhitaji hiyo special treatment kinachotakiwa ni chombo chenye kutoa miongozo sahihi kwa waumini, Bakwata ilianzishwa kwa nia njema tu lakini ukweli imeshindwa kutekeleza majukumu yake kama chombo, huu ni mwanzo mzuri tu, naamini waislamu wakieleshwa haki zao msingi mabadiliko makubwa ya kisiasa yatatokea Tanzania, kumbuka baadhi ya wanasiasa wetu wameanza kupandikiza chuki za kidini kwa maslahi yao binafsi.

  Chama
  Gongo la Mboto DSM.
   
Loading...