Waislamu tanzania kususia bidhaa za mfanyabiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waislamu tanzania kususia bidhaa za mfanyabiashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by changamoto, Sep 26, 2008.

 1. c

  changamoto Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislamu wana mkakati wa kususia bidhaa mbalimbali za mfanyabiashara maarufu nchini ambaye ananasibisha Uislamu nchini na Ugaidi na kushabikia matumizi ya kondomu na zinaa kupitia kwenye vyombo vyake vya habari.

  Kwa mujibu wa redio Kheri, mfanyabiashara huyo ambaye vyombo vyake wala jina lake havikutajwa alikuwa ni gumzo lililochukua mdua mrefu katika kikao cha hivi karibuni cha viongozi hao.

  Inavyoelezwa ni kwamba bwana huyo anajali fedha zaidi kuliko maadili na mahusino mema kati ya Watanzania.

  Ametuhumiwa pia kuwa na chuki binafsi na wafanyabiashara wenzie ambao ni Waislamu ambao kaika miaka ya hivi karibuni wamenza kupewa heshima ambazo zamani alikuwa akipewa yeye.

  Katika kikao hicho pia kumezuka madai ya Serikali kubagua Waislamu pamoja na bunge kutokuheshimu siku ya Ijumaa ambayo ni siku muhimu kwa Waislamu.

  Hivi karibuni bunge lilifungwa sikuya Ijumaa tena katika saa za kusali bila ya wabunge Waislamu kukataa jambo hilo.

  Viongozi hao wamewataka pia viongozi na watumishi wa serikali na vyama vya kisiasa ambao ni Waislamu kukomesha tabia ya kujidharau na kuidharau dini yao huku wakitoa heshima na kuwa waoga kwa dini nyingine.

  Imesemekana hivi sasa viongozi na watumishi wa umma ambao ni Waislamu ndio wanaowanyanyasa Waislamu wenzao kuliko wale wasio Waislamu.

  Hata hivyo, baadhi ya wazungumzaji wamedai kuwa matatizo mengi ya Waislamu yanatokana na kutokuwa na viongozi bora na wa safi na wamefananisha dini hiyo na jengo lenye paa bovu.

  Kutokana na sababu hii dini hiyo imeshindwa kuwa na mipango na mikakati madhubuti ya maendeleo maana viongozi wake mara kwa mara wanaishia katika mapambano ya ndani kwa ndani na kulinda nafasi zao ambazo zimegeuzwa njia ya kujipatia riziki wala sio fursa ya kuongoza umma wa kiislamu barabara!

  Amedai kiongozi mmoja mwenye msimamo huu kwamba hadi hapo Waislamu watakapojipanga vyema na kuwa na umoja siku zote watakuwa watu wa kulalama na matatizo wakati wana uwezo wa kuweka ajenda muhimu katika namna nchi yao inavyoendeshwa labda kuliko hata watu wa dini nyingine.
   
 2. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mmh hapo sisemi

  sijui na wakristo wakigomea bidhaa za waislam itakuwaje.

  just a comment

   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  kama huyo mfanyabiashara akisema anatoa misaada ya kusaidia vijana au kina mama watajipanga mistari au wanasusia biashara zake tu? Inanikumbusha kisa kimoja cha Mchungaji na Mfanyabiashara mmoja Mbunge...
   
 4. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani Manji, mbona unaanza kumwandama tena Reginald Mengi wangu? Huyu anatupenda sana waislaamu. Nilikuwa kimya muda mrefu nilikuwa kwetu Jang'ombe. Amesaidia sana waislaamu huyu hata kwetu. Tumpe heshima badala ya kushambulia hasa katika kipindi hiki cha ramadhani.

  Asha
   
 5. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni vita kati ya Mengi na Manji sasa imehamia kwenye nyumba za ibada
   
 6. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Watu wachache wenye ajenda zao wanajifanya tena kuzungumzia jamii nzima ya waislamu! Kwa nini basi wasiwataje majina ( asante dada Asha) kama si unafik na kujaribu kupanda chuki baina ya waumini wa dini hizi?
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Binafsi nasikitishwa sana na mgogoro wa Manji na Mengi kuchukua sura ya kidini. Mengi amekuwa akitoa misaada bila kujali dini ya mtu wala rangi yake. Na yeye anakiri kwamba biashara zake na za Manji huwa haziendani kabisa. Ninavyojua mimi, ni matangazo haya haya ya kondomu yanayozalisha pesa ambazo Mengi anawapa hawa Waislamu na watu wengine kama misaada, na huwa hawazikatai kwamba zinatokana na matangazo ya kondomu na pombe!
  Huu ni unafiki.
  Huwa anawakaribisha futari Waislamu wakati wa mfungo, futari ambayo inatokana na pesa za kondomu na pombe, huwa hawakatai!
  Iweje leo?
  Nawasilisha!
   
 8. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  mtu unaposimama na kuongea fikiria kwanza unasema nini na ni kwa nini unasema unachokisema. Tangu lini watz tukaweza kususia jambo kwa upamoja watu wana shida zao za kuwatosha badala ya mtu kuwaelezea mambo yatakayowasaidia katika maisha yao unawaongezea mamtatizo zaidi.
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Nathani hapo tatizo ndipo hasa lilipo..!!
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inachekesha sana kuona kuna wastu tayari walikwisha dakia mpira na kuanza kuwalaumu Waislaam wote wakati kichwa cha habari hakizungumzi dini ya mhusika..
  Tayari wamekwisha shika ngao za kujikinga wakati ukisoma vizuri maelezo yote utagundua kuwa ni mbinu ya uchonganishi ambayo imetungwa ama kuandikwa na mshaiki wa upande wa mshitaka...
  Jambo amalo linanifanya nijiulize yeye alikuwahapo mkutnoni kama nani?.. na aliweza vipi kujipenyeza hata kutka na habari nzito zinazowahusu viongozi wa kiisaam ambao tena inadaiwa ktk habari hiyo hiyo kuwa Uislaam umekosa viongozi bora..
  Upuuzi mtupu!... amkeni mliolala.....
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yeboyebo utaniwia radhi hili kosa umekuwa ukilifanya mara kwa mara the word is nadhani
   
 12. M

  Major JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2008
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi utawala unapokuwa legelege mambo mengi ya kipuuzi huwa yanaibuka na hii inanikumbusha ule utawala wa mzee Ruksa maana kila siku mbwa walikuwa wanajazana misikitini.mbona wakati wa mzee ben mambo kama haya hayakutokea?shame on you J
   
 13. s

  sumar Member

  #13
  Oct 1, 2008
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mambo yataharibika. Naomba ufafanuzi kuhusu "mbwa kujazana misikitini." Hakika sijaelewa vizuri. Jazba linanipanda, hasira zinani kolea. Hebu tuelimishe kabla hatujapasuka.This is serious- very serious.
   
 14. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Inaonekana Watuhumiwa wa Ufisadi wote vita ikiwa kali hukuimbilia nyumba za Ibada ili kupata faraja.
   
 15. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2008
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watanzania tusipokuwa makini na hawa watu, nachelea kusema mafisadi lakini naamini walioanzisha na kueneza hizi chokochoko ni mafisadi watatufikisha kwenye hali iliyotokea Rwanda 1994. Ukiangalia haya mambo yalivyokaa watajidai kujikita kwenye imani za kidini na kutokana na ulimbukeni wa baadhi ya watu wataamini kweli kuwa ni wenzao kiimani na wataanza kushabikia ujinga na ushetani wao. Wakitoka kwenye dini wataanza kupenyeza ukabila na katika hilo watu wasipokuwa makini utatokea mgawanyiko mkubwa baina ya wananchi.

  Hawa watu naomba tusiwaruhusu waendelee kupandikiza mbegu ya chuki kati yetu. Naamini hata anayofanya Mtikila kwa sasa ni matokeo ya mikakati ya uovu inayofanywa na mafisadi. Wanaiba rasilimali zetu kwa ujanja wa hali ya juu na pale wanapohisi kuwa tunawashtukia wanatafuta mbinu ya kutugawa ili tusiweze kuuliza japo kwa kuwapigia kelele. Nakumbuka kuna wakati majambazi yalipora mamilioni ya fedha na pale wananchi walipoanza kuyafukuza wao walikimbia na kuanza kumwaga fedha nyingi na wengi kati ya wale waliokuwa wanawafukuza walipumbazika na kuanza kugombea zile hela zilizomwagwa na kusahau kuwa azma yao kuwa ilikuwa ni kukamata yale majambazi.
  TUWE MAKINI WATANZANIA, TUSISAHAU YALE TUNAYOPASWA KUFANYA KWA KUDANGANYWA NA VITU VIDOGOVIDOGO.
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Oct 3, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi mnawaona waislamu mazezeta kiasi kwamba wakiambiwa wagomee bidhaa basi watagomea tu ili mradi watu wamesema kukidhi matakwa yao?Hivi mnadhani waislamu hawana elimu?haya basi hawana elimu hata common sense hawana?Mie sidhani kama Waislam watakubaliana na hoja zisizo na mshiko mimi nikiwa mmoja wao!siwezi kukubali mafisadi waliingize suala la ufisadi kwenye nyumba za kuabudia! Alhamdullilah wametumia Redio na sio Msikiti maana ingenisikitisha sana. Ila napenda kuwataadharisha wanaJF wenzangu kuwa Waislam Alhamdullilah hatuna ujuha!Tuna uwezo wa kujiuliza sisi si kama wale wanaoambiwa kubadilika kwa imani tukafata hatuwezi kuwa kama wafuasi wa kibwetere wala Sabato Masalia.

  Shukran.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Very skeptical..

  Waislamu majuha wako wengi tuu, tena nawafahamu kwa majina na wengi tu wakumwaga..Na hapa JF weengi ni majuha pia..Hao wafuasi wa kibwetere wana afadhali sana tena sana kwani they caused harm to themselves, lakini majuha wakiislamu they make sure people fro other beliefs die for their 'good' religion.

  Now what is worse?

  Need I continue?
   
Loading...