Sis tunafata maagizo! Musa alivyoambiwa avue viatu sio kwamba wakristo wote tuvur viatu! Yani kiufupi unataka tuwafate mnavyoamaini au?
Ni hivi Kutoka 3:5 Mungu alimwambia Musa
"Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguni mwako; maana mahali hapo ushikapo ni ardhi takatifu.’’
Sababu kwanini hatuvui viatu kanisani linatokana na tofauti ya mazingira, agano na kusudi.
Katika Agano la Kale, Mungu alizungumza na watu kwa njia za moja kwa moja sana (kama kwa Musa), na alionesha utakatifu Wake kwa alama za nje kama moto, moshi, kuvaa mavazi fulani, na kuvua viatu..
Lakini katika Agano Jipya, Mungu anakaa ndani yetu kwa Roho Mtakatifu.
1 Wakorintho 3:16
"Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?"
Agano la Kale lilifanyika kwenye mazingira ya Kiyahudi na Mashariki ya Kati ambako kuvua viatu ilikuwa ishara ya heshima. Katika tamaduni zingine (kama za Afrika au Ulaya), heshima huonyeshwa kwa njia tofauti — kimavazi, kimoyo, kimtindo.
Lengo ni moyo wa ibada, si viatu kama unavyodai wewe hapo Yesu mwenyewe alisema kuwa “Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.”(Mathayo 15:8)
Kwa hiyo, heshima ya kweli kwa Mungu si tu kwa kuvua viatu, bali moyo wa unyenyekevu na utakatifu ndani.
Unaweza ukawa unavua sana viatu, unasali usiku na mchana lakini moyoni mwako kumejaa chuki na visasi, Mungu hakai katika hekalu na namna hii mwisho wa siku unaishia kuwafurahisha wanadamu na si Mungu!