Hii ndiyo shida inayojitokeza unapoona suala hili kwa jicho moja badala ya yote mawili. Mauaji haya sio ya kushabikia hata kidogo. Na hayakuaanza jana bali yalianza siku nyingi. Mauaji yalianza mara mapinduzi yalipofanyika, kwa wale ambao sio wavivu wa kusoma habari za kimataifa wanajua hili siku nyingi kuwa Muslims are killing christians in CAR but nobody cared kwa sababu CAR is a failed state like Somalia. Wafaransa wakaingilia kati kama washirika wa CAR, tukumbuke hili ni koloni lao, pia UN ikastep in, wakati haya yakifanyika Christians nao wakawa wanajimobilize maana walikuwa wanachinjwa kama kuku mitaani, visasi vikaanza. Mambo sasa yamekuwa mazito kwa wale walioanza mauaji, naona sasa wengine ndiyo mnakuja hapa kuwa akina fulani wanauawa, mauaji yalianza siku nyingi.
Cha muhimu tujiulize sisi tuna fanya nini ili kukabiliana na mauaji ya reja reja yanayotokea nchini kwetu, kwa wale waliosahau nawakumbusha kuwa watu wengi wamekufa Kilosa, Mvomero, Ulanga, Kiteto na sehemu nyingine za nchi. Tumefanye nini kukomesha hiyo migogoro inayoleta hiyo rabsha, au tumebaki na wagalatia bana!!!!!!!! MWENYE UFAHAMU NA AFAHAMU