Waislam wauawa kinyama huko Bangue-C.A.R

Waislam wauawa kinyama huko Bangue-C.A.R

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo, nao ni Magaidi au kwa kuwa ni wakristo jina linabadilika!
Mkuu hao wote ni magaidi. Tatizo ni ardhi, hao watu walikuwa wakiishi kwa Amani ila wageni kutoka Chad na Sudan wakaanza kuwafanya kama Janjaweed wanavyofanya.

Wote wamekosea kwa sababu ardhi ipo duniani ya kutosha tu, wafikirie kabla ya kuamua.
 
Kwa hiyo, nao ni Magaidi au kwa kuwa ni wakristo jina linabadilika!
Wala sio magaidi, hao ni wananchi wenye hasira wameingia mitaani kuwasaka waisilamu nyumba hadi nyumba, wala hawahitaji kupanga mipango ya kigaidi kwa mwezi mzima au mwaka mzima, na wala hawajifichi. Magaidi wanajificha na wanapanga mikakati yao kwa siri. Hao naweza kuwafananisha na wafugaji vs wakulima hapa nchini, kwani nao utawaita magaidi? Wanaingia village kumsaka mkulima au mfugaji waziwazi
 
Magaidi hua ni waisilamu tu wakristo wenyewe wakiuwa hua wanaitwa wanamapinduzi.... tena watatetewa mno.

Ndio ninaposhangaa! Mkuu ungeona zile video za watoto na akina mama wa kiislamu walivyouawa, ingekuwa wamefanya waislamu, vyombo vyote vitoa habari hiyo front page,"Magaidi waua tena," Lakini waliouliwa ni waislamu na wauaji ni wakristo unaambiwa eti wanalipa kisasi! Sio magaidi! Kwa hiyo na wale wa Westgate nao walilipa kisasi basi!
 
Mkuu hao wote ni magaidi. Tatizo ni ardhi, hao watu walikuwa wakiishi kwa Amani ila wageni kutoka Chad na Sudan wakaanza kuwafanya kama Janjaweed wanavyofanya.

Wote wamekosea kwa sababu ardhi ipo duniani ya kutosha tu, wafikirie kabla ya kuamua.

Hapo sawa mkuu.
 
Wala sio magaidi, hao ni wananchi wenye hasira wameingia mitaani kuwasaka waisilamu nyumba hadi nyumba, wala hawahitaji kupanga mipango ya kigaidi kwa mwezi mzima au mwaka mzima, na wala hawajifichi. Magaidi wanajificha na wanapanga mikakati yao kwa siri. Hao naweza kuwafananisha na wafugaji vs wakulima hapa nchini, kwani nao utawaita magaidi? Wanaingia village kumsaka mkulima au mfugaji waziwazi

Mkuu, umeonyesha wazi kwamba wewe umependezwa sana na jambo hili! Yaani wanaoendesha mauaji dhidi ya waislamu ni wakristo we unasema ni wananchi wenye hasira kali! Maajabu! Nipe tafsiri ya neno gaidi.
 
Hao sii wakristo kama umefuatilia vizuri huo ugonvi unawahusisha wapagani. Maana wamevaa hirizi mwili mzima sasa hayo mabo ya hirizi kwenye ukristo hayapo.Sii imani ya kikristo kuua na biblia imekataza kwenye kitabu cha kutoka kuua pamoja na kulipiza kisasa
 
Mkuu, ukweli unauma, wakristo hamlipendi jina la ugaidi!
 
Tuacheni Ushabiki wa kidini, Vita havina Macho na havina tumuombe Mungu atuepushie Balaa hili
 
kimsingi waislamu ndiyo walianza kuwauwa wakristo na kukosekana serikali madhubuti kudhibiti uovu huo, umepelekea maumivu makubwa kwao na hivyo kujihami.

Jambo la kujifunza ni umuhimu wa serikali kudhibiti chokochoko zozote za kidini, ili kujenge msingi wa kuamianiana na kuitunza amani.
 
Kwa sisi wabongo misingi mizuri na imara ya undugu bila kujali udini Naomba Mwenyezimungu azidi kutuepusha na dhahama kama hilo
 
Wangekuwa waislamu wanawaua wakristo, Marekani wangepeleka bomu kuwauwa na wangeitwa magaidi, sasa hawa wakristo na sio magaidi sasa?

We ulikuwa wapi kukemea kipindi waislam wanawaua wakristo, mbona ulikakaa kimya? Leo kibao kimegeuka mbio unakuja na topic yako hii... Siwatetei ila wanapaswa kuwaonyesha adabu kidogo maana Waislam wanajifanyaga wao ndo wenye hasira na kuwaua watu wenye imani tofauti... Acha waone uchungu ni jinsi gani inauma ndugu yako akiuawa.
 
Mentality ipi hiyo mkuu?

soma historia vizuri,,,wakati wanamgambo wa seleka wanawaua wakristo mbona hukuja kulalama hapa jamvini? acha kukurupuka,,huo ni udini kwa sababu wanaouawa sasa hivi ni waislamu ndio unalalamika,,,hao wakristo waliokuwa wanauawa zamani na hao waislamu hawakuwa watu?
 
Wangekuwa waislamu wanawaua wakristo, Marekani wangepeleka bomu kuwauwa na wangeitwa magaidi, sasa hawa wakristo na sio magaidi sasa?

Marekani inaingiaje ktk hili? Au umesahau Saudi, Qatar na Iran nao inapeleka mabumu Syria kuua Waislam?
 
Mkuu, ukweli unauma, wakristo hamlipendi jina la ugaidi!

Jambazi au kikundi kile cha wale vijana hivi karibuni walikuwa wakivamia nyumba za watu(looting & terrorising) na hata kubaka hapa Dar wakivamia nyumba yangu na mimi nika retaliate na kuanza kuwafuatilia kwa dhumuni la kulipiza kisasi kwa hasira mimi pamoja na waathirika(victims) wenzangu wote. Mr Ralphryder Utaniita mimi jambazi au mbakaji??? You are missing a point Mkuu!! tuache ushabiki wa kidini, lets all come clean na kama sio wenye siasa kali kuanza kuwaua wenzao wenye dini tofauti yanayotokea sasa yangeepukika mkuu! ni kama paka ukijifungia nae chumbani na kumchapa au kumtesa naye atachoka na kufight back! Ni muda sasa wa kuishi kama ndugu na sio kujifanya wababe na kuwaona wanaoamini na kufuata dini nyengine kuwa kama maadui au hawastahili kuishi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom