Kama kweli cdm wanakosa kwenye hili basi dua itawadhuru lakini kama sio na iwadhuru masheikh watakao omba hiyo dua
Hakuna kitu hapa, tusidanganyane. Ndugu zangu Waislam kweli kuna haja ya kuwa makini ktk matamko yenu. Mtaifanya imani hii kushakiwa na waumini wenu na hata wenye mapenzi mema na Uislamu. Mi si mwislamu lkn nina mapenzi mema na Uislamu. Ninaanza kupata picha halisi ya kile ambacho sipendi kukisikia kutoka kwa waislamu hasa hili la kutoa tamko za ajabu.
Mungu si Abdallah wala Veronika. Tukumbuke hilo na wala tusijisahau kiasi hicho cha kuendekeza njaa za matumbo na akili zetu. Waislamu ndio wanaamka kutoka kwenye usingizi pono baada ya huyu mama mnafiki kushughulikiwa na vijana wa CHADEMA. Kama kosa ni kuvulishwa hijabu ambacho kinaelezwa kuwa si hijabu basi mjaribu kutafuta namna mwafaka ya kuuelezea chulizo hilo.
Msipoteze muda wenu kwenye vitisho vya kishenzi, havitasaidia hata kidogo. Ni mara ngapi wanawake wanadhalilishwa na serikali ya CCM? Waislamu mlikuwa mmelala wapi? Na sasa kipi kimewaamsha kutoka usingizini. Imani si siasa na kama mna haja ya siasa basi mkisajili chombo chenu hicho kiwe chama cha siasa.
Ni jambo la ajabu kwa kikundi cha dini kuwashawishi watz na waumini wake kukichagua chama fulani cha siasa. Tz si Iran au Saudia au Vatican ambacho serikali ni ya kidini au karibu raia wote ni watu wa imani fulani. Mnaleta haya Tz mkiwa mnataka kuifanya Tz iwe nchi ya kiislamu? Njaa ni mdudu mbaya sana. Tupelekeni watoto wetu wapate elimu bora ili tuondokane na hizi fikra za kijinga.
Kweli kama CHADEMA nao wataingia kwenye mtego huu mchafu wa kuanza kuomba msamaha kwa hili kundi la watu njaa, wakoram; itakuwa heri kutoswa maana Watz wanaona kinachoendelea na ni kwa kiasi gani kosa limefanyika. Hakuna kosa lolote hapa maana haya ni mazingira ya kisiasa na kila mmoja alikuwa anatimiza wajibu wake wa kisiasa na hata huyu Fatuma naye alikuwa anatumia vibaya wajibu wake wa kisiasa.
Sasa kama haya mambo yametokea ktk mazingira ya kisiasa kwanini mahakama isifanye wajibu wake kama ilivyotafsiriwa ktk katiba ya nchi? Sasa waislamu wanahusika vipi hapa au nikujipendekeza tu ili mradi waonekane wao wana dini babu kubwa. Na kila dini ikianza kufanya kazi ya kutafsiri katiba tutafika wapi?
CHADEMA achaneni kujibizana na vikundi vya kihuni, fanyeni kazi zenu. Ni usaliti wa namna ile ile ambao hata wakati wa ukombozi kuna watz waliokuwa wanapata neema kutoka kwa wakoloni walikuwa wanaona hakuna haja ya kudai uhuru wetu kwa sababu tu watakosa kile chao kidogo wanachokipata kwa kuwa kama matarishi au maboyi ligiligi, wafagizi, wahudumu wa vyoo vya kizungu, wapishi n.k.
Waislamu na Wakristo: Bora tukawekeza kwenye elimu kwa faida ya watoto wetu. Achana na siasa hizi za akina CCM na CDM. Maana hazitasaidia bali zitatupumbaza na tukaonekana mizoba, mitumba, pumba nk.
Chukua tahadhari na watu wa namna hii ni hatari kabisa kwa mukhstakabali wa nchi yetu.
''Ashakum si matusi''