Wahuni wananikosesha usingizi

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Ni muda mfupi sana toka nimehamia huu mtaa, ila nimeshapachoka tayari,,, nyumba ya pili toka hapa ninapokaa kuna studio ya kurekodia muziki huu wa bongo fleva, sasa hapa kuna vijana masaa 24 wapo tu, wanapiga sanaa kelele.

Muda wote wanaimba kwa makelele ya juu alaf sasa hawaangalii ni muda gani, kwao saa nane za usiku ni sawa tu na saa saba mchana, mbaya zaidi wanaimba ujinga ujinga sanaa, sasa mpaka unawaza mbona mtaa mzima hakuna anaekwazika na maudhi haya, au mtaa mzima wamekulia mazingira haya? like no body business.

Wakazi wa hapa sijui wamekwishazoea hali hii au hawa ni vijana wao kwaio wanachukulia mambo kwa uzito mwepesi tu? Maana ni usiku kucha unaskia watu wanaimba kama wehu hasa ule muziki sijui ndio singeli huo unakela kuliko jambo lolote, na hapa wala sio hata uswahilini labda niseme kawaida yao.

Jamani nani kakiroga kizazi hiki? Yaani nchi nzima kila kijana ni msanii wa bongo fleva? Hili ndio taifa la kesho vichwa vya kuku madebe matupu, kwaio miaka ijayo hapa kwetu tutakua na rais mvaa jeans za kuchanika magotini na baraza la mawaziri wanyoa viduku.
 
pole mkuu,hiyo ndio DAR!
 
studio si zinakuaga na sound proof ambaye haitoki njeee... au hao wanaiimbia nje ya studio
 
Wakati nakuja Dar Slum miaka ya 2005 nilikuwa nakaa Magomeni! Basi makelele ya mziki kwenye Bar au mitaani kukiwa na shughuli usiku kucha hamlali. Na bahati mbaya sana watu wa uswazi wanapenda kupiga nyimbo ambazo kiukweli zinakarahisha watu wastaarabu! Baada ya muda nilizoea tu ila baada ya mwaka nilihama...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom