Wahuni wananikosesha usingizi

Ni muda mfupi sana toka nimehamia huu mtaa, ila nimeshapachoka tayari,,, nyumba ya pili toka hapa ninapokaa kuna studio ya kurekodia muziki huu wa bongo fleva, sasa hapa kuna vijana masaa 24 wapo tu, wanapiga sanaa kelele.

Muda wote wanaimba kwa makelele ya juu alaf sasa hawaangalii ni muda gani, kwao saa nane za usiku ni sawa tu na saa saba mchana, mbaya zaidi wanaimba ujinga ujinga sanaa, sasa mpaka unawaza mbona mtaa mzima hakuna anaekwazika na maudhi haya, au mtaa mzima wamekulia mazingira haya? like no body business.

Wakazi wa hapa sijui wamekwishazoea hali hii au hawa ni vijana wao kwaio wanachukulia mambo kwa uzito mwepesi tu? Maana ni usiku kucha unaskia watu wanaimba kama wehu hasa ule muziki sijui ndio singeli huo unakela kuliko jambo lolote, na hapa wala sio hata uswahilini labda niseme kawaida yao.

Jamani nani kakiroga kizazi hiki? Yaani nchi nzima kila kijana ni msanii wa bongo fleva? Hili ndio taifa la kesho vichwa vya kuku madebe matupu, kwaio miaka ijayo hapa kwetu tutakua na rais mvaa jeans za kuchanika magotini na baraza la mawaziri wanyoa viduku.
Huo ni mtaa gani? Sehemu gani kwa dar labda? Ushauri: tafuta 20000/=, tafuta lile gari la polisi la patrol, ongea na mkubwa wao kuhusu hilo tatizo, mpe hiyo hela ya kubrashi viatu, then utakuja kutupa mrejesho kama bado hao wahuni wapo. Serikali ya mtaa uliohamia ushawapa malalamiko? Kama bado fanya hivyo kwanza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom