NGAYANIMO
Member
- Feb 17, 2026
- 43
- 58
Ukwaju wa kitambo
Leo nimebahatika kukutana na msanii Kigwema Bosco kwa jina Maarufu anafahamika kama kigwema. Ni msanii wa zamani wa Bongo Fleva. Naimani unatamkumbuka kwa ngoma kali kama Vile Binti Skendo na Ngoma nyingine inaitwa " Sitomsahau ft Marlaw,".Nimekaa naye akanisimulia safari yake yote kimuziki Toka enzi hizo wakati anaanza Game. Hii hapa historia yake.
Kwa Naitwa Kigwema Bosco, maarufu kama Kigwema Hii ni safari yangu.
"SAFARI YANGU YA MUZIKI: KUTOKA MTONI MPAKA JUKWAANI"
Hivi unafahamu ni Kwa Nini Nilichagua Muziki:
"Kilichonifanya niwe msanii ( Mwanamuziki) wakati ule ni tabia yangu ya kupenda kusaidia watu kwa kuwashauri. Nikajiuliza: Je? Ni wapi nitaweza kufikisha maoni yangu na ushauri wangu kwa watu wengi zaidi? Jibu likawa muziki.
Hapo ndipo nilipoanzia safari ya utunzi. Nilianza kwa kuandika hadithi magazetini chini ya mwandishi Nguli Enzi anaitwa "Seif Amran" kwenye Upande wa Umri kiukweli sikumbuki vizuri, ila ilikuwa kama vile mwaka 1997 nikiwa form one. Kutoka kuandika hadithi, Ndipo nikaingia kwenye kuandika mashairi, na hatimaye nikagundua muziki ndio chombo kamili cha kufikisha ujumbe kwa jamii kwa njia rahisi.
Mwanzo wa Safari:
Nilitembea Kwa Miguu Kuelekea Ndoto:
Safari haikuwa rahisi. Kikwazo kikubwa kilikuwa ukosefu wa fedha za kurekodi. Ilifikia hatua Nenda studio kuomba nafasi ya kurekodi. Safari za matamasha nazo zilikuwa ngumu – nilitembea kwa miguu. Na Kumbuka siku moja Niliweza kutembea kwa Miguu kutoka Mtoni kwa Azizi Ali, Temeke Hadi Kinondoni Club Asset Enzi ama zamani palijulikana kama FM Club. Yote haya nilifanya kwa mapenzi ili tu Nami siku moja nipate nafasi jukwaani na nionekane, wakati huo huo mapromota pamoja na wadau wengine walikuwa wanakuja na magari kwenye kilinge cha J-MOS.
Njia Nilizotumia Kujikwamua :
Mlango ulifunguka kupitia mdogo wangu ambaye alikuwa na urafiki wa karibu na djs & promota JD - John Dilinga. Nilimuomba aniunganishe naye. Wakati huo nilikuwa Tayari nipo chini ya Recording lebo inafahamika kwa jina la Baucha nilihipata baada ya kushinda shindano la kuimba, lakini haikunipa chochote cha maana.
Ndipo nikaamua kuachana nayo rasmi na kuanza kujitegemea. JD hakika alinisaidia sana – si kwa fedha, bali kwa Namna ya kipekee alinielekeza namna ya kuwa rapa bora na kunipigia Promo kwenye event mbalimbali mtaani dj jd alifanya hivyo pale anapopata chance ya kuhost kama dj sehemu mbalimbali kwa kucheza wimbo wangu.
Hatua ya Mabadiliko: Remix ya "Niite Basi"
Kwa kuwa nilikuwa na ukaribu na Crew ya Wakali Kwanza ilikuwa hivi Baada ya msanii Joslin kutoa wimbo wake unaoitwa "Niite Basi" Na kufanya vizuri, nilichofanya nikamuomba niufanye remix wimbo ule na joselin alikubalia. Shida ikawa ni moja tu je? Nitaweza kupata beat ya chorus. Hapo JD akafanya utaalamu wake akaniletea beat, nikaitungia mistari. Aliposikia alishangaa Sana.
Bahati nzuri kipindi hicho alikuwa anaandaa show ya Eid mji kasoro Bahari Morogoro, jd akaniunganisha na mimi. Akalimbia gharama za studio pale kwenye studio za "Sey Records" Ili niweze kuingiza Sauti kwenye ile beat ya chorus. Huo ukawa mwanzo wangu mzuri. Kwenye ile show Joslin alikuwepo na akataka tupafomu wote. Tangu hapo nikawa kama mmoja wa members kwenye crew ya "Wakali Kwanza.
Mafanikio na Ngoma Zilizonigusa:
Ngoma iliyobadilisha maisha yangu ni Ngoma inaitwa "SITOMSAHAU ft Marlaw" Lakini ngoma niliyoipenda zaidi Toka moyoni mwangu ni BINTI SKENDO
Sikuachana na muziki, ila nilishindwa ku-balance majukumu ya kimaisha na sanaa yangu.
Matukio Nisiyosahau:
Moyo wangu bado unamkumbuka shabiki aliyenituza hela jukwaani kidogo kidogo hadi zikafika kiasi cha tsh laki 2. Alikuwa analia kila nikiurudia wimbo wa SITOMSAHAU. Akafikia hatua ya shabiki huyo kukosa hata nauli ya kurudi kwa sababu alinitunza fedha zake mimi.
Halafu kichekesho kingine ni show moja ilifanyika Tarime nikiwa na marehemu msanii Side Boy. Yule jamaa alikuwa muoga sana jukwaanj . Alikuwa anaimba huku anatetemeka, akajikuta anaimba karibu masaa 2 anaogopa kuwaambia inatosha. Akawa anarudiarudia tu 😀
Masomo Niliyopata
Kwa msanii anayeanza, ushauri wangu ni huu: usiwahi kuanzisha familia kabla ya kuona mwelekeo wa sanaa yako.
Na kama muda ungerudi nyuma, ningebadilisha management yangu kimuziki. Nilipata management isiyokuwa na uelewa wowote wa muziki, hivyo nilifeli. JD hakuwa manager wangu, alinipush tu. Alipotoka Radio Uhuru hatukuwa tunaonana tena. Hadi kile kipindi nafanya ngoma na Marlow na kuiachia Hewani , nilikuwa mbali na wala sikuwa na management.
Chanzo cha Moto: Mfano Wangu wa Kuigwa:
Katikati ya mapambano yote, kilichonipa nguvu ya kuendelea alikuwa ni msanii Solo Thong" Tangu mwanzo alikuwa mfano wangu mkubwa kwenye game. Nilimwamini na nilitaka kufuata nyayo zake. Ndiye aliyenipa imani kwamba hata kama unatokea mbali, ukipambana unafika.
Hadi Leo: Safari Inaendelea
Ningependa nikumbukwe kama mpambanaji wa sanaa Kwa matukio niliyofanya kama kutwaa Tuzo ya Kili, na pia kwa kuwa msanii nisiyependwa na radio fulani kubwa wakati ule.
Leo hii furaha yangu kubwa ni familia yangu Nina watoto 5 na hilo ndilo kitu ninalofurahia zaidi.
Lakini safari haijaishia hapa. Kalamu bado inayo wino, na kichwani bado kina mistari. Mungu akijaalia, mtasikia tena Ngoma kutoka kwangu. Kaa karibu...
UKWAJU WA KITAMBO
kwa story kama hizi ndio zinatuonesha muziki wa Bongo umetoka mbali. Kama umeguswa na historia ya Kigwema LiKE page hii, SHARE post, na endelea kufuatilia bado tunawapa Elimu kuhusu sanaa na kumbukumbu za wasanii wengi wa zamani.