Wahuni siyo watu wazuri

dawa yenu

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
2,822
3,650
Wahuni sio watu. Wengi hudhani huu ni msemo tu kama ilivyo "usinifokee" au msemo huu mpya ulioibuka jana mishale ya saa mbili usiku wa "usinitetemeshe!" Tofauti na misemo hiyo mingine, wahuni sio watu ni uhalisia wa maisha. Wahuni sio watu ni funzo, hili ni somo ambalo nasikitika nilichelewa Sana kulijua.

Ulimwengu ulinifunza somo hili kikatili Sana, sitakuja kusahau! Ndani ya jiji la Dar es salaam, enzi hizo bado naitwa wa kusoma! Nakumbuka ilikuwa siku ya ijumaa, siku ya michezo au tuite siku ya football maana ndio mchezo pekee uliokuwa ukifanyika pale shule. Sisi ambao hatukuwa wachezaji tuliutumia muda huu kupiga soga, pia ulikuwa muda mzuri Sana wa kutongozana! Ijumaa ilikuwa ijumaa kweli, bora uumwe siku zote ila sio ijumaa! Baadhi ya walimu na wanafunzi kwa umoja wetu tulifeli maadili!

Siku hiyo nilikuwa na wanangu pembeni ya uwanja tunapiga soga huku tukifurahia soka la kiwango, ghafla nikaguswa bega. Alikuwa Grace, ingekuwa zama hizi basi tungemuita Hamisa Mobetto wa shule! Binti maringo, mvuto wa sura yake Kama Angeline Jolie ila tabia yake inatisha kuliko Masoud sura mbaya! Sauti yake tamu utadhani Zuhra Yunus wa BBC, maneno machafu kama Gigy Money! Grace alikuwa msafi hatari, anachana nywele zake vizuri maana humo ndimo kahifadhia ujinga wake!

Akaniomba nimsindikize sehemu! Sauti yake ya kumtoa nyoka pangoni ikazipumbaza akili zangu, moyo wangu ukapoteza utulivu. Siwezi kumkatalia Grace, halafu hata nikimkatalia ataondoka na mwingine moyo utaniuma! Golden chance never come twice. Bila ajizi nikawaaga washkaji na kuanza kumsindikiza Grace bila hata kuhoji tunaenda wapi.

Mitaa miwili mbele Grace akanishika mkono, nikasisimka mwili na nafsi! Akanishika begani, tukaanza kutembea kimahaba na uniform zetu hofu hatuna! Kuna sehemu tukapita kuna wajuba wawili wakatoka kwenye jumba bovu huku wanavuta bangi wakatusimamisha. Swali la kwanza waliloniuliza ni kwanini naleta dharau!

Waliuliza kibabe na Mimi siwezi kuwa mnyonge mbele ya Grace. Nikauliza kibabe, "dharau nimeleta wapi?" Kumbe ndio lilikuwa kosa langu aisee! Jamaa mmoja akanisukuma nusu nianguke. Bahati nzuri hili tukio kuna jamaa yangu aliliona akaja pale ametuna Kama Simba, liwalo na liwe hawezi kukubali mwanae nizinguliwe kibwege mbele yake.

Nilipoona nimepata msaada halafu nikicheki pembeni mtoto Grace Kama anataka nifanye jambo hivi basi nikajikuta Shah ruh Khan pale. Nikasimama kibabe sana nikamchagua ninayemmudu nikamsukuma akaangukia mtaroni. Sijui kilitokea nini ila ghafla Mimi na jamaa yangu tulijikuta tumezungukwa na washkaji Kama sita hivi, nyuso zao zimejaa shari, wanatembea bega moja juu jingine chini, suruali wamekunja mguu mmoja! Wamekomaa viungo vya mwili, Wana makovu, hawajipendi, wamechoka na maisha na dhahiri Wamejaa chuki na hasira dhidi yetu! Jamaa yangu Kama kishada vile akatoka nduki pale nikabaki Mimi na Hamisa Mobetto wangu tunasubiri hukumu yetu mbele ya hakimu mkazi Kisutu!

Wakanishtaki kwa kosa la kumchukua demu wao halafu kwenda kuleta dharau maskani kwao. Dooh... ndio nikajua Kumbe Kuna mwamba pale ametoka kupewa kibuti na Hamissa Mobetto wetu! Halafu jamaa mwenyewe anaonekana anapenda ugomvi kuliko kula. Nikawa mdogo kama piriton. Watanifanya nini Hawa wajuba? Kumbe Grace alisema nimsindikize huku ili aje kumlingishia mtalaka wake kuwa maisha yanamuendea vyema amenipata mpenzi mpya! Khaa!!! Mobetto kanileta machinjioni, nachinjwa bila dua wala kuelekezwa Kibra!

Kabla hukumu haijasomwa yote likatokea kundi la washkaji zangu wote waliokuwa uwanjani wanacheza mpira. Kumbe jamaa yangu alikimbia kwenda kuwatonya kuwa wakichelewa basi nitafanywa asusa na watakuta mifupa tu! Walipofika pale bila maelezo kilichofuata ni timbwili, patashika, shika nikushike, huyu jiwe huyu fimbo, huyu nondo huyu tofali, yaani kazi kazi, Vita ni vita, show ya kibabe wale wajuba wakakimbia maana waliona roho zao zipo rehani.

Grace a.k.a Cleopatra wa shule msababisha dhahama akawa ananifuta vumbi huku anasifu ujasiri wangu eti alijua tu wale wahuni hawaniwezi, muda huo Mimi nipo kimya tu nafurahi moyoni yaani najiona kama Angelo wa kwenye The promice nipo Yna wangu.

Niliponyanyua uso nikaona vumbi kwa mbaaaaali linakuja kasi. Kabla sijajua ni nini nikakoswa koswa na tofali la uso, ghafla watu wote wakaanza kukimbia! Kumbe wale wajuba walienda kuita jeshi lao, jeshi la kisasi. Kwa mara ya kwanza nilimuona Israeli right before my eyes!
Ghafla Nikawa Usain Bolt, nikafunga mota miguuni sijawahi kukimbia Kama siku ile huku mvua ya mawe inanikosa kosa.

Nikakata kona ya kwanza huku nyuma nasikia vishindo vya jeshi la wajuba, Wamebeba siraha za jadi za kila aina! Nikajua hapa siponi nikaingia bila hodi kwenye nyumba moja ilikuwa mlango wazi, nikafunga mlango! Humo ndani kulikuwa na wamama wawili wanakula, waliponiona tu wakajua Kuna shari bahati nzuri hawakunifukuza. Jeshi la wajuba likapita nje na kutokomea kusikojulikana kumbe windo lao nimefichwa ndani Kama mwanamwali wa kimakonde! Wale wamama wakasema nisubiri Hadi giza liingie ndio niondoke.

Ndio wale wamama wakaniambia wale wajuba wanajiita WATALEBANI. Kikundi chao kimepinda mbaya! Wamejikita zaidi kwenye shughuli za uvuta wa bangi pia ni wakabaji wabobezi! Wanavuta mmea Kama hawana akili nzuri. Wanapiga chuma kujiweka fiti kimsingi wamejipanga, wapo vizuri. Na polisi wapo kimya ni Kama vile hawajui kinachoendelea. Wakaniambia Kikundi kingine kipo Mbagala kinajiita WAMAREKANI yaani wamefungua mabranch maeneo tofauti tofauti jijini Dar.

Giza lilipoingia nikaondoka. Nafika nyumbani ndio napata story kuwa baadhi ya wenzangu wamepigwa nondo wameumia vibaya wamepelekwa Amana! Nikavaa viatu vyao, nikaona vizito nikaachana navyo. Weekend ikapita kwa amani. Jumatatu nilipofika shule ndio nikapewa habari yangu kuwa WATALEBANI wameweka nadhiri kwamba popote watakaponipata Mimi na kivuruge wangu mamaa Mobetto herself watakachotufanya hajawahi kufanyiwa mtu yoyote Afrika Mashariki na Kati. Zilikuwa taarifa nzito kwangu na kwa demu wangu niliyemilikishwa ghafla bin vuu.

Muda wa kurudi nyumbani ulipofika FBI na CIB wa shule wakatuambia mimi na Grace tusiondoke maana WATALEBANI wameishona majambia wanasubiri sisi tu hapo uwanjani. Binafsi nilijihisi kuumwa UTI ya ghafla! Grace bado alikuwa ananiaminia Shah ruh Khan wake! Tulikaa shule hadi saa kumi na mbili ikabidi niende kwa headmaster nikamueleza huku nikifukia mashimo ili Grace asiwe hatiani. Head master akawaita polisi jamii wakatuchukua hadi nyumbani. Kwa wiki nzima Mimi na Grace tukawa Kama Chibu Dee na Zuchu tunalindwa na mabaunsa muda wa kwenda nyumbani. Sisi ndio sisi kama Romeo na Juliet.

Amani ilirejea baada ya wananchi wenye hasira Kali kuanza kujichukulia sheria mkononi. Nasikia kuna MTALEBANI alienda kufanya undava Sinza, eeh wajanja wa Sinza wakampiga kiberiti akawa jivu chap. Wakaanza kupigwa Moto back to back, WATALEBANI na washirika wao walishikwa pabaya wakaanza kuishi kwa hofu na mashaka roho mkononi na baada ya muda wakajibrand na kuanza kujiita PANYA ROAD, hili lilikuja kuwa tatizo kubwa sana. Nashukuru this time sikuwa target yao tena ila waliniachia funzo kuwa Hawa wote ni wahuni na WAHUNI SIO WATU.

Taratibu nikaanza kuona tabia mbaya za Mobetto wangu zinavumilika and actually sio mbaya kiviiiiiile, halafu alikuwa anajiona guilty kwa aliyonisababishia. End of the story tuliishia tu kupendana Sana ila maisha yalikuja kututenganisha! Mobetto wangu now ni mke wa mtu!

NB
Grace sio jina lake halisi
 
wanaume wanazaliwa sehemu moja, halafu kifo chao mara nyingi hubabishwa na kupenda sehemu walipo toka
 
Siku nyingine ukiwa na demu mtangulize mbele wewe kuja nyuma mdogomdogo kama hatua kadhaa...mkuu hiyo ni protokali hata kama ni mkeo, kuna siku utakuja kudanja kimasikhara tu,mi kabla ya kuijua hii miaka kadhaa nyuma kulikuwa na kidemu flani kilikuwa kinanishobokea kichizi yaani halafu mitaa yetu iko mbalimbali,

sasa tulikuwa na tabia moja hivi kalikuwa kanakuja gheto saa 9 au 10 hivi,tunapiga mambo yetu saa 12 au saa 1 hivi nakasindikiza hadi karibu na mitaa yao,sasa kuna siku hiyo ndo niliingia anga za masela mida ya saa 1 hivi usiku,nashangaa tu machizi wamenizunguka,

masela kama wanne hivi kwa hesabu za harakaharaka "oyaa we fala wapi na demu wetu"??""dah siku ile nilikula makofi mitama mixer ndosi za maana tu, hata kujitetea nilishindwa,pindi hiyo nilikuwa chalii tu halafu wale wahuni walikuwa mabraza yaan njemba...cha kunishangaza yule demu alikuwa ananitetea kwa kuwataja majina yao yaani walikuwa wanafahamiana..tokea siku washkaji wakanishauri nikiwa na demu nisitembee naye sambamba yan atangulie mbele halafu mi nije kwa nyuma mdogo mdogo
 
Siku nyingine ukiwa na demu mtangulize mbele wewe kuja nyuma mdogomdogo kama hatua kadhaa...mkuu hiyo ni protokali hata kama ni mkeo,kuna siku utakuja kudanja kimasikhara tu,mi kabla ya kuijua hii miaka kadhaa nyuma kulikuwa na kidemu flani kilikuwa kinanishobokea kichizi yaani halafu mitaa yetu iko mbalimbali,sasa tulikuwa na tabia moja hivi kalikuwa kanakuja gheto saa 9 au 10 hivi,tunapiga mambo yetu saa 12 au saa 1 hivi nakasindikiza hadi karibu na mitaa yao,sasa kuna siku hiyo ndo niliingia anga za masela mida ya saa 1 hivi usiku,nashangaa tu machizi wamenizunguka,masela kama wanne hivi kwa hesabu za harakaharaka "oyaa we fala wapi na demu wetu"??""dah siku ile nilikula makofi mitama mixer ndosi za maana tu,hata kujitetea nilishindwa,pindi hiyo nilikuwa chalii tu halafu wale wahuni walikuwa mabraza yaan njemba...cha kunishangaza yule demu alikuwa ananitetea kwa kuwataja majina yao yaani walikuwa wanafahamiana..tokea siku washkaji wakanishauri nikiwa na demu nisitembee naye sambamba yan atangulie mbele halafu mi nije kwa nyuma mdogo mdogo
Daah nimechelewa sana kuijua hii....
 
Dah! Hii mambo kitambo Jamaa yangu alichukua pikipiki ya baba yake bila kuomba tukaenda kuchota kwa Demu wake, tepaki njiani mahibfi yakiwa na mbelewele, tunabonga na Mtoto, yaani twajiona tupo juu sana, Mara nilipita KIPANDE cha Tofali katikati yetu vuuuuuu! *****, tulipoteana. Kila mmoja aliingia kwake. Day 2 tunaingia shule sec asubuhi kila moja hajui mwenzake ilikuwaje. Kumbe Jamaa alienda home akaja na broo wako kuchukua pikipiki usiku na waliikuta Uko vizuri tu. Yule Binti alienda sema kwa baba yake kuwa kaka zake walituvsmia sisi wkt tulienda pale kumpelekea material. Mzee alikuwa msure tu akasgiza ilindwe HD wenyewe waje. Kipindi hicho 1990s wansojua pikipiki hamna kabisa. Ingalikuwa sasa wasingeikuta
 
Back
Top Bottom