Bambanza jr.
JF-Expert Member
- Aug 6, 2011
- 355
- 36
naomba nikuambie una upeo mkubwa sana tatizo wengi hawatak ilo, plz ni pm jina lako na contacts zako!Kazi ziko nyingi sana kama utaamua kuvaa uso wa mbuzi, nitatoa mifano michache ya kazi za kujiajiri ambazo bado hazina wenyewe, kwa mfano ufugaji wa chura (tuna chura wazuri Mtwara for export),ziko pili pili mtama hapo Morogoro, kuna nyuki wasio uma hapo ktkt ya nchi hawana mtu,hapo Morogoro kuna samaki kafugeni,fungueni vituo vya huduma kwa watoto mitaani kwenu.
Kuna shule hazina walimu,kafundishe tuition,kila siku wanatangaza nafasi za Ma- VEO, mbona hamuombi. Moja ya matatizo ya ajira kuwa haba ni wote kubanana Dsm na miji mingine mikubwa, huku maporini tuliko wenzenu kazi ziko nyingi ajabu, hata vyeti havihitajiki huku vijijini, wewe njoo huku kijijini, anzia chini kisha upande kidogo kidogo.
Nina jamaa hapa wilayani alianza kama Revenue collector wa kata na sasa yuko halimashauri ndani ya muda mfupi, lakini alikubali kuanzia chini kabisa bila kujali vyeti vyake.