Wahitimu wa vyuo walioko mtaani

Kazi ziko nyingi sana kama utaamua kuvaa uso wa mbuzi, nitatoa mifano michache ya kazi za kujiajiri ambazo bado hazina wenyewe, kwa mfano ufugaji wa chura (tuna chura wazuri Mtwara for export),ziko pili pili mtama hapo Morogoro, kuna nyuki wasio uma hapo ktkt ya nchi hawana mtu,hapo Morogoro kuna samaki kafugeni,fungueni vituo vya huduma kwa watoto mitaani kwenu.

Kuna shule hazina walimu,kafundishe tuition,kila siku wanatangaza nafasi za Ma- VEO, mbona hamuombi. Moja ya matatizo ya ajira kuwa haba ni wote kubanana Dsm na miji mingine mikubwa, huku maporini tuliko wenzenu kazi ziko nyingi ajabu, hata vyeti havihitajiki huku vijijini, wewe njoo huku kijijini, anzia chini kisha upande kidogo kidogo.

Nina jamaa hapa wilayani alianza kama Revenue collector wa kata na sasa yuko halimashauri ndani ya muda mfupi, lakini alikubali kuanzia chini kabisa bila kujali vyeti vyake.
naomba nikuambie una upeo mkubwa sana tatizo wengi hawatak ilo, plz ni pm jina lako na contacts zako!
 
Kitu cha muhimu sana ni networking(kujuana) na experience kwa hiyo kama inawezekana kutafuta internship au part-time inayohusiana na unachosoma WAKATI BADO UPO SHULE ni vizuri sana.

Kama unachosoma ni kitu ambacho ni creative au rahisi kutengeneza mwenyewe bila funds kubwa ni vizuri uwe na portfolio ya vitu ulivyotengeneza kwa mfano kama ni programmer uwe na project zako ambazo umetengeneza, kama ni web designer uwe na site ulizodesign etc.

East Africa iko rich sana kwenye Archaeology kwa sababu ya Rift Valley, kuna eneo huko Kenya wameanza kuchimba akina Dr. Leakey mpaka leo wanachimba na hakuna dalili za kufikia mwisho, so usihofu sana.

ila acha dogo asome maana inaonesha amefanya tafiti za kutosha kuhusu hiyo archaeology,and more than ana connection na watu wanaodili na hiyo course.
 
mie naona sometimes we shld have to take risk for the others, hii inatokana na mfumo wa serikali yote hujajipanga vizuri,viongozi wanafanya kazi ya kujaza matumbo yao. ila tumewashtukia sasa,tushaanza kuweka mambo sawa kuepuka hicho chama chao tawala, so tunakwenda kubadilika kuanzia uchaguzi ujao 2015 hatutarudia tena makosa. Mie naona dawa ndyo hiyo tu.vinginevyo tutaendelea kuumia mpka wajukuu wetuwatachapika,au vip jamani?
 
C bora huyo wa archaelogy atleast ana uhakika wa kutoka,unakuta mkaka na misuli yake mingi eti anakomaa kusoma community development.,c ni heri mtu uishie zako form6 tu ukapge ishu zako than waisting your time.
 
sasa ndugu yangu telecommunication kweli ujiajiri???? kwanza angalau uajiriwe upate uzoefu wa kazi then ndo ianze michakato ya kujiajiri,hata ukiangalia walojiajiri kama hawa maktech,techmaster na wengineo kwanza walianzia kwenye makampuni kama TIGO,VODA nk
au wataka labda nijiajiri mpesa,au kuuza vocha????
 
sasa ndugu yangu telecommunication kweli ujiajiri???? kwanza angalau uajiriwe upate uzoefu wa kazi then ndo ianze michakato ya kujiajiri,hata ukiangalia walojiajiri kama hawa maktech,techmaster na wengineo kwanza walianzia kwenye makampuni kama TIGO,VODA nk
au wataka labda nijiajiri mpesa,au kuuza vocha????

hawakutakii mema hawa,yani na bachelor au diploma yako upige ishu za mpesa? Kwanza unatukana course uliyoisoma kwa hali hiyo.
 
Watu sio wanapenda kusoma course za education ila hali ya ajira inafosi.So angalia hali ya ajira kabla ujaanza course fulan unaweza ukasota miaka 6 kitaa
 
sio kujipa moyo.... Ndio ukweli huo. Nimeangalia future na nikapata ushauri kwa mtu anayefanya kazi ya Archaeology Arusha.

Dogo kaza msuli ili ujiandae kwenda kushinda makumbusho ukingoja elfu 80-100 per month.teh teh teh!
 
siku hizi kazi za kuajiliwa zinategemea mambo kadhaa kama haya:
1.bahati ya mtu.
2.ufaulu wa mtu.
3.uhitaji wa kozi uliyosoma.
4.kujuana.
zaidi ya hapo mkuu utasugua benchi sana mikuna ndugu yangu kamaliza degrii ya computer sayanyi ila bado yuko kitaa!

kaka hata siku hiyo nayo ni inshu sana,watu wanataka wew kama wewe unanini cha ziada zaidi ya ufaulu wako,yaani kunatatizo sana kwenye mfumo wa elimu yetu....
 
ina maana nyie wote mnaoalalamika hapa hamna kazi au ajira?...mmesomea kozi gani?/zipi?
 
ina maana nyie wote mnaoalalamika hapa hamna kazi au ajira?...mmesomea kozi gani?/zipi?

hata kama tunazo ila hazikidhi mahitaji yetu kaka.Ajira zipo nyingi sema watu wanazikwepa kutokana na kiwango fulani cha elimu,mf kuna kazi za ufundi geleji,kuosha magari na ukondakta hizi zote haziitaji darasa ni akili tu ya kawaida inaitajika kufanya hizi kazi,sasa kwa muhitimu wa chuo unataka akachezee tope kwa kusaka mahela?
 
Back
Top Bottom