Wahitimu wa Tanzania hamuajiriki

m ni mwitimu wa chuo kimoja hapa mchini kwetu.. nachoweza sema training tu mhitimu akipewa na organzation yoyote anapiga kazi.. hawa watu ni wahitimu kweli kweli na wana elimu, ila maisha yetu tu hapa nchini n stresfull sana.. ndo maana unaonekana haujui, umechanganyikiwa nk. wapen kaz wawe kama ninyi waongee nao
 
Jagaju umeongea kitu cha mana sana tena sana cjui kama namie ndo yananikuta ujue.
Una njaa kitabu utakisoma vipi
 
mmoja alinionyesha barua yake ya kuomba kazi nikamuonea huruma, nilijiuliza hiyo degree katolewa wapi hata format ya kuandika barua hajui.. Kuna basic skills ambazo ni a must mtu kua nazo, very basic qualities ambazo ilitakiwa kila mtu azionyeshe, mtu anatuma barua ya kuomba kazi anaandika tu ka story kafupi na matatizo aliyo nayo kwao, utadhani wewe kwenu ndo matatizo hakuna. Siwezi laumu wabongo wote though, najua kuna very good talents out there sema ni za kuhesabu.

Nadhani kuna tatizo mahali kwenye mfumo wa Elimu juu ya skill set, pia kujituma kujifunza.
Hivi iweje graduate ashidwe kuandika logical and sound applicatication letter? Tulifundishwa uandishi wa barua tangia STD IV!
 
Tunasema watz hawaajiriki, je hawaajiriki katika level zipi za kazi? Je katika sector zipi?Mbona NGOs nyingi ni watanzania haohao wanadeliver. Suala la muhimu ni kuwa na utaratibu kama nchi kuwapa wahitimu wa vyuo angalau nafasi za kujitolea kwa muda wa miezi sita had mwaka. Kulaani tu kuwa WTZ hawaajiriki kwa kuwa hawawezi kuandika kiingereza kizuri, hilo sizani kama ni kweli.
 
Huo ni ukweli usiopingika, katika mia labda mmoja.

Ukiwa na nia ya kuajiri Watanzania waliomaliza chuo, basi ujiandae tena kuwapa mafunzo ya kazi utayowaajiri kwa mwaka mmoja au miwili.

Kwanza lugha wanakuwa hohe hahe.

Mtu anakuja anakwambia nimesoma Business Management na ukitazama makaratasi ya uthibitisho aliyokuletea unakuta kasoma pia na IT ukimuuliza IT umesoma nini? anakwambia "excel", mpe hiyo "excel" mwambie haya chukuwa risiti hizi niwekee matumizi ya vitu hivi na unifanyie analysis vitu gani vinatugharimu sana. Utalia machozi, hajui hata aanzie wapi.

Kuna shirika lilinipa kazi ya ku assess wafanyakazi wapya waliomaliza "orientation" na walikuwa kwenye "probation" ili wajuwe nani wakumbakisha na nani wakumwachia akatafute kazi kwengine. Nililia na kucheka at the same time kwa kimbembe nilichokutana nacho.

Vijana walikuwa sita, wanawake wawili na wanaume 4.

Kila mmoja nilimpa barua ya mteja kaleta malalamiko, nikamwambia tunaomba muandike draft ya majibu mniletee, kuwa tunashughulikia malalamiko yake na tunaomba mkutano nae siku fulani ili tupange "way forward plan" na team yetu itakuwa na fulani na fulani na fulani na tungependa tuufanye mkutano nje ya mazingira ya kiofisi, tutagharamia lunch, watujulishe watakuja wangapi tunapendekeza tukutane hoteli fulani kuanzia saa tatu asubuhi mpaka wakati wa lunch.

Kazi ambayo walikuwa tayari wamefanyiwa orientation na wapo hapo kwa mwezi mmoja na nusu, haki ya Mungu nililia.

Wa kwanza kaja mwanamme, kama baada ya lisaa limoja, akanambia naomba kuuliza kidogo, nikamwambia karibu uliza tu. Nilishangaa! ananambia, mama naomba nisaidie, mimi hii kazi nnaihitaji sana kwetu kuna matatizo haya na haya na haya, kwa hiyo nisimwangushe na yupo tayari kugawana na mimi nusu kwa nusu mishahara yake ya miezi sita ya mwanzo.

Haki ya Mungu nililia machozi. Imagine a simple letter imemshinda kuandika na akaona aje kunihonga.

Wa Pili kaleta barua aliyoiandika, kaenda sijuwi kuchukuwa barua gani alijibiwa mteja akaikopi neno kwa neno akaniletea, haihusiani kabisa na nilichomwambia, yeye kaleta barua ya kuwaalika wateja kuhudhuria uzinduzi wa bidhaa mpya hoteli ya Serena. Nilibaki kucheka tu.

Watatu kaona isiwe tabu, kaja, kanambia Anti, mimi kazi basi, waambie mabosi nilishapata kazi kwengine.

Wanne na watano hawajarudi kabisa siku hiyo na wala hawajaleta nilichowaagiza, siku ya pili wamekuja kazini kama kawaida nikaita mmoja kwa boss wao kila mmoja kwa wakati wake wakanipa "identical Answer", kuwa "ala, kumbe barua ilikuwa inatakikana tukuletee jana" mimi sikujuwa na sijaanza kuitayarisha kwani nilikuwa na kazi zingine!

Wa sita, kajisikia vibaya kaomba kwenda kumuona daktari.

Hao ndiyo nguvu kazi ya Kitanzania. halafu tunauliza kwanini hatuendelei?
 
FaizaFoxy nakuheshimu sana lakini katika hilo ulilosema hapo juu naomba nikwambie kuwa umedanganya, huwezi kuniambia kuwa graduate sita eti wote wameshindwa kuandika barua kama hiyo. Ni kweli kuwa graduate wengi wa tanzania ni wabovu lakini si kwa kiwango hicho, yawezekana hiyo hali ni kweli ulikutana nayo kwa kiwango chake lakini si kwa kiwango hicho unachotaka kutuaminisha.
 
Last edited by a moderator:
FaizaFoxy nakuheshimu sana lakini katika hilo ulilosema hapo juu naomba nikwambie kuwa umedanganya, huwezi kuniambia kuwa graduate sita eti wote wameshindwa kuandika barua kama hiyo. Ni kweli kuwa graduate wengi wa tanzania ni wabovu lakini si kwa kiwango hicho, yawezekana hiyo hali ni kweli ulikutana nayo kwa kiwango chake lakini si kwa kiwango hicho unachotaka kutuaminisha.

Kudanganya si katika sifa zangu.

Nnakwambia nililia machozi na nilicheka at the same time.

Unashangaa hao sita? kuna wakati nimekwenda kuwafanyia assessment wafanyakazi waliopo kazini tayari kama 40 hivi wa kazi tofauti tofauti na wengine wapo kazini kwa miaka kadhaa, utashangaa nikikwambia 80% wakawa disqualified kwa sababu mbali mbali? usishangae, huo ndiyo ukweli.

Mwajiri ananiuliza nifanye nini? nikamwambiwa wa replace kidogo kidogo na wafanyakazi kutoka nje ya Tanzania. Akabaki kaduwaa.

Tanzania tuna matatizo makubwa sana ya waajiriwa, lakini sababu kuu mimi nnazijuwa, kwani moja ya kazi zangu nnazojifanyia ni hii ya ku assess "productivity" ya wafanya kazi. Nna uzoefu mkubwa sana.

Kama walikuwa graduates kweli au walikuwa wameghushi vyeti hiyo ilikuwa si kazi yangu kuchunguza hilo.
 
Inaonekana Employers hapa wao walikuwa graduates wazuri na wanaelewa kila kitu. Kumbe ni uzoefu na training mbalimbali ndio zinazowafanya sasa muongee hivyo. Je mnataka kusema kwamba baada tu ya kumaliza chuo direct mkawa waajiri. Naamini siyo hivyo na hususani baadhi yao nao waliwekwa tu kwakuwa kuna ndugu, jamaa, mpenzi au rushwa juu. But nakubali wahitimu wengi hawako strong enough.
 
m ni mwitimu wa chuo kimoja hapa mchini kwetu.. nachoweza sema training tu mhitimu akipewa na organzation yoyote anapiga kazi.. hawa watu ni wahitimu kweli kweli na wana elimu, ila maisha yetu tu hapa nchini n stresfull sana.. ndo maana unaonekana haujui, umechanganyikiwa nk. wapen kaz wawe kama ninyi waongee nao

Nakuunga mkono mkuu...mtu anaweza akaandika barua nzr sana kama mkuu moja alivyosema kuwa alimwambia mwenzake amsaidie..then kwenye training akachemka vibaya sana then what employer will do...hapa tunajaribu ku protect soko la kazi kwa vijana wetu..jaribuni kuwa train..maana hili suala la ukosefu wa ajira ni bomu linalosubiriwa kulipuka..tusiwadharau..bali tuwape msaada wa kutosha..sometimes ni stress zinawasumbua..mtu hajawahi kufanyiwa usaili na mzungu toka azaliwe anapanic maswali ambayo ni so simple..just common knowlege..anayaona kama hajawahi kuyasikia..let us help them..utasoma vitabu kama hujala?
 
wahitimu wengi wa Tanzania tunakosa kitu kinaitwa soft skills na maanisha communication skills,computer skills, innovation skills ndio vitu vinavyo tukwamisha katika soko la ajira tunaposhindana na wenzetu wa nchi jirani
 
FaizaFoxy nakuheshimu sana lakini katika hilo ulilosema hapo juu naomba nikwambie kuwa umedanganya, huwezi kuniambia kuwa graduate sita eti wote wameshindwa kuandika barua kama hiyo. Ni kweli kuwa graduate wengi wa tanzania ni wabovu lakini si kwa kiwango hicho, yawezekana hiyo hali ni kweli ulikutana nayo kwa kiwango chake lakini si kwa kiwango hicho unachotaka kutuaminisha.
Sita wachache hivyo? Mimi nime deal na graduates wa SAUT, UDSM, tena waliosomea journalism na mass communications kozi ambazo Uandishi ndio basis, Lakini zero. Unajua watanzania wanaamini vyeti siyo ujuzi na hii itatu cost sana.
Kuna mdada mmoja graduate yeye anajitapa tu.... Wai, mimi nina master yangu! Lakini performance siyo hata zero bali Pengine minus 50
 
Last edited by a moderator:
hahahahaha............ tafadhali FaizaFoxy naomba appointment ya kuonana nawewe. Naamini ombi langu litakubaliwa.
hahahahaha

Njoo Lumumba na Udoe, jengo jipya lililogandana na ofisi za CCM za Mkoa, ghorofa ya tatu, siku ya kuonana na watu wa appointment nisiowajuwa ni Jumanne tu. Ukiulizwa unataka "kumuona na nani?" wape code 323X, code hiyo itatumika mara moja kwa mtu mmoja tu na itatumika siku ya Jumanne yoyote ya mwezi April 2015 tu.

Kazi kwako.
 
Kuna Kitu kimoja kinatumaliza Vijana(wengi wetu) wa Kitanzania, Hatujawahi kuwaza kujifunza vitu tofauti tofauti, Muda wetu mwingi tunatumia Whatsp, Facebook na Mitandao mingine. Laiti kama tungalitumia kusoma vitabu au kujifunza vitu tofautitofauti mimi naamini tungebadilisha sana Maisha yetu.
Niliwahi kufanya Online Aptude Test za Kpmg, Pwc na Delloite. Kpmg walitaka kupima IQ ya mtu, Pwc walipima Knowledge and Decision Making, Delloite walipima Ujiniazi. Kwa hiyo kama wewe siyo mtu ambaye anataka kujua what is going on in the world in current issues and professionals lazima wakuache. Swali moja niliulizwa(2011) PWC eti hivi hapa Tanzania kuna kitu gani kinaendelea? Kwa vile nilijiandaa nikajibu ni Bajeti! wakaniuliza Bajeti ya Nishati unaionaje?

hapa namaanisha nini sasa, kwa ambaye anatafuta kazi Jitahidini sana kuandaa document zenu vizuri:
1.CV-Lazima ireflect kazi unayoiomba
2.Application/cover letter-Lazima ieleze wewe ni nani na kwa nini wewe upewe hiyo nafasi
3.Vyeti relevant-

kila kitu kipo google
 
dah.. hv n barua ya aina gan ntakayoshndwa kuandika.. labda barua ambayo sijawh kuisikia wala kuiona lakn ntahtaj maelezo tu ya msing naandika.. tatizo mtanzania akijua kitu bas atadharau sana wenzie kwamba hawajui.. zc z bu*sht
 
hv huyu faizafix n raia wa wap..? kama n mtanzania huna haki ya kudharau elimu yetu kiasi hiki! kisa kujua kuandika aina ya vibarua.. wapo wanaojua zaid yako hawaongei.. mi natamani npate chance ya kuasses uwezo wako someday..
 
Nchi yoyote ulimbukeni. Huko nchi nyingine nako wenye kuandika barua za ovyo wapo wengi tu na pia wanapata shida kuajiriwa.
Ila watanzania walikubali KUSOMA NA KUJIFUNZA kweli hapa Tz tupo juu sana na ndio tegemeo huku tulipo. Tunawabeba sana hao yes sirrrr.
Kiingereza kiiingi mipango ya ovyo haitekelezeki kila siku wanaelezea failures kwa maneno badala ya kuonyesha mafanikio yanayoshikika.
Tunawaona sanaa tu. Masuti, vimini, maelezo mazuuuri ya boardroom. Ma odeas mazuri toka nchi zingine. Na wanajua sana kuwateka roho hawa wawekezaji. Tunaona sana. Ikifika kwenye kazi sasa ndio sheeeda.
Watanzania tuko juu tuache kujinyanyapaa.
Shida yetu ni kujijua mtu ulipo na utajitoaje hapo.
Kwa uhakika ufaulu wa PASS au C haukufikishi mbali sana.
Pia kujua ni wachache wetu ambao ajira za kutoka wawekezaji wa nje zitatusaidia.
Wengi tutatoka kitanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom