JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,556
- 18,423
Ukikaa mtaani na wale vijana wa chini kabisa,ambao wengine hata kidato Cha nne hawakufika, utashangaa,Sijui fani nyingine ila nina watu wangu wengi waliosomea hii fani wengine nilisoma nao O Level wengine shule ya msingi, marafiki na pia ndugu zangu.
Wengi nawaona wanasota nyumbani tu. Sijui hii fani imekumbwa na nini kipindi hiki.
Mtaa ninaoishi Kuna vijana Hawa Kwanza ni madereva wa bodaboda, pili ni mafundi ujenzi,bomba,wengine,wataalamu wa kuweka Tiles.
Yupo mmoja huu ujuzi Kwanza alifundishwa na kaka yake,then akaenda kusomea VETA,huo mtaa mzima ndie fundi bora anaye kubalika katika kuweka mfumo wa mabomba kwenye nyumba,kujenga chemba za vyoo,na vile vile ni dereva wa bodaboda,anafamilia na ameweza kujenga nyumba yake ya kawaida tu.
Mwingine ni kijana alitoka Iringa,akaja Dom,kwa kazi nzuri za kuweka Tiles,anazofsnya,anapata kazi nyingi,mpaka mikoa mingine.
Kwanini wenye "degree"hawawezi hivi vitu(sio wote lakini).
Kuna haja ya kuwafanya vijana wetu wafanye hizi kazi ndogondogo,Kwanza wao tayari Wana msingi wa elimu kubwa,wakiweka nia hizi kazi wanaweza kuzipiga ki uhandisi zaidi,mambo yakawa poa.
Nilienda Zenj,nikakutana na vijana waliotoka huku bara,wapo Zenj wanafsnya kazi za umeme wa majumbani,Kuna wakandarasi wakubwa,wanachukuwa tender,then wanawatumia Hawa vijana na vibarua wao kufanya hizi kazi.
Pesa wanayopiga,acha kabisa,jamaa alinionyesha apartments ambazo anafanya kazi,kazi ikiisha atakuwa ana 99Millioni cash!
Kwa jinsi kazi zilivyonyingi,hakosi 5M!kwa mwezi!!
Wakati huo Mimi Na Degree yangu nimekomaa na ajira!ya laki 8,Kwa mwezi! Kuna sehemu wasomi tunschemka,sio kwamba hatuna ujuzi!!tatizo ni mtazamo,fikra zetu vichwani,Miundombinu ya kuweza kufanya yale tuliyoyasomea ki engineer zaidi,kwenye ofisi,viyoyozi,mshahara mnono,kwa sasa hv ni changamoto,then what!lazima tuanzie chini!!
It's do or die