Wahitimu wa civil engineering wanasota mtaani, siamini macho yangu

Wahitimu wa civil engineering wanasota mtaani, siamini macho yangu

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,727
Reaction score
13,466
Sijui fani nyingine ila nina watu wangu wengi waliosomea hii fani wengine nilisoma nao O Level wengine shule ya msingi, marafiki na pia ndugu zangu.

Wengi nawaona wanasota nyumbani tu. Sijui hii fani imekumbwa na nini kipindi hiki.
 
Faza miradi yote inaratibiwa na TBA na humo ndimo walimokuwa wakitegemea kwa asilimia kubwa, nyumba za watu binafsi sasa hivi ni chache mno zinazojengwa kiasi cha kuchukua kampuni ya ujenzi kuja kukujengea.


Nguvu ya Manunuzi imeshuka pakubwa mnoooo! Kila siku inazidi kupungua huku ukata ukichukua chati kwa spidi ya Ajabu
2664467_A6CBFDF1-1CD9-4EEF-923F-DA0C3036A007.jpeg
 
Faza miradi yote inaratibiwa na TBA na humo ndimo walimokuwa wakitegemea kwa asilimia kubwa, nyumba za watu binafsi sasa hivi ni chache mno zinazojengwa kiasi cha kuchukua kampuni ya ujenzi kuja kukujengea.


Nguvu ya Manunuzi imeshuka pakubwa mnoooo! Kila siku inazidi kupungua huku ukata ukichukua chati kwa spidi ya AjabuView attachment 1694892
Duuh hapa naona TBA kashika kila kitu hata kule kigoma Jafo alikuwa anawalaumu hawa nadhani kwa kuchelewesha kukamilisha mradi.
TBA wapo kila kona
 
Duuh hapa naona TBA kashika kila kitu hata kule kigoma Jafo alikuwa anawalaumu hawa nadhani kwa kuchelewesha kukamilisha mradi.
TBA wapo kila kona
Kuna jamaa yangu ni Architect nilimuonesha hii kitu akaishia kutikisa kichwa tu. Yeye mwenyewe imembid aache kazi alikokuwa ameajiriwa sababu ana mwaka analipwa nusu mshahara na kuna vitu kibao vimepunguzwa ofisi haina pesa haina kazi.
 
Sijui fani nyingine ila nina watu wangu wengi waliosomea hii fani wengine nilisoma nao O Level wengine shule ya msingi, marafiki na pia ndugu zangu.

Wengi nawaona wanasota nyumbani tu. Sijui hii fani imekumbwa na nini kipindi hiki.
Yani weww na wao pia ni watu mnao amini kupata kupitia ajira,kwamba ulisoma sasa lazima ufanikiwe kupitia mawazo ya wengine(ajira). Hamuoni kwamba mnachemka?
 
Wazazi ndo wanaumia kuliko hata hao wahitimu.

Unamsomesha mwisho unaanza tena kumpa hela ya vocha.

Inaumiza.
Nchi bado inahitaji ma engineer wengi tu,msiwavunje moyo jamani Mambo yatakaa sawa tu.lakini pia kutanua wigo wa kimawazo Ni muhimu,nchi Kama Sudan,Mozambique,Zambia,zmbabwe,Malawi zhauhtji kwa watu ccivil Sana tu,ukitua huko hawakuachi mkuu.watanue mipaka.
 
Kuna jamaa yangu ni Architect nilimuonesha hii kitu akaishia kutikisa kichwa tu. Yeye mwenyewe imembid aache kazi alikokuwa ameajiriwa sababu ana mwaka analipwa nusu mshahara na kuna vitu kibao vimepunguzwa ofisi haina pesa haina kazi.
So sad mkuu. Katika watu ambao tulitegemea waenjoy awamu ya 5 ni hawa wazee wa civil sababu jamaa anapenda sana miradi ya ujenzi.

Shida inakuja hataki kushirikisha sector binafsi ambazo zinatengeneza sana ajira kwa wahitimu.
 
Ukikutana na mtu anakwambia eti graduate wa Civil Engineering ajiajiri mchape makofi. Unaanzaje kujiajiri wakati mtaji hata wa milioni 30 huna? Mtu kasoma kwa mkopo unamwambia ajiajiri kwa mtaji wa mamilioni ya pesa.

Kwanza miradi yenyewe ya kuajiri iko wapi. Hata kukodisha mitambo ni gharama kubwa kuliko uwezo wa watu wengi. Malipo yenyewe yanacheleweshwa ufanye kazi leo ulipwe miaka miwili mbele wakati kampuni ndio inaanza.
 
Yani weww na wao pia ni watu mnao amini kupata kupitia ajira,kamba ulisoma sasa lazima ufanikiwe kupitia mawazo ya wengine(ajira). Hamuoni kwamba mnachemka?
Kuna watu mkisha shiba mnaanza kuona wengine km mapimbi.

Katika nchi za dunia ya tatu serikali ina role kubwa ya kutengeneza ajira hata kwa multiplier effect sio lazima moja kwa moja sababu wananchi wake hawana vipato vya kutosha kuweza kutoa ajira kwa watu wengi.

Wananchi wanaojenga kwa kutumua makampuni ya ujenzi ni wachache sana hivyo ni muhimu serikali watoe kazi kwa makampuni ya ujenzi ili nao watoe ajira kwa vijana lakini serikali sasa wanafanya kila kitu wao.

Unategemea Civil engineer akapige koleo kwa mchina amwage zege mana ndio ajira za mchina hizo.
 
Hata hao wachina mnaowasifia wanapewa mitaji kwao kwa mikopo nafuu ndio wanaweza kufanya projects hizi wanazopewa. Utashangaa watu wanakaa bungeni na kusema vijana mjiajiri wakat hata mikopo nafuu hakuna wataenda kumwaga zege site?
 
Back
Top Bottom