Bahati ni kwamba sasa tumepata angalau kiongozi mwenye maono ya kuweza kuona tatizo kutokana na hawa wageni/raia wenye asili ya kihindi. Kwa muda mrefu tunasikia mambo mengi wakiyafanya ambayo hayana maslahi na taifa hili. Uchaguzi mkuu unapokaribia ndio wa kwanza kupaki vitu vyao na kukaa mkao wa kuondoka. Ndio maana wamejazana kwenye majumba ya msajili na wako tayari kutumia gharama yoyoye kupata nyumba hizo. Sasa watakuwa na amani maana NHC imejenga nyumba za kutosha.
Tumesikia kuhusu ishu ya IMTU kipindi kile ambapo walikuwa wakitumia miili ya binadamu kufanyia mazoezi kwa vitendo na kisha kwenda kutupa viungo huko kwenye machimbo ya mchanga, kamaunaenda Tegeta. Karibuni tumesikia tena ishu ya vyuo vya St Joseph ambapo wanafunzi wanalalamika sana kuhusu huduma mbovu zinazotolewa na vyuo hivyo kuanzia elimu, malazi, hadi nidhamu. Serikali imeamua kuingilia kati na isiishie tu kuhamisha wanafunzi bali ihakikishe inawapa somo hawa wenye chuo.
Kadhalika tumesikia tena kuhusu huko Dangote ambako waswahili wananyanyaswa sana na wahindi. Serikali yetu tukufu isifumbie macho suala hili. Tunahitaji uhuru wa kweli na heshima kwenye nchi yetu. Hawa ni wa tu wa kupita tu na wao wanajua. Hii nchi isiwe shamba lililokosa mwenyewe. Wahindi wameshikilia uchumi wa nchi hii pale ambapo sekta binafsi inahusika. Wanatumia fursa hii kuwapelekesha watanzania kwa namna wanavyotaka.
Tumesikia tena kuhusu huko Minjingu ambapo wafanyakazi wanalalamika kuhusu mikataba na mishahara yao. Minjingu inamilikiwa na makalasinga. Tunataka tufike mahali wageni waiheshimu Tanzania, waheshimu na watanzania. Na ifike mahali pia mgeni ajiulize mara mbili mbili kama kweli anataka kuja Tanzania ikiwa hana uhalali wa kufanya hivyo
Weka akili yako katika mazingira bila ya kiroba halafu fikiria bila ya hawa...kujitahidi kuchukua risks za kibiashara na wakaweza kuajiri bguguzo wengi hali ingekua vipi?
zaidi ya mengi sioni mtu serious anaye wezakujotolea kuchukua risks za kufungua viwanda na biashara kubwa
hawa wamei saidia sana nchi hii kuliko wewe baba ako na babu zako wakichanganywa kwa pamoja
nyumba za NHC ni za mababu zao zilitaifishwa hazija jengwa na ccm wala serikali
leo lifikirie jiji la Dar tu peke ya..Samora...,
azikiwe
mnazi mmoja
ohio
bibi titi
sokoine
kariakoo
masaki--
msasani
changombe viwandani
nyerere road viwandani
mbezi viwandani
kila kona haa jamaa wamechukua risks na ku invest ili wewe upate kazi na serikali ipate kodi
Maadam umeleta ubaguzi na mimi nakumalizia kwa ubaguzi ..wewe kama mwafrika mtanzania umefanya nini kuwasaidia wwenzako wapate kazi ? wewe au wengine wamefanya kiasi gani kusaidia wenzao wapate kazi au kodi ?
waafrika wengi wakipata watafungua bar au sehemu ya disco..wachache sana walosoma wenye mawazo kama ya wahindi ndio wanafanya kweli..hawa ni kina mengi ambao wenye wameajiri wahindi kibao..
kwa ufupi usichukulie makosa ya hapa na pale ukajamba ubaguzi...wahindi ni raia wa nchii hii wamefanya mengi mnooooo kuliko hata wafrika kwa ujimla wao..
wamekujengea Muhimbili hospital
walikujengea first jengo la bunge
majengo ya mwanzo mengi yalio kuwa na ofisi za serikali ni ya wahindi yalochukuliwa
wahindi ndio walokuja kujenga reli hii ya kati....walitoka kwao kama manamba na kuja kuijenga kutoka Dar mpaka Kigoma..wajerumani walikua na nyinyi hapa lakiki aliona mna kasoro akachukua manamba wa wakihindi
hata mchina alipo jenga tazara alileta wafungwa waki china kibao..na juzi uwanja wa Taifa..
wacha maneno ya kijiweni kama hujui mjii huu na nchii hii nani ameifikisha kimaendeleo angalau hapa ilipo...
sasa safiri uende Tanga
Mwanza
tabora
znz
arusha
moshi mjini
kila sehemu ya town hali ni hio hio ..wamefanya mengi..na uchache wao lakini walofanya ni zaidi ya wewe ulofanya na wenzako..WACHA UBAGUZI