Zamiluni Zamiluni
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 13,996
- 15,118
Shukran ndugu.. umemaliza yote "tunahitaji kubadilika" !!Asanteni mada ya wahindi sikuwa mwanachama lakini mada imenigusa nimejisajili na maoni yangu: Mimi nimechanganya mhindi, mbulu na mzigua. Nimelelewa na bibi mhindi. Jamani no nidhamu nidhamu nidhamu. Nilifundishwa na bibi kuwa mwanamke u we mbunifu mwanamke ujitume mwanamke lazima ufiche akiba iko siko mume atakosa. Mchana hatukuruhisiwa kulala tulipika maandazi, tulitwanga hina n.k. wali ukibaki tunaanika na siku pesa hakuna tunakaanga na kunywa na chai. Mhindi hata mzee atafanya shughuli yeyote ile. Mhindi hafanyi kufuru ya pombe wala chakula na hata siku moja hutaona wakitupa chakula. Mhindi hajazi ndugu ndani ya nyumba waliokaa bure wakitegemea kaka a shemeji no aibu na matusi makubwa sio wenye nyumba wameamka kutafuta riziki wewe upo unakunywa chai ya bure kisha kwenye TV unabadilisha channel. Mhindi akichukua mkopo anaotakiwa kulipa tarehe 1, tarehe 25 mhindi amesharejesha. Kweli wapo wanyanyasaji lakini pia inakera mtu 1 hr ofisini anakunywa chai, kazi ya dakika 30 inachukua masaa 3, kill kit no matayarisho Jamani unajijua uta retire a utazeheka je mwili umeutayarisha? Akili je, akiba je? Mhindi akipata 10,000 atatumia 4000 anajua kupata sio kila siku. Wahindi wana mema yao na waafrika mema yao ni wana imani, wanasaidiana na pia kulemazana. Hivyo wote wanahitaji kubadilika. No mengi ya kusema mhindi hachezei pesa eti vikao au mchango wa harusi nje ya uwezo ajili ya show off hakuna kitu kama hicho Jamani ni mhindi na ni muafrika I am proud of both especially nikiitwa mbulu sijui mtanihukumu vipi. Na kuna maarifa mengi sana kuhusu maisha. Thank bros and sisters kama nimekosea kumradhi
God Bless Tanzania