Wahindi wanaonewa sana kuitwa Wahindi

Wahindi wanaonewa sana kuitwa Wahindi

East African Eagle

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2013
Posts
3,759
Reaction score
2,209
Tanzania ina watu wa aina mbalimbali na makabila mbali mbali lakini huoni kwenye vyombo vya habari mtu akitajwa kwa kabila lake au rangi yake.Wahindi ni watanzania kama ambavyo wengine ni watanzania.Kitendo cha kuwabagua na kuwaita wahindi ni uonezi mkubwa tena sana.Waitwe watanzania tu basi.
Hivi kwa nini mtu ang`ang`anie kuwaita wahindi hawa watanzania wenzetu raia wa Tanzania?

Na baadhi yao wanaojiita wahindi wakome kabisa kujiita wahindi.Wahindi wako india sio tanzania.Tanzania ni ya watanzania.
 
Na wewe ukiwa India tutakuita muhindi.sawa boss
 
Siku zote usimuite mtu kwa rangi au kabila. Nimejifunza mengi sana. Nimejifunza wapi??

Singapore: Ni nchi iliyotokana na mchanganyiko wa watu mbalimbali kama wahindi, wajapan, wazungu. Shule zao hazina kubagua. Hazina shule za wenye uwezo au wa rangi Fulani. Mwisho, wanaaminiana na wanasonga mbele sana ukilinganisha na mataifa mengine ya Asia. Hii ipo hata Hong Kong.

Marekani: Hii ni nchi yenye kuzalisha watu wenye ubaguzi wa hali ya juu. Tunaweza angalia sasa ukafikiri watu weusi ndo wanabaguliwa. Hapana. Hata weupe wanabaguliwa sana. Wanachoangalia ni kipato, rangi na asili yako. Huwezi kupeleka motto shule za wenye nazo. Hii imetokea hata kugawa watu "African-American, White, Spainic, nk. Sahizi matokea tunayaona ndo haya ya kuchoma nymba na makanisa ya weusi.

Katika ubaguzi kama huu, wametumia hata kugawa dunia kama sS-Africa, North Africa, Middle East, nk. Hawa ndo wanongoza.

Tujifunze haya: tukiwatambua watu kwa dini na rangi mwisho tutatengeneza kundi la kuchukiana baadaye. Hasa kuonyesha kwamba kuna makundi yametufanya tuwe masikini.

Nyerere ameliongelea hili. Pangekuwa hakuna kusajili watu kwa makundi huko USA, naamini kungekuwa na mtangamano mzuri kabisa wa makundi yote. Mpaka Obama akasema 'we are not free of racism DNA'.

Naona serikali yoyote amabyo inajua inafanya nini ingepunguza haya mambo hasa katika ajira za serikali. Wahindi ni wachache sana.
 
Tanzania ina watu wa aina mbalimbali na makabila mbali mbali lakini huoni kwenye vyombo vya habari mtu akitajwa kwa kabila lake au rangi yake.Wahindi ni watanzania kama ambavyo wengine ni watanzania.Kitendo cha kuwabagua na kuwaita wahindi ni uonezi mkubwa tena sana.Waitwe watanzania tu basi.
Hivi kwa nini mtu ang`ang`anie kuwaita wahindi hawa watanzania wenzetu raia wa Tanzania?

Na baadhi yao wanaojiita wahindi wakome kabisa kujiita wahindi.Wahindi wako india sio tanzania.Tanzania ni ya watanzania.

Kwanini wewe uwasemee?,kwani wao hawawezi kujisemea?,au ndo kujikomba kwao!.
 
East African Eagle

Tatizo la wahindi wabongo wanajitengenezea wenyewe uadui na sisi. Sawa, tuseme wote sisi ni watanzania kwa nini wananyanyasa watanzania weusi na kuwapendela watanzania wa kiasia kwenye maofisi na majumbani kwao? Kwanini hawataki kublend in na watanzania wenzao na kupendelea kuendeleza tamaduni na miiko ya kihindi wakati hawajawahi kukanyaga hata INDIA? kuna wahindi hata Kiswahili hawajui wakati maisha yao yote wamekulia bongo. Utamuita mtu kama huyo mtanzania? Sipendi ubaguzi lakini hatuwezi kuwaachia watubagui lazima tukemee tabia hizi.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mleta uzi kuchemsha sana..hilo ndy tatizo la kupinga kila jambo ona mpaka yeye anajipinga hahahaahaha
 
Back
Top Bottom