Wahariri wapuuza agizo la viongozi wa TEF

Wahariri wapuuza agizo la viongozi wa TEF

Sasa waondosheni hao tuwawekee Makada na msijute baadae.. hii mbinu ya kususa Tunaomba muendelee nayo hadi mkomae kamuulizeni Seif.

Mwanaume hupambana hadi mwisho na huitwa Shujaa
 
TEF wao ndo walikuwa wamekosewa !? Wanavyo vyombo vya habari wanamiliki ?....kwa sababu wameigeuza issue binafsi dhidi ya makonda aibu haiko mbali nao


Hapana, TEF ndio walikuwa wamemkosea Makonda, that is according to TEF wenyewe. Mwenyekiti wao Mzee Makunga kasema anaomba msamaha!

Mwandishi mmoja akamuuliza kwa nini TEF inaomba msamaha? Ilikuwa ni makosa kum ban Makonda? Akagwaya, hakujibu!

Makamu Mwenyekiti Balille nae has lost his marbles. Anatueleza habari ya mtoto wake anaelekea chuo. Anasema uchunguzi ulisikiliza upande mmoja. Wakati ni yeye ndio aliandika ripoti na ni yeye aliyeitetea na kueleza kwa nini ilikuwa ya upande mmoja.

Ushaona wapi duniani Mwenyekiti wa Tume anaipinga hadharani ripoti yake mwenyewe? Kadata na yule Balile.

Katibu, Meena, ndio alikuwa kidume chenye brass balls. Aliuona uozo wa TEF wenzake na hakujiuma-uma. Tatizo alipochemka ni kumtaka Makonda aombe msamaha wakati walipokubaliana behind closed doors hakukuwa na concessions za kuombana misamaha! Ikabidi Makonda ateke nyara press conference, akawafunika wooote!
 
Hahahaaaa.. Kazi ipo Mungu huyu tunaemtania kila mara.. Kunasiku yaja maana huwezi kumuhusisha Mungu katika,kuenenda katika njia isiyokubalika
 
TEF wao ndo walikuwa wamekosewa !? Wanavyo vyombo vya habari wanamiliki ?....kwa sababu wameigeuza issue binafsi dhidi ya makonda aibu haiko mbali nao

Halafu rafiki angalia tu wasije wakakupima UTI
 
Hahahaha, kwa kweli Tz kuna vituko. Naamini wapo wenye weledi na maadili ya uandishi. Mengi na ITV wanaugomvi na Dkt Magufuli kwa sababu mtu wa kaskzini alishindwa urais, watu wa kazkazini wana chuki na serikali ya awamu ya 5 kwa sababu waliamini eti wao ndiyo wenye haki miliki ya kuiba na kutawala nchi hii, watu wa kazkazini ndiyo wanaongoza kwa kuiibia/kufanya ufisadi, na ndiyo maana sehemu kubwa unakuta wameendeleza makwao, leo hii tumepata rais anayetuunganisha then watu mnaanza kuleta unafiki. Watu wa kazkazini mpaka wachungaji/manabii ili mradi tu wake zao wanatoka kazkazini basi nao wameingia kwenye mkubo. Hakika system haitakuja kuwaacha salama watu wa kazkazini.

Kama wewe ni muelewa huu ugomvi kaa mbali, acha system ifanye kazi ili kuleta usawa, hatutaki mambo ya wakikuyu hapa Tz, lazima nchi hii kila kabila liwe na haki ya kutawa, tuna hitaji kuchagua viongozi wetu kulingana na sifa, na siyo kuchagua kwa sababu eti lowasa anatoka kazkazini, na siyo eti ITV wanamuonesha lowasa sana kwenye kampeni kwa sababu ni wa kazkazini. Kaeni mjitafakari sana!
Mudawote nimeona aibu wakati nasoma post yako. Bila shaka hujielewi, una chuki binafsi , umekata tamaa ya maisha na kwakweli ushauri mzuri ni wewe kupambana na hali yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana, TEF ndio walikuwa wamemkosea Makonda, that is according to TEF wenyewe. Mwenyekiti wao Mzee Makunga kasema anaomba msamaha!

Mwandishi mmoja akamuuliza kwa nini TEF inaomba msamaha? Ilikuwa ni makosa kum ban Makonda? Akagwaya, hakujibu!

Makamu Mwenyekiti Balille nae has lost his marbles. Anatueleza habari ya mtoto wake anaelekea chuo. Anasema uchunguzi ulisikiliza upande mmoja. Wakati ni yeye ndio aliandika ripoti na ni yeye aliyeitetea na kueleza kwa nini ilikuwa ya upande mmoja.

Ushaona wapi duniani Mwenyekiti wa Tume anaipinga hadharani ripoti yake mwenyewe? Kadata na yule Balile.

Katibu, Meena, ndio alikuwa kidume chenye brass balls. Aliuona uozo wa TEF wenzake na hakujiuma-uma. Tatizo alipochemka ni kumtaka Makonda aombe msamaha wakati walipokubaliana behind closed doors hakukuwa na concessions za kuombana misamaha! Ikabidi Makonda ateke nyara press conference, akawafunika wooote!
Mkuu Tindikali. Hivi unafahamu Meena na Mzee Makunga wanafanyakazi wapi? Meena alikuwa Mhariri Mtendaji Tanzania Daima lakini ninafahamu kwamba kwa sasa hayupo (mkataba wake ulikatishwa/aliukatisha au uliisha akasepa au kusepeshwa). Mzee Makunga alikuwa Mwananchi, sina uhakika kama bado yupo lakini ninachofahamu nafasi aliyokuwa nayo Mwananchi iko na mtu mwingine. Nina shaka kama bado yupo, hisia zangu zinanituma kuwa hayupo Mwananchi. hata kama yupo basi ni kwenye nafasi ambayo "haishibishi." Hawa wawili nathubutu kusema kwa sasa wanaishi kwa kuitegemea TEF. Mashirika na taasisi mbalimbali zinapowapeleka TEF kwenye mahoteli makubwa makubwa kwenye yale yanayoitwa mazungumzo baina ya "wahariri na mashirika au taasisi hizo" fahamu kwamba viongozi wa TEF na wahariri mifuko yao hutuna.

Balile kwa kushirikiana na Manyerere, enzi za akina Lowasa walipokuwa wakipambana kumuingiza madarakani, nao walikuwa wakipambana kupata mtaji wa kuanzisha gazeti la 'Jamhuri'. Walifanikiwa baada ya 'kupambana' kwa namna ambayo sina uhakika sana kama wanaweza kuieleza hadharani. Gazeti la 'Jamhuri' linaendeshwa kijanjanja kwa kuuma na kupuliza. Ni wasaka matangazo! Ukishangaa ya Balile kuipinga ripoti yake mwenyewe, utafanya nini kwa Manyerere (naibu wa Balile) kuomba matangazo Ikulu mbele ya Rais wakati wenzake wakiuliza maswali yenye maslahi mapana kwa taifa!

Mtu yeyote ambaye anafikiri TEF wanaweza kuwa na msimamo endelevu wenye kulinda heshima ya taaluma ya habari, kwenye jambo lolote sio tu hili la Makonda, atakuwa anapoteza muda wake bure. Hata kama malengo ya TEF ni mazuri, lakini kwa sasa chombo hicho kipo katika mikono isiyo salama.
 
Mkuu Tindikali. Hivi unafahamu Meena na Mzee Makunga wanafanyakazi wapi?

Okay, fine, kwa hiyo hawamiliki magazeti, hawaandiki gazeti lolote, na hawauzi gazeti. Hawana economic interest yeyote ya kumlamba miguu Makonda, walitakiwa waitetee TEF.

But again, mimi sina tatizo na Katibu Meena, at least ameonyesha msimamo. Mwenyekiti na Makamu ndio waliwauza wenzao. Meena anafaa kuchukua hatamu za TEF. Makunga amechoka, ajiuzulu. Unakujaje pale kusema TEF ndio wanaomba msamaha, huna aibu?

This was a brokered peace agreement. Mnamaliza uhasama kwa makubaliano, sio kwa mmoja kusema nilikuwa njia panda nimeshukiwa na roho wa Bwana kanambia nitubu kama Mtume Paulo, hapana! Halafu mnakuja mbele ya hadhara kusema yale mliyokubaliana, huwezi kuleta jipya pale eti Makonda omba radhi. Au kama Mwenyekiti alivyosema TEF wanaomba msamaha, you crazy?
 
Back
Top Bottom