TUHUMA ZA RUSHWA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA.
Jukwaa la Wahariri, TEF ni miongoni mwa Taasisi nchini ambazo weledi wake ulipaswa kuwa ndio kiini cha utendaji wa tasnia ya habari. Hali hiyo haipo kwa TEF ya Mzee Theofili Makunga baada ya taarifa kusambaa kuwa Kamati ya utendaji wa jukwaa hilo imejikuta ikishindwa kuelewana kutokana na baadhi ya wajumbe kutuhumiwa kupewa rushwa na Mkuu wa mkoa wa Dar na kumsafisha tuhuma zinazomkabili kuvamia kituo cha Radio.
Kwa wale wasiofahamu Mwenyekiti wa TEF, Ndugu Theofili Makunga amepewa rushwa na Makonda ili kuhakikisha kuwa mkutano ulioitishwa siku ya leo unamsafisha RC na kuifanya kamati iliyoundwa na Mh Nape ionekane ina Makosa na mapungufu makubwa katika kuchunguza tuhuma za uvamizi alizozifanya siku chache zilizopita katika kituo cha Habari cha Clouds Media.
Na ndio maana hata mjumbe wa Kamati hiyo Neville Meena amelalamika kutokuwepo kwa ushirikiano kwa baadhi ya wajumbe wa jukwaa la Wahariri.
Aidha, baada ya waandishi kuuliza maswali kutokana na sintofahamu ya kutokujua nini hasa lengo la mkutano wa leo, Waandishi walishikiza Makonda aombe radhi mbele ya waandishi wa Habari na watanzania kwa ujumla badala yake kauli ya msamaha ilitoka mdomoni kwa mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri ndugu Theofili Makunga ambaye Alisema dhamira yao inawasuta na hawaoni haja ya kuzuia kuandika habari za Makonda ndipo ukumbi mzima ukaanza kuguna kutokubaliana na alichokisema mwenyekiti huyo.
Niwasihi waandishi wenzangu wenye weledi na tasnia hii ya habari msiingie kwenye mtego huu wa panya. Watanaswa na wasiokuwemo.
Naamini TAKUKURU wanafuatilia kwa karibu tukio hili. Hakuna linalofanyika gizani TAKUKURU wasilijue. Naamini kuwa wanaendelea kuchunguza miamala ya kibenki ya na kwenye simu ya Wajumbe hao wa Jukwaa la habari Tanzania (TEF) ili kubaini kiasi cha fedha waoichopata ili kumbeba Makonda.
Kinachotakiwa kufanyika ni kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za TEF Mh Makonda alipaswa kuomba radhi Kwa tuhuma tu zinazomkabili ni sababu tosha za yeye kuomba radhi.
TEF inakosa credibility ya kuendelea kusimamia jukwaa la habari kwa kitendo cha leo kutokana na mgawanyiko uliopo na hizi tuhuma za Rushwa.
Nashauri Mwenyekiti wa Kamati ile ya Mh Nape Nnauye, Ndugu Deo Balile aachie ngazi mara moja kwa kushindwa kusimamia msimamo wake wa awali pamoja na wajumbe wote wa kamati wamepoteza sifa za kuendelea kusimamia jukwaa la wahariri.
Nashauri Wajumbe wengine wateuliwe haraka iwezekanavyo ili wasimamie Jukwaa hilo.
Nawasilisha.
Mhariri Gazeti la Rai.
Sent using
Jamii Forums mobile app